Monday, August 05, 2013

PEPSI WAIPA YANGA KIBURI...!!!



056 8dc84
Sakata la Yanga kugomea udhamini wa Azam Tv limechukua sura mpya baada ya klabu hiyo kutaka kupewa kitita cha Sh600 milioni ili kukubali kudhaminiwa na Azam. (HM)


Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa, Yanga wamepata kiburi cha kugomea udhamini wa Azam baada ya kuwa na ofa mbili mkononi ya Pepsi na ile ya Zuku.
 

“Pepsi wanatoa kinywaji chao kipya Pepsi Cola na wametupa ofa ya Sh600 milioni, Azam walifuatwa na kuelezwa juu ya ofa hiyo wakakataa Pepsi wasiingie kwa vile ni wapinzani wao kwa Azam Cola,” kilisema chanzo cha habari.

Chanzo hicho kilisema kuwa, Yanga waliwapa sharti Azam la kuongeza dau kutoka Sh100 milioni na kama isingewezekana basi waingie mkataba na Kampuni ya Pepsi.


“Hiki ni kinywaji cha Pepsi ni kipya na wanataka kukitangaza kupitia Yanga, Zuku nao wametupa ofa ya Sh400 milioni, kilichopo hapa ni mgongano wa kimasilahi,” kiliongeza chanzo hicho.
 

Inadaiwa kuwa, Azam wameingia kwenye ligi kwa sababu wanataka kuuza ving’amuzi vyao, lakini dau walilotoa la Sh100 ni dogo ingawa klabu nyingine ikiwemo Simba wamekubali.
 

Hata hivyo, Yanga kila kukicha imekuwa ikija na madai tofauti na tayari wameshaweka msimamo wao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanachama wao kupinga suala la udhamini wa Azam.
 

Klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani imekuwa kila kukicha ikitoa madai mapya ya kusisitiza kugomea udhamini huo wa Azam na mapema wiki hii walisema wanagomea kwa vile kuna kipengele cha CD za mchezo ambazo Azam ndiyo watazimiliki na kwamba wasingekuwa na shida na mkataba wa Azam kama kampuni hiyo isingekuwa na timu kwani kitendo cha kumiliki CD kuna uwezekano wa kuididimiza timu yao.
 

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia akizungumzia suala hilo alisema madai hayo ya Yanga hayana mashiko kwani klabu zote zinapewa CD za kila mchezo, pia suala la TBL Yanga siyo peke yao ambao wanadhaminiwa na TBL, kwani hata Simba nao ni wadhamini wao na wamekubaliana na mkataba huo wa Azam. Chanzo: mwananchi

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...