Kama kawaida rafiki wa nyavu: Drogba alifumania nyavu mara mbili na kutwaa taji la kombe la Emirates
Drogba akimpeleka sokoni kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny
Mnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi
Ufunguzi wa karamu ya mabao: Walcott akiandika bao la kuongoza kwa klabu yake ya Arsenal
Amerudi
nyumbani: Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa nahodha wa Galatasaray akiwa
amerufi nyumbani katika klabu yake ya zamani ya Arsena
Daah! hata kakombe haka kananishinda: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akitazama vijana wake wakiburuzwa.
Didier Drogba “Tembo” amekumbukiza enzi hizo akiwa ndani ya jezi ya Chelsea akiifunga Arsenal baada ya nyota huyo mwenye miaka 35 kwa sasa kuifungia klabu yake ya Galatasaray ya Uturuki mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya kombe la Emirates na kutwaa taji hilo.
Kiukweli mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki zaidi na haikuwa na thamani yoyote katika msimu, lakini Drogba ameonesha tena umwamba wake wa kuwafunga vijaba wa Arsene Wenger kwani alifanya kazi hiyo mara nyingi zaidi wakati ule akicheza ligi kuu soka nchini England.
Kocha wa Arsenal, mzee Wenger alionekana akilaumu sana kama mechi hiyo ni muhimu mno baada ya kumfuata na kumfokea kamisaa wa mechi hiyo Andre Marriner kutokana na kitendo cha mwamuzi wa kati wa mechi hiyo, Jon Moss kutoa mkwaju wa penati kufuatia beki wake
Ignasi Miquel kumfanyia madhambi mshambulaiji huyo raia wa Ivoru Coast.
Kikosi cha Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs (Miquel 69), Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla (Zelalem 61), Walcott, Sanogo (Giroud 61)
Goli: Walcott 38
Wachezaji wa akiba: Martinez, Koscielny, Podolski, Akpom
Kikosi cha Galatasaray; Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo (Sarioglu 66), Engin Baytar (Gulselam 32),Altintop (Colak, 45), Amrabat, Elmander (Drogba 45)Umut Bulut (Sneijder 45)
Wachezaji wa akiba: Nounkeu, Balta, Kazim-Richards, Kilic, Kurtrlus, Iscan
Mabao: Drogba pen 79, 88
Mwamuzi: Jon Moss