Monday, August 05, 2013

MTOTO MDOGO WA KIKE AUAWA KINYAMA MKOANI MBEYA...!!!


MTOTO mmoja wa kike ameuawa kinyama kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyofolewa macho na ubongo wake.


Tukio hilo la kikatili, limetokea mwishoni mwa wiki eneo la Idiwili kata ya Isuto wilaya ya Mbeya vijijini mkoani hapa.


Mtoto huyo wa kike, asiye na hatia, mwenye umri wa miaka miwili, aliyejulikana kwa jina la Lilian Nex Kasonso, alikatishwa uhai wake kwa makusudi kisha mwili wake kutelekezwa chini ya mti.


Baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliozungumza mwandishi wa habari hii wamesema kuwa, Mama wa mtoto huyo, alimwacha mwanae akiwa salama mikononi mwa bibi yake kisha yeye kwenda kutafuta kuni.


Punde, Bibi yake Lilian, naye alienda kuchota maji mtoni huku akimwacha mjukuu wake akiwa na furaha tele, ndipo majitu hayo makatili, kwa makusudi walimteka mtoto huyo kisha kutokomea naye pasipo mtu kuwaona ama kuwashitukia.


Mama wa marehemu aliporejea na kuuliza mwanae yupo wapi, ndipo ikawa kama amewazindua ndugu waliokuwepo jirani kisha ikapigwa nkolo ya kutaka msaada, wananchi wakasambaa na kuanza kumsaka mtoto Lilian. Endelea kutembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.


Wakiwa katika harakati za mahangaiko ya kumtafuta, wananchi wanasema, walimuona mtu mmoja kwa mbali akiwa amevalia shati jeupe ndani ya mashamba ya kahawa, na walipojaribu kumfuatilia aliwatoroka na walipofika eneo ambalo alionekana mtu huyo, lahaula, wakaona majani ya kahawa yakiwa juu ya mwili wa mtoto Lilian.


Wakaanza kuona miguu, na walipofunua zaidi, wakashtuka kumkuta Lilian akiwa amefariki, huku mwili wake ukiwa hauna tena macho na ubongo ukiwa umechokonolewa na kwa dhihaka kubwa ya wauaji hao, wakaweka gogo la mti lenye ukubwa wa mkono wa mtu mzima juu ya kichwa chake.



Askari polisi walitaarifiwa na kufika eneo la tukio ambapo baadhi yao wakiwa wamevalia sare la Jeshi hilo, wakajikuta wanaangua kilio na kusema kuwa hawajawahi kuona mauaji ya kikatili namna hii.



Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, amesema halitasalia jiwe juu ya jiwe kwa waalifu wa aina yeyote wanaofanya matukio mkoani hapa. 
 ......................................................................................................


MBEYA VIJIJINI. MAUAJI

MNAMO TAREHE 04.08.2013 MAJIRA YA SAA 18:40HRS HUKO IKUMBI-SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. NASIBU S/O MATINYA, MIAKA 25, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA SONGWE ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUTUMIA MAPANGA, MAWE NA FIMBO KISHA KUMCHOMA MOTO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUIBA MAHINDI DEBE 3 MAHARAGE BAKURI 10, DOTI 3 ZA VITENGE NA PAMPU YA BAISKELI 1 NYUMBANI KWA HEBRON S/O MWAKIMONYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.



WILAYA YA MOMBA - MAUAJI 

MNAMO TAREHE 02/08/2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA, MSAWILE S/O HALINGA, MIAKA 70, MKULIMA MNYIHA, NA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBELA ALIUWA KWA KUKATWA NA SHOKA SEHEMU ZA MGONGONI, SHINGONI NA KICHWANI AKIWA NYUMBANI KWAKE NA MKE WAKE AITWAYE ESTER D/O MGALA, MIAKA 60, MKULIMA, MNYIHA NA MKAZI WA KIJIJI HAPO KUJERUHIWA SEHEMU ZA MKONO WA KULIA NA KICHWANI WAKATI AKIJARIBU KUMSAIDIA MUMEWE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA, MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMWITA MAREHEMU SEHEMU ZA KIZANI NA KISHA KUMSAMBULIA. JUHUDI ZA KWASAKA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO ZIENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA KUWAUWA WAZEE/VIKONGWE KWA DHANA ZA KISHIRINA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA PIA ANATOA RAI WA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.


WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI

MNAMO TAREHE 30-31/07/2013 MAJIRA YASIYOFAHAMIKA HUKO KIJIJI CHA MPUMBULI KATA YA MPUGUSO WILAYA YA RUNGWE, LUKAS S/O MWAKYOMA, MIAKA 50, MNYAKYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MPUMBULI ALIUAWA NA RAMADHANI S/O MWAKYOMA, MIAKA 45, MNYAKYUSA, MKULIMA WA MPUMBULI NA GODWIN S/O MWAKYOMA, MIAKA16, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA    PILI SHULE YA SEKONDARI MPUMBULI KWA KUPIGWA NA FIMBO SEHEMU ZA KICHWANI NA KUVUNJWA SHINGO KISHA KUFUKIWA KWENYE SHIMO LA UREFU WA FUTI MBILI {2}. MNAMO TAREHE 03/08/2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS MWILI WA MAREHEMU ULIGUNDULIWA NA KUFUKULIWA KISHA KUZIKWA UPYA BAADA YA UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA MASHAMBA NA WATUHUMIWA WOTE WAMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE KUYATATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  MAZUNGUMMZO  ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.



Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Na, Mwandishi wa kalulunga blog

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...