Tuesday, August 06, 2013

MGOMBEA ALITUMIA ZIWA NYASA KUJIPIGIA DEBE MALAWI

banda e1188

Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa. (HM)


Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi  Mkoa wa Kati.

Akikaririwa na gazeti la  Nyasa Times, Mutharika  alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.

Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.

Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na  akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.

 “Hakuhitajiki majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi, litakuwa la Malawi,” alisema Mutharika ambaye alichukua masomo ya Sheria Tanzania.
 “Tanzania inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi wetu, lakini ukweli, hawana hata tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza haya yote. Nitaleta meli nyingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana,” alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi wake.
 Tanzania inataka kugawana ziwa, lakini Malawi imegomea mpango huo na suala hilo liko katika majadiliano ambayo Banda alisema kama mwafaka haukupatikana ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa (ICJ). Chanzo: mwananchi

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...