Rais
Jakaya Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye
umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa wa
Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko
Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye awali
alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo Dar es Salaam,
alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya
Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu.
Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais
Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha
Dogodogo Centre |
Rais
Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji
wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya
dunia
Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais
Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na
kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote
katika michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti
wa Sport Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema kuwa
walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua
kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema
kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha
kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba
mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo
alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika
Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na
washiriki 480 kutoka timu 44 kutoka nchi 14 ambapo
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy
Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na
jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa,
na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili
kuukuza ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao na
kuitangaza Tanzania.