Sunday, August 04, 2013

AUA MKE WAKIBISHANA KIPI KITANGULIE KUPIKWA KATI YA MAINI NA NYAMA ....!!!

 Photo: Aua mke wakibishana nini kianze kupikwa maini au nyama

Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida, kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.

Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.

Kamanda Kamwela alisema baada ya kufika nyumbani mume alimwagiza mkewe aanze kupika nyama ya maini lakini mkewe akadai anataka aanze na nyama mchanganyiko.

"Baada ya kufika nyumbani, baba mwenye nyumba alimtaka mke aanze kupika maini halafu baadaye amalizie na nyama ya ng'ombe mchanganyiko, lakini badala yake mkewe alikataa akamwambia mtuhumiwa kuwa ataanza kwanza kupika nyama ya ng'ombe kwa madai kuwa huchukua muda mrefu kuiva,"alifafanua Kamwela.

Alisema baada ya mvutano huo uliochukua muda mrefu, ndipo mtuhumiwa alianza kumpiga mateke na ngumi mkewe sehemu mbalimbali za mwili akidai hataki kufuata maagizo yake.
Kamanda Kamwela alisema kutokana na kipigo hicho, mkewe alianguka chini hali iliyomuogopesha mumewe na kutoka nje kuwaita majirani ambao walipofika walimkuta Amina akiwa amefariki dunia.

Alisema taarifa ya daktari inaonyesha kifo cha marehemu kimechangiwa na kipigo kilichosababisha bandama kupasuka na kuvuja damu pia kunyongwa shingo na kwamba baada ya upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji hayo.
Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida, kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya
kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.

Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.

Kamanda Kamwela alisema baada ya kufika nyumbani mume alimwagiza mkewe aanze kupika nyama ya maini lakini mkewe akadai anataka aanze na nyama mchanganyiko.

"Baada ya kufika nyumbani, baba mwenye nyumba alimtaka mke aanze kupika maini halafu baadaye amalizie na nyama ya ng'ombe mchanganyiko, lakini badala yake mkewe alikataa akamwambia mtuhumiwa kuwa ataanza kwanza kupika nyama ya ng'ombe kwa madai kuwa huchukua muda mrefu kuiva,"alifafanua Kamwela.

Alisema baada ya mvutano huo uliochukua muda mrefu, ndipo mtuhumiwa alianza kumpiga mateke na ngumi mkewe sehemu mbalimbali za mwili akidai hataki kufuata maagizo yake.
Kamanda Kamwela alisema kutokana na kipigo hicho, mkewe alianguka chini hali iliyomuogopesha mumewe na kutoka nje kuwaita majirani ambao walipofika walimkuta Amina akiwa amefariki dunia.

Alisema taarifa ya daktari inaonyesha kifo cha marehemu kimechangiwa na kipigo kilichosababisha bandama kupasuka na kuvuja damu pia kunyongwa shingo na kwamba baada ya upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji hayo.
HABARI LEO

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...