Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe(PICHANI) amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo. |
Thursday, June 27, 2013
WATU WA MIKOANI WASHAURIWA KUTOENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA HADI ATAKAPO MALIZA ZIARA YAKE.
KUMEKUCHA BIG BROTHER, MWAKILISHI WA BB TANZANIA FEZA KESSY NDANI YA PENZI ZITO NA O"NEAL WA BOTSWANA
FEZA KESSY (TANZANIA)
O"NEAL (BOTSWANA)
Feza akilana denda na O'neal kitandani.
HAKI ZA BINADAMU WAMTAKA WAZIRI MKUU PINDA AOMBE RADHI WATANZANIA, AKIKATA AWAJIBISHWE KWA MUJIBU WA SHERIA....!!!
Akizungumza
na waandishi wa habari janaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba amesema kitendo cha
Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuruhusu matumizi ya nguvu kwa polisi dhidi
ya raia ni cha kulaaniwa na wapenda haki wote na amemtaka waziri mkuu
kuwaomba radhi watanzania.
KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013
Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.
Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.
Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu. Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.
KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013
Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.
Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.
Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu. Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.
CHADEMA WAKATAZWA KUVAA KOMBAT BUNGENI...!!
Kombati za CHADEMA mzozo
Siku moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.
Mbowe na wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.
Uamuzi huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.
Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi yanayohitaji majibu.
Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).
Kipengele hicho cha kanuni kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia.
Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo, lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
kuchukua hatua ya kuwazuia.
“Zile wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.
Siku moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.
Mbowe na wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.
Uamuzi huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.
Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi yanayohitaji majibu.
Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).
Kipengele hicho cha kanuni kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia.
Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo, lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
kuchukua hatua ya kuwazuia.
“Zile wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.
SAFARI YA RONALDO KUREJEA MAN U YAIVA
CRISTIANO Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo.
Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania.
Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa Man u kabla hajaenda kuanza msimu mpya Madrid.
Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.
Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi.
"Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.'
Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema. Chanzo: binzubeiry
Wednesday, June 26, 2013
TANGAZO: NAFASI ZA MASOMO
| ST. THOMAS
INSTITUTE OF TECHNOLOGY & MANAGEMENT
P.O. BOX 6089, Morogoro.
CEL: 0713 530261, 0717-707025, 0767 530261, 0655 758980
Email: magkit2005@yahoo.com
Chuo kipo Morogoro mjini, Kilakala. Chuo Kipo katika mazingira
mazuri ya kujifunzia. Studio za kisasa kwa wanafunzi wa Uandishi wa habari na
Utangazaji.
LIST
OF COURSES
S/N
|
COURSE
|
DURATION
|
1
|
CERTIFICATE
IN BUSINESS ADMINISTRATION
|
1YEAR
|
2
|
CERTIFICATE IN HOTEL MANAGEMENT
|
6MONTHS
|
3
|
CERTIFICATE
IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
|
1YEAR
|
4
|
CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
|
1YEAR
|
5
|
CERTIFICATE
IN COMPUTER SCIENCE.
|
1YEAR
|
6
|
CERTIFICATE
IN RECORD MANAGEMENT
|
1YEAR
|
7
|
CERTIFICATE IN PROCUREMENT AND
SUPPLY
|
1YEAR
|
8
|
CERTIFICATE
IN NURSERY TEACHING AND KIDERGATEN
|
6MONTHS
|
9
|
CERTIFICATE IN
ACCOUNTANCY.
|
1YEAR
|
10
|
CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
|
1YEAR
|
11
|
CERTIFICATE IN
JOURNALISM&MASS COMMUNICATION
|
1 YEAR
|
12
|
BASIC
CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION
|
6MONTHS
|
13
|
BASIC
CERTIFICATE IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
|
6MONTHS
|
14
|
BASIC
CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
|
6MONTHS
|
15
|
BASIC
CERTIFICATE IN COMPUTER SCIENCE.
|
6MONTHS
|
16
|
BASIC
CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT
|
6MONTHS
|
17
|
BASIC CERTIFICATE IN PROCUREMENT
AND SUPPLY
|
6MONTHS
|
18
|
BASIC
CERTIFICATE IN ACCOUNTANCY.
|
6MONTHS
|
19
|
BASIC
CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
|
6MONTHS
|
Kwa wanachuo wa Uandishi wa Habari na Utangazaji
Muhula mpya utaanza Rasmi tarehe July 8 mwaka huu..
MZEE MANDELA AFANYIWA MAOMBI MAALUM
ASKOFU
mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo
Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson
Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi
hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini
ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu
zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo
vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa
Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern
Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta
ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela.
Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela
ya afya ilikuwa mbaya sana. Chanzo: bbcswahili
Ujio wa Obama: Mashirika ya ndege yatakiwa kubadili ratiba za safari Julai Mosi
Maandalizi
ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto
huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Aidha,
kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege
kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua
nchini. Jana,
waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika
uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba
halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema
jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa
ugeni huo.Alisema
kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo
hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni
kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege
zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,”
alisema Malaki.Pia
alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na
tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa
nyakati mbalimbali. “Sijawahi
kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini
ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.Alisema
awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni
mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa
ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana,
Julai Mosi.Mkurugenzi
huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya
pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na
maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo
itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
MTOTO WA MNADHIMU MKUU WA JWTZ AFUMWA KWA MGANGA WA KIENYEJI AKIROGA
Mama
mmoja ajulilikanae kwa jina la Magreth simon Nkwera ambae ni mtoto wa
kwanza wa mnadhimu mkuu wa kwanza wa JWTZ Brig Gen Simon Nkwera
amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la
kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha
maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili
moja akisubiri kupandishwa kizimbani.
Mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mganga na mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa mauwaji
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa
Mtuhumiwa
akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa shirima Afisa polisi jeshi daraja la
Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa
sangoma.
CHANZO VIJIMAMBO
NATASHA AFUNDWA: MASTAA WAKATA MAUNO MBAYA:
Baadhi ya waalikwa wakijiachia pamoja na Natasha (kushoto) wakati wa sherehe hiyo.
Na Imelda MtemaHUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru. APEWA SOMO Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa. |
Alipotoka
nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo
kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma. KIASILI ZAIDI Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo. Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari. |
Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.” |
SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERIA
Serikali
imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza
kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata
kiasi cha kusababisha madhara au kifo.
Kauli
hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa
bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote
wanaokaidi kutii sheria.
“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.
Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha
18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa
kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au
kifo katika mazingira ya kisheria.
Aliyataja
mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia
madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia
mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo
kinyume na maumbile.
Pia
kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au
kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai
wa mtu au mali.
Alieleza kuwa Kifungu
cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio
mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda
mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya
Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.
RAIS WA MAREKANI BARAK OBAMA KUANZA ZIARA BARANI AFRIKA LEO
Rais Barack Obama anafanya ziara ya pili barani Afrika kuanzia leo Jumatano. Atazuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Rais
wa Marekani Barack Obama Jumatano anaanza ziara ya wiki moja nzima
katika nchi tatu za Afrika kwa lengo la kuhamasisha demokrasia na
uwekezaji wa Marekani barani humo.
Rais
Obama atakwenda Senegal leo Jumatano ambako atakutana na rais Macky
Sall na kesho Alhamis atatembelea nyumba ya kihistoria ya watumwa wa
Afrika walioletwa Marekani katika kisiwa cha Goree.
Ijumaa
bwana Obama atakwenda Afrika Kusini ambako atakutana na rais Jacob Zuma
na kutembelea kisiwa cha Robben ambacho rais wa zamani Nelson Mandela
alifungwa jela.
Maafisa
wa Afrika Kusini walisema ziara ya bwana Obama itaendelea licha ya
kuwepo na hofu kote nchi humo kuhusu kudhoofika kwa afya ya bwana
Mandela. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye miaka 94 yuko
katika hali mahtuti na amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
Tuesday, June 25, 2013
KAJALA AKUNUSHA KUHUSU KUGOMBANA NA WEMA SEPETU
Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.
Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.
Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.
“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala
Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.
Subscribe to:
Posts (Atom)