Rais Barack Obama anafanya ziara ya pili barani Afrika kuanzia leo Jumatano. Atazuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Rais
wa Marekani Barack Obama Jumatano anaanza ziara ya wiki moja nzima
katika nchi tatu za Afrika kwa lengo la kuhamasisha demokrasia na
uwekezaji wa Marekani barani humo.
Rais
Obama atakwenda Senegal leo Jumatano ambako atakutana na rais Macky
Sall na kesho Alhamis atatembelea nyumba ya kihistoria ya watumwa wa
Afrika walioletwa Marekani katika kisiwa cha Goree.
Ijumaa
bwana Obama atakwenda Afrika Kusini ambako atakutana na rais Jacob Zuma
na kutembelea kisiwa cha Robben ambacho rais wa zamani Nelson Mandela
alifungwa jela.
Maafisa
wa Afrika Kusini walisema ziara ya bwana Obama itaendelea licha ya
kuwepo na hofu kote nchi humo kuhusu kudhoofika kwa afya ya bwana
Mandela. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye miaka 94 yuko
katika hali mahtuti na amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
No comments:
Post a Comment