Wednesday, April 24, 2013

Zitto Kabwe atoa majibu kwa Umma kuhusu Habari za mama yake Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola.


Mh.Zitto Kabwe.
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba 
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu. 
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa. 
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya  ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.

POMBE YAMTOA MADEE...ANADAI IMEMPA HESHIMA KUBWA MTAANI......!!


Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
  
Akiongea  na  mwandishi  wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal

Tuesday, April 23, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA KIKRISTO LEO IKULU

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
 Raisi akiwa katika picha ya Pamoja na viongozi wa dini mbalimbali
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
PICHA NA IKULU

HII NDIO STYLE MPYA YA NYWELE YA TUNDA MAN

Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection maarufu kama Tunda Manameonekana kubadili muonekano wake wa zamani na sasa kuja na mpya ....

Muonekano huo mpya wa style ya nywele zake [pichani] umeonekana kuwashangaza watu kwa jinsi ulivyokuwa wa kipekee ...

Haijafahamika ameutoa wapi na ni kwa ajili gani anautumia, ila hivi ndivyo anavyoonekana sasa Tunda Man kichwani kwake ...

MCHINA AJA NA SIMU MPYA INAYOCHAJIWA KWA SODA

HII NDO SIM INAYOCHAJIWA KWAKUTUMIA SODA YA COCA COLA

Wanasema hii dunia kilichoshindikana ni kumtengeneza binadamu peke yake, kuna vitu vingine ni ngumu kuamini lakini ni ukweli vimetokea, hiyo ni simu ambayo chaji yake inatokana na soda ya Cocacola.

MAAFANDE WACHEZEA NYETI ZA MTUHUMIWA KWA KISINGIZIO CHA UKAGUZI.......!!

Pengine hizi  ndo  starehe  pekee  wanazozipa  "maafande" hasa  wale  wanahusika  na  ulinzi  wa  mageti.....
Miongoni  mwa  majukumu  yao  ni  "kuwapapasa"   na "kuwashika- shika" watu wanaofika  katika  maeneo  hayo  yenye  ulinzi  mkali  ili  kujiridhisha  kwamba  hawana  silaha  au  kitu  chochote  kibaya....
Kinachoshangaza  zaidi  ni  kitendo  cha mafande   kukomaa  na  nyeti  za  akina  mama  wakati  kuna  sehemu  zingine  kibao  za  mwili  ambazo  walitakiwa  wazikague.....
 
Hata  hivyo, kwa  dunia  ya  leo, ukaguzi  kama  huu  umepitwa  na  wakati  kwa  sababu  kuna  vifaa vingi  sana  vya  kitaalam  ambavyo  vinaweza  kufanya  kazi  hizi  badala  ya  maafande  kushinda  wakicheza  na  makalio  ya  watu.
Sourec Gumzo la Jiji

RAIS MASKINI KULIKO WOTE DUNIANI


NCHI ya Uruguay yenye raia takribani milioni 4, inatajwa kuwa na bahati ya kuwa na Rais asiye na chembe ya tamaa. Hana makuu, kiasi kwamba anatajwa kuwa ndiye Rais masikini zaidi kuwahi kutokea duniani.
Huyu si mwingine, bali ni Jose Mujica, Rais wa sasa wa Uruguay ambaye pia ni Rais wa 40 wa nchi hiyo. Tangu aingie madarakani Machi mosi mwaka 2010, amekuwa akionekana kuwa kiongozi wa tofauti kabisa, tofauti na waliomtangulia.
Mathalan, baada ya kufanikiwa kuishika nchini, hakuwa na tamaa ya kukimbilia Ikulu, yeye alichokifanya ni kuamua kuishi katika makazi yake yaleyale, katika nyumba ya mkewe iliyoko shambani, nje ya Jiji la Montevideo.

Kwa ujumla, anapenda maisha ya kawaida, maisha ya kuwahurumia wengine na kujitahidi kuonesha kwa vitendo.
Ni vigumu kuamini, licha ya kuwa ni Rais wa nchi, amejishusha mno kiasi cha mara kadhaa kuonekana akijichanganya na raia wake katika shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwamo ujenzi wa barabara, kulima mashamba ya mfano.

WALIMU WAPIGWA MAWE NA WANAFUNZI WA SHULE YA MIZENGO PINDA KWA MADAI KUWA NI WACHAWI

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda  kata ya Kibaoni  Wilayani Mlele mkoani Katavi, wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu hao baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi, Joseph Myovela, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2:30 usiku shuleni hapo baada ya kuzuka kwa tafrani iliyodumu kwa zaidi ya saa 1:30.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kilitokana na mwanafunzi mmoja aitwaye Jofley Pinda kushikwa na ugonjwa wa mapepo uliomfanya aanguke chini ambapo tukio hilo lilitokea mchana wa saa saba.

Alisema wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja Alico Kamyoge (36) ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa mapepo.

MAKAHABA WAILALAMIKIA POLISI NA KUDAI KUWA IMEWAGEUZA "ATM MASHINE"

Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela.

Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, limelalamikiwa kwa vitendo vya baadhi ya askari wake kuvamia vyumba vinavyodaiwa kupangwa na watu wanaodaiwa kuwa makahaba (madanguro) na kuwapora fedha, simu na vitu vingine vya thamani nyakati za usiku.

Aidha, askari hao wamedaiwa kuwageuza wanawake hao mashine za kutolea fedha (Atm) ambapo hufika katika vyumba vyao kila baada ya wiki moja na kuwadai fedha kati ya Sh.30,000 na 50,000 kila mmoja kama hongo ili wasiwafikishe polisi.

Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya akina mama wanaoishi eneo la Mwananyamala walipozungumza na NIPASHE baada ya askari hao kukamata wanawake zaidi ya 87.

Kiongozi wa wanawake hao, Judith Rugamwa alidai kuwa, askari hao kutoka vituo vya Oysterbay na Mabatini wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga, jambo ambalo ni kinyume cha haki zao binadamu.

Upelelezi kesi ya Lwakatare umekamilika - Mkurugenzi

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, amesema upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatale na mwenzake Joseph Ludovick umekamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mulungu alisema kwa sasa jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.

Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu.

Watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.

Kuhusu kesi ya kumwagiwa tindikali Kada wa CCM, Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Igunga Septemba 2011, alisema tayari watuhumiwa wawili wamekwishafikishwa mahakamani.

Mulungu alisema kuhusu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na matukio mengine yaliyotokea Zanzibar, upelelezi bado unaendelea na kwamba upo katika hatua mbalimbali. Aliwataka watu kuwa na subira.

"Lady Jay Dee, mnafiki wa miaka 10, shujaa wa siku 30.....!!" asema Saleh Ally


Imeandikwa na Saleh Ally wa  www.salehjembe.blogspot.com
MGOGORO wa kimuziki kati ya msanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidi kuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake na kuamini linachoamini.
Kundi ambalo linamuunga mkono Jaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine, la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.
Jaydee anashutumu kubaniwa nyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameeleza wazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwa wakionyesha chuki binafsi dhidi yake.
Jaydee pia aliwaponda wasanii Ben Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.

Samata aziponda Yanga, Simba

Lubumbashi, DR Congo. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samata amesema viongozi wa klabu za Tanzania hawana malengo ya kutwaa ubingwa wa Afrika ila wanapigania kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu tu.
Samata alisema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa mtandao wa klabu ya TP Mazembe wakati timu hiyo ilipokuwa imeweka kambi mjini Ndola, Zambia kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Alisema,”Viongozi wa klabu kubwa za Tanzania, Simba na Yanga hawana malengo ya kutaka kushinda ubingwa wa Afrika na kucheza mashindano ya FIFA ya klabu bingwa ya dunia, viongozi wanapigania kushinda Ligi Kuu tu.”
Samata alisema,”Viongozi wa TP Mazembe wana malengo ya juu, wapo tofauti na viongozi wa klabu kubwa za Tanzania, ndiyo maana TP Mazembe inakuwa klabu kubwa.
“TP Mazembe haionei wivu klabu nyingine za Afrika, ila zipo klabu nyingi za Afrika zinazoionea wivu, TP Mazembe ina vifaa vyote muhimu vya kuwaandaa wachezaji, ina miundombinu ya soka, ina wafanyakazi wanaoijua soka na ina wachezaji wenye kiwango cha juu,”alisema Samata.
Alisema, “TP Mazembe ina wachezaji nyota kutoka DR Congo, Ghana, Zambia, Tanzania na Uganda, naona faraja kuchezea klabu hii, nataka mwaka huu nitwae ubingwa wa Afrika nikiwa na klabu yangu ya TP Mazembe.
Nataka nicheze mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa ya Dunia, ambapo naweza kucheza dhidi ya Barcelona na kuonyesha uwezo wangu.”
Mwanacnhi

MATUSI YATAISHA BUNGENI ENDAPO SPIKA ATAACHA UPENDELEO"........TUNDU LISSU





Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema fujo zitaisha bungeni ikiwa Spika wa Bunge, Naibu na Wenyeviti watafuata na kusimamia kanuni za Bunge bila kupendelea upande wowote.

Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Alisema fujo hazitaisha kama watu hawatafuata kanuni na Spika kusimamia na kuzingatia mamlaka yake bila ya upendeleo wowote. 
“Tatizo kubwa Spika anafanya kazi bila kufuata kanuni za Bunge. Kuna mambo mengine anayatolea maamuzi bila kufuata kanuni za Bunge. Mfano suala letu la adhabu tuliyopewa wabunge watano wa Chadema ya kutohudhuria vikao vitano. Hakuna katika kanuni za Bunge. 
Spika alipaswa kupeleka majina yetu katika Kamati ya Maadili ili ichunguze na kupendekeza adhabu kisha ipeleke taarifa bungeni na Bunge ndilo litoe adhabu," alisema.

ZIARA YA KICHAMA YA DKT SHEIN KUTEMBELEA MIKOA YA ZANZIBAR


19
Na Maelezo Zanzibar
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein amesema kuwa ataendelea kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuulinda Muungano wa Serikali mbili uliopo.
Kauli hiyo ameitoa leo huko katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.
 Dkt Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa kuna kila sababu ya kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu wake na kwamba Muungano uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya kuendeleza mashirikiano ya kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 23.04.2013

.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...