Sunday, April 21, 2013
Saturday, April 20, 2013
Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf akamatwa akijiandaa kugombea ubunge.
Polisi nchini Pakistan wamemtia mbaroni rais wa zamani wa nchi hiyo Jenerali Mstaafu Pervez Musharraf.
Musharraf amekamatwa leo nyumbani kwake mjini Islamabad na kufikishwa mahakamani.
Kiongozi
huyo alirejea Pakistan mwezi uliopita, akitarajia kuwania ubunge katika
uchaguzi mkuu mwezi ujao, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minne.
Hata
hivyo ombi lake lilikataliwa na maafisa wa uchaguzi, kwa misingi
kwamba anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yanayohusiana na kipindi
chake cha utawala.
Hapo Jana mahakama mjini Islamabad iliamuru Musharraf akamatwe.
ROSE NDAUKA AWATEGA MADENTI WA DSJ, HIKI NDO ALICHOKIFANYA
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose
Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua
madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao
walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
ANAYEMWEZESHA WEMA SEPETU KIMKWANJA AJULIKANA,
VIROBA TISHIO JIPYA LA SARATANI YA KOO KWA WANAUME
Daktari
bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya saratani katika Kitengo cha
Patholojia, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Henry Mwakyoma na
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road, Dk Crispin Kahesa wameeleza hayo jijini Dar es Salaam.
Walisema
kuwa ingawa bado hakuna visababishi kamili vya saratani hiyo, asilimia
90 ya wagonjwa wa saratani ya koo wamekuwa na historia ya uvutaji
sigara, unywaji pombe kali kama viroba na kula aina za vyakula
vilivyochomwa
ikiwamo nyama na samaki, ulaji pilipili, ndimu, ‘chilisosi’ na unywaji wa vitu vya moto kupita kiasi.
“Ongezeko
ni kubwa, asilimia 90 ya wagonjwa tuliowapokea hapa wana historia ya
kutumia vilevi vikali, sigara, pilipili kwa wingi na aina nyingine na
vitu vinavyosababisha saratani hii,” anasema Dk Kahesa.
Fid Q Atoa Mauzo RBT Ya Wimbo Wake Mpya Kuweka Kumbukumbu Ya Marehemu Bi. Kidude ...
Kuna uthubutu wa kusema kuwa hili inawezekana kuwa ni wazo zuri na jema kabisa ambalo toka mwaka uanze umewahi kulisikia ...
Rapper
kutoka MWANZA CITY, Fid Q amependekeza kujengwa kwa kumbukumbu
itakayomuenzi ambayo pia itatumika kusaidia waliokuwa karibu na marehemu
Bi. Kidude aliyefariki na kuzikwa jana huko visiwani Unguja ...
Akiongea
katika radio interview na kipindi cha XXLkinnachoongozwa na BDozen,Fid Q
amependekeza kufanyika kwa jambo hilo hata kwa harambee
itakayochangisha fedha za kufanikisha kitu hicho ...
Kwa
kuanzia, Fid Q ambae alipata nafasi ya kurekodi wimbo pamoja na
marehemu,"JUHUDI ZA WASIOJIWEZA" uliokuwa kwenye album yake ya
Propagandaametoa mauzo yote ya miito ya simu, yaani Ring Back Tones
[RBT]yatakayouzwa kwa wananchi na wapenzi wa muziki katika kusaidia
ujenzi wa museum hiyo ...
Fid Q "Sitachukua hata thumni ..."
Hiki
ni kitu cha kujivunia kuwa na mwanamuziki kama huyu ambae naweza kusema
anauona umuhimu wa wanamuziki wakubwa hapa nchini, Bi. Kidude amekuwa
mwanamuziki wa Taarabu aliyefanya vizuri sana na kuitangaza nchi hii ...
Mimi na wewe, tuanze kwa kushiriki kwenye hili ... BIG UP Fareed !!!
R.I.P Bi. Fatuma binti Baraka a.k.a Bi. Kidude
DARASA LA SABA KUJIUNGA VYUO VIKUU
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na ChuoKikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”
Wanaotumia laini za simu zisizosajiliwa kutozwa Sh500,000 au kufungwa
Ni kauli ya TCRA ikinukuu sheria ya mawasiliano. Lengo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika
maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha
130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba
za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu
yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.
“Katika vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na Aprili 11 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa
Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu na vyombo vya
usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na uvunjifu
wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa
ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika jamii.
Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema
namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia 93 na asilimia 7
hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki inatakiwa kuondoka haraka..
Friday, April 19, 2013
BABA KANUMBA HAONI ULAZIMA WA KULIONA KABURI LA MWANAE KANUMBA
BABA
wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba amefunguka kuwa haoni
ulazima wa kuliona kaburi la mwanaye na kuhusu kufanya maombi mwaka
mmoja baada ya kifo, alifanya akiwa huko nyumbani kwake Shinyanga.
Akizungumza
kwa njia ya simu hivi karibuni, mzee Charles alisema mtu anapofariki
kikubwa ni kuombewa na hilo la kwenda kulitazama kaburi lake haliwezi
kuwa na faida.
“Mimi
nilifanya sala ya kumuombea Kanumba pamoja na mtoto wa dada yake ambaye
walikufa kwa kufuatana kwenye Kanisa la AIC Shinyanga,” alisema mzee
huyo na kuongeza;
“Mtu
akishakufa kinachobaki ni kumuombea huko aliko na kaa ukijua kwamba
huku ndiyo kwenye chimbuko la marehemu hivyo nisingeweza kwenda kufanyia
maombi kwenye mji mwingine.”
'Chadema kuwa na mabalozi nyumba 10'
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbrod Slaa
--
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kimeanza mkakati
kuhakikisha kinakuwa na mabalozi wa nyumba kumi kwa kila eneo. Hatua
hiyo ni katika kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi
kitongoji .
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alisema hatua hiyo imeanza kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya taifa ya chama hicho.
Alikuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa taifa waweze kwenda kutoa mafunzo ngazi ya kanda ambao nao wataendelea kutoa elimu hiyo kwenye jimbo kata hadi vijiji.
Lengo la chama hicho ni kuhakikisha kinajiimarisha na kuwa na viongozi wenye kufuata maadili na misingi ya chama na kujiandaa kushika dola kwa kuwa na uongozi wenye weledi wa hali ya juu, alisema.
“Sisi hatutaki mwanachama anunue shashada ya kura, tunajiandaa tunapeleka silaha ya kujiandaa kushika dola na ndiyo maana tunawaandaa kuhakikisha tunaposhika dola, tunakuwa tayari na viongozi wenye weledi mkubwa,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa aliwashangaa watu wanaodai kuwa M4C imekufa.
Alisema watu hao hawajui kuwa Chadema imejipanga na ina mbinu za utawala ambazo hazina hila kama baadhi ya vyama vingine vinavyofanya.
“ Navishangaa vyama vingine vinasifika kwa hila badala ya kuijenga Tanzania na wananchi wake… serikali za mitaa hadi wilaya ni wizi mtupu sisi tunatengeneza wataalamu wenye uchungu wa kulinda rasilimali zao,” alisema.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa chama hicho, Benson Kigaula alisema inategemewa watafundishwa wakufunzi 30,606 ambao watavifikia vitongoji vyote nchini.
Alisema hadi Oktoba mwaka huu vijiji 18,000 vitakuwa vimefikiwa na kupewa walimu na wakufunzi hao.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alisema hatua hiyo imeanza kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya taifa ya chama hicho.
Alikuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa taifa waweze kwenda kutoa mafunzo ngazi ya kanda ambao nao wataendelea kutoa elimu hiyo kwenye jimbo kata hadi vijiji.
Lengo la chama hicho ni kuhakikisha kinajiimarisha na kuwa na viongozi wenye kufuata maadili na misingi ya chama na kujiandaa kushika dola kwa kuwa na uongozi wenye weledi wa hali ya juu, alisema.
“Sisi hatutaki mwanachama anunue shashada ya kura, tunajiandaa tunapeleka silaha ya kujiandaa kushika dola na ndiyo maana tunawaandaa kuhakikisha tunaposhika dola, tunakuwa tayari na viongozi wenye weledi mkubwa,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa aliwashangaa watu wanaodai kuwa M4C imekufa.
Alisema watu hao hawajui kuwa Chadema imejipanga na ina mbinu za utawala ambazo hazina hila kama baadhi ya vyama vingine vinavyofanya.
“ Navishangaa vyama vingine vinasifika kwa hila badala ya kuijenga Tanzania na wananchi wake… serikali za mitaa hadi wilaya ni wizi mtupu sisi tunatengeneza wataalamu wenye uchungu wa kulinda rasilimali zao,” alisema.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa chama hicho, Benson Kigaula alisema inategemewa watafundishwa wakufunzi 30,606 ambao watavifikia vitongoji vyote nchini.
Alisema hadi Oktoba mwaka huu vijiji 18,000 vitakuwa vimefikiwa na kupewa walimu na wakufunzi hao.
OBAMA ATOA KAULI KUHUSU JAY Z NA BEYONCE KUTEMBELEA CUBA.
Rais
wa Marekani Barack Obama ameikana ziara ya rapa nyota nchini humo Jay- Z
na mke wake Beyonce akisema kuwa hana habari na safari yao waliyoifanya
hivi karibuni kwenda nchini Cuba
Hivi
karibuni Jay Z na Beyonce walisafiri kwenda nchini Cuba kwa ajili ya
kuadhimisha miaka mitano ya ndoa yao jambo lilolosababisha maofisa wa
Chama cha Republican kutaka ufanyike uchunguzi ama amevunja vikwazo vya
kusafiri
Akiwa
nchini humo rapa huyo alizindua kibao chake alichokipa jina la'Open
Letter' ambacho mashahiri yake yanaonekana kama Obama alikuwa amemzuia
kufanya ziara hiyo,hata hivyo taarifa iliyotolewa na Msemaji wa White
House, Jay Carney ilieleza kuwa utawala wa Serikali ya Rais Obama ulitoa
baraka zote kuhusu safari hiyo ya Jay Z kwenda Cuba na kwa sasa rais
huyo ametoa kauli kama hiyo
Rais Kikwete amemteua Bw. Raymond Mbilinyi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Raymond P. Mbilinyi(Pichani) kuwa Katibu Mtendaji, Baraza
la Biashara la Taifa , (TNBC).
Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, 19 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu
Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo
ulianza Machi 4, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huu, Bwana Raymond P. Mbilinyi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendanji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na anachukua nafasi iliyoachwa na Bwana Dan Mrutu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
19 Aprili, 2013
RAIS UHURU KENYATTA AMEITANGAZA STRUCTURE YA SERIKALI YAKE
President
Uhuru Kenyatta unveils the structure of his Government, In exercise of
the authority vested in him by the Constitution of Kenya 2010 and in
conformity with the expectations of a lean and effective structure,
President Kenyatta officially released the list of ministries and state
departments that will form the National Executive as follows:
Under
the Presidency, there will the Executive Office of the President and
the Executive Office of the Deputy President with two ministries:
Ministry of Interior and Coordination of National Government.
Ministry of Devolution and Planning.
Other
ministries are: 3. Defence 4. Foreign Affairs. 5. Education which will
have the Department of Education and Department of Science and
Technology 6. The National Treasury 7. Health 8. Transport and
Infrastructure which will have the Department of Transport Services and
the Department of Infrastructure.
9.
Environment, Water and Natural Resource 10. Land, Housing and Urban
Development 11. Information, Communication and Technology (ICT) 12.
Sports, Culture and the Arts 13. Labour, Social Security and Services
14. Energy and Petroleum 15. Agriculture, Livestock and Fisheries under
which are the Department of Agriculture, Department of Livestock and
Department of Fisheries 16. Industrialization and Enterprise
Development.
17.
Commerce and Tourism which has the Department of Commerce and
Department of Tourism 18. Mining, The structure also contains the Office
of the Attorney General and Department of Justice.
In
the new structure, President Kenyatta has collapsed the ministries from
44 to 18. The reduced structure is geared towards achieving a lean,
efficient and effective executive branch of Government.
In
the structure, the President has given special focus to the youth,
gender, devolution, planning as well as national cohesion and
integration which have all been brought under the Presidency.
Also
given special focus is mining which is now a stand-alone ministry.
Information, Communication and Technology ministry as well as Sports,
Culture and Arts are also stand-alone ministries with a view to
leveraging on the creative potential of the youth. Infrastructure
ministries as well as national resources ministries have also largely
been brought under the same roof. Picha na Millard Ayo
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya
akionyesha kitabu alichokiandika kwa wabunge wakati akichangia
Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Utawala Bora na Uratibu na Mahusiano kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini
Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi. Picha na Pamela Chologola.
Dodoma. Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu),Profesa Mark Mwandosya ametoa
majibu kwa wanaoisakama Idara ya Usalama wa Taifa akilieleza Bunge kuwa
ni muhimu ikatafutwa kamati itakayokuwa inajadili masuala ya idara hiyo
na si bungeni.
Profesa
Mwandosya alisema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za baadhi ya
wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka 2013/14.
Juzi
wakati wa kuwasilisha hoja kambi rasmi ya upinzani bungeni,iliitaka
Serikali kuwachukulia hatua maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa–Ikulu
ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya utekaji na
utesaji watu wanaoonekana kuikosoa Serikali. Madai hayo yalitolewa
bungeni na msemaji wa kambi hiyo, kuhusu bajeti ya Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Profesa Kulikoyela Kahigi katika
hotuba ambayo awali ilizua mvutano wa mambo gani yasomwe na yapi
yabakiwe.
Hata
hivyo katika kikao hicho hotuba hiyo iliamriwa iahirishwe kwa muda,hadi
kamati ya kanuni ikutane na kutoa uamuzi wa baadhi ya mambo yanayotaja
majina ya watumishi wa usalama wa taifa na mengine yaliyoko mahakamani
yaondolewe.
Akizungumzia
hali hiyo, Mwandosya alisema anashangazwa na watu wanaozungumza kuhusu
usalama wa taifa kama vile ni ndugu zao au marafiki kitu ambacho si
sawa.
“Usalama
wa Taifa hauwezi ukawa unazungumzwa tu hivi hivi, inatakiwa kuwe na
kamati ya kuujadili kama ilivyo kwa nchi za wenzetu Marekani, Uingereza
katika mashirika yao kama FBI na MI6,”alisema Profesa Mwandosya na
kuongeza:
“Usalama
wa taifa hauwezi ukazungumzwa hapa kuna sehemu ya kuzungumzia kwani
kuzungumza hapa ni sawa na kujianika, usalama hauwezi kuwa wa kutoa
kucha watu kwani utakuwa huo si usalama bali ni uhalifu.”
Wakati
huo huo, Mbunge wa Longido, Michael Laizer amependekeza Bunge la sasa
livunjwe ili Serikali itangaze uchaguzi mpya kutokana na wabunge wengi
kutojua wajibu wao.
Mbali
na hilo, mbunge huyo amevitaka vyama vya siasa vyenye wabunge kukutana
na wabunge wao na kujadiliana namna bora ya kulifanya Bunge liwe na
heshima mbele ya Watanzania.
“Hapa hakuna mtu anayestahili kuitwa mbunge, maana sioni mwenye heshima hiyo”, alisema Laizer.
Mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)