Mchakato
wa marekebisho ya kanuni za Bunge umeibua mjadala mkali baina ya
wabunge, huku wengi wao wakieleza kuwa hatua hiyo ina lengo la
kulifanya Bunge kukosa meno ya kuisimamia Serikali.
Miongoni
mwa mambo yaliyozua mvutano katika kikao cha awali cha wabunge wote ni
suala la muda wa wabunge kuchangia bungeni na jinsi wanavyotakiwa
kupangwa kulingana na idadi yao kwa kila chama.
Bunge
linakusudia kuwasilisha azimio la kutaka kubadili kanuni ambazo
zilitarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika jana bungeni, lakini kutokana
na baadhi ya mapendekezo kupingwa, hatua hiyo iliahirishwa hadi leo.