Wakati
Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho, Kamati Kuu ya
Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulibana Bunge
kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na Spika na
wasaidizi wake.
Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8, mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.
Kambi
ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa kwa hoja binafsi za baadhi
ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Maji), James
Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari, ambaye hoja yake ilihusu
utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.
Jana,
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Kamati
Kuu ilibaini kwamba matukio yaliyotokea katika kikao 10 yalitokana na
meza ya spika kutofuata kanuni.