Thursday, March 28, 2013

MBUNGE SALIM HEMED HAMIS AANGUKA GHAFLA


Mbunge wa chambani (CUF) Visiwani zanzibar Salim Hemed Hamisi ameanguka ghafla akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake

Mbunge huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya afya yake amefikwa na dhahama hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward Lowasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Wednesday, March 27, 2013

DIVA wa CLOUD FM AONYESHA KADI YAKE HADHARANI YA CHAMA CHA CHADEMA, JIONEE MWENYEWE

Ms Loveness Diva

Mwanachama halali wa CHADEMA

SIKU CHACHE BAADA YA KUFUNGA NDOA JACK WA CHUZ YADAIWA KAIBA MUME WA MTU



Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa blog hii kribuni tulikuletea habari juu ya Jack wa Chuz kufunga ndoa na kubadili dini kwa habri zilizoko ni kwamba baada ya saa 48 tu Jack kufunga ndoa ymekuja mapya kabisa baada ya dada Mariam Omary anayedai Jack Chuz kamchukulia baba(Gardner Dibibi) watoto wake akiwa na mwanaye.
Mwanamke huyu mwenye jina la Marium Omary inadaiwa kuwa na mahusiano na Gadner Dibibi kwa muda wa miaka mitatu sasa na kufanikiwa kupata mt0to mmoja wa kiume.
Dada huyu ambae anishi Kigogo jijini dar es salaam alisema siku ya tukio ya ndoa ya Gadner alimuaga kuwa anasafiri anaenda Morogoro hivyo hatakuwepo dar lakin baada ya muda dada huyu alipata taarifa kutoka kwa watu kuwa mumewe anafunga ndo na mwanadada Jack wa Chuz

Dada huyu alialamika na kusema kuwa Jack wa Chuz anajua kila kitu kuhusu yeye na Dibibi na kusema
“Hakuna asichokijua kati yangu na Dibibi, kwa usalama wake Jack aniachie mume wangu,” alilalama mwanamke huyo.
Baada ya Jack kulizwa swala hili alisema hivi ‘’baba wa mtoto anayemjua ni mama peke yake na isitoshe kuzaa naye isiwe sababu kwani yeye hakumuoa’’
Na Dibibi naye alikuwa na haya ya kusema
“Alikuwa demu wangu na kuzaa mtoto isiwe sababu. Hata hivyo, ukweli wa baba wa mtoto anayejua ni mama. Sikumtolea mahari wala kumvalisha pete ‘so’ hana kizuizi na ndoa yangu,” alisema jamaa huyo kisha akakata simu’’

KWA WALE WAPENDA TATOO ANGALIA MADHARA YAKE KWENYE MIILI YETU

Hii ni kwa wale wote wapenda kujichora miili ya kwa inayojulikana kama tattoo

UJUMBE WA FIFA KUSIKILIZA WAGOMBEA TFF APRILI 16

tff_LOGO1SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe huo ambao moja ya shughuli zake kuwasikiliza wote walioenguliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na hawakuridhika na uamuzi huo, utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka huu.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na kutoa ripoti kwa mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa mwongozo.
Ujumbe huo utakutana na pande mbalimbali zinazohusika wakiwemo wagombea, kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia ujumbe huo unatarajia kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi wa viongozi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika kuwa hawakutendewa haki na wangependa shirikisho hilo liingilie kati.

‘Siri ya Kuuawa Zitto Yafichuka’ – Sio Kweli.

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

TIGO yazindua Ofa ya bei moja kupiga simu kwenda mitandao yote

Meneja wa Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi, kushoto kwake Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma .
Mtaalam wa ofa za bidhaa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupiga simu kwenda mitandao yote ndani ya nchi kwa bei moja na punguzo la 20% kupiga nje ya nchi.

Albam ya Justin Timberlake yauza kopi 968,000 katika wiki ya kwanza

Albam mpya ya Justin Timberlake, “The 20/20 Experience” imekamata nafasi ya kwanza kwenye Billboard 200 chart, kwa kuuza kopi 968,000 katika wiki yake ya kwanza, kwa mujibu wa Nielsen SoundScan.
justin-timberlake-the-2020-experience-photo-shoot-tom-munro-main-600x450
“20/20,” ilitoka March 19, na ndio albam aliyouza zaidi katika wiki ya kwanza. Albam yake ya mwaka 2006 “FutureSex/LoveSounds,” iliuza kopi 684,000 na ile ya kwanza aliyoitoa mwaka 2002, “Justified,” iliuza kopi 439,000.
Mauzo huzo hayo ya “20/20′s” ni makubwa zaidi tangu SoundScan ianze kuchukua data za mauzo ya albam mwaka 1991.
Albam ya kundi la zamani la Timberlake, ‘N Sync, “No Strings Attached” iliuza kopi milioni 2.42 katika wiki ya kwanza na kukamata na kuongoza chart ya Billboard 200, April 8, 2000.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 27 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS HAYA HAPA

.


.
.

Dk Slaa awatuhumu Usalama wa Taifa


Dar es Salaam. 
Kwa ufupi
“Chadema ni chama makini na hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote wala idara yoyote inayotumiwa na baadhi ya watu ili kutaka kukizohofisha,” alisema Dk Slaa ambaye mara kwa mara amekuwa akilalamika kuchezewa rafu.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa ameanza kuisakama Idara ya Usalama wa Taifa kuwa wanatumia mbinu mbalimbali kuwahujumu na kwamba mbinu zinazofanywa na idara hiyo ni kueneza propaganda walizodai za uongo dhidi yao.

Akizungumza jana makao makuu cha chama hicho jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema: “Tumezibaini mbinu zinazofanywa na Usalama wa Taifa kwa kutumiwa na CCM kueneza propaganda za uongo dhidi yao kwa lengo la kukichafua chama, lakini haziwezi kufanikiwa kwani tayari tumegundua mbinu zao.

ROSE NDAUKA: KAJALA AJIPANGE KUTIMIZA NDOTO ZAKE


Habari na saluti5
NYOTA wa filamu, Rose Ndauka amemzungumzia msanii mwenzie wa filamu, Kajala Masanja aliyeponea chupuchupu kwenda jela miaka mitano na kusema kuwa, anachoamini ni kwamba sasa Kajala atajipanga na kuyafanya maisha yake yaende kama alivyokusudia hatimaye kutimiza ndoto zake.Saluti5 ilizungumza na Rose ili kupata maoni yake juu ya kuachiwa huru kwa Kajala aliyekuwa jela kwa muda mrefu, ambapo alisema kuwa kikubwa ni kushukuru mungu kwa kuweza kwake kurudi tena uraini, lakini pia sasa ni wakati wa kuzijenga upya ndoto zake.
“Binafsi, siwezi kujua kwa sasa Kajala mwenyewe amepanga kitu gani juu ya maisha yake, lakini ninaamini atafanya yale anayayowaza katika akili yake, hususan kuhusiana na kuendeleza mipango yake ya kimaisha,” alisema Rose.

UGONJWA UTOKANAO NA KUWEKA LAPTOP MAPAJANI HUU HAPA

HATARII...UGONJWA UTOKANAO na KUWEKA  LAPTOP MAPAJANI MWAKO PINDI UTUMIAPO.Huu ndo ugonjwa utokanao na kuweka laptop mapajani.Kwa faida ya afya zetu thechoice inawakumbusha kuepuka kutumia laptop kwa mtindo huo na yakupasa kutumia mbinu mbadala ili kuweza kulinda afya zetu.

DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA AFIKISHWA MAHAKAMANI







Akiteta jambo na Issa Mnally  ndani ya mahakama kabla ya hakimu kuwasili. 

  Waandishi wa habari wakimpiga picha (Simbo) wakati akiingia mahakamani

JK: afunga rasmi mafunzo ya JKT ya muda mfupi kwa wabunge RUVU JKT

8E9U3088Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo  yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy Maro)

8E9U3018
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.

RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UZALISHAJI JKT RUVU

8E9U3121Mwakilishi wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana.8E9U3133Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mris8E9U3151Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU leo.8E9U3177Wabunge walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...