MSANII wa
nyimbo za muziki wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Baby Madaha
amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na maswala
ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la 'Kijibwa' kuwa
ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia kufanya kitendo hiko
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Msanii huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya
wasanii hususani wa kike kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana
wenye umri mdogo huku wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi
matakwa yao ya kingono
Alieleza
kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii
hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo
kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao
"Unajua hao
wasichana wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana
kiumri ndio maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na
ndipo hapo jina la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo
na mbwa unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda
tu " aliongezea kuwa
"Kwa sababu
mvulana huyo anapewa kila kitu ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye
anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo hamna mapenzi zaidi ya utumwa na
kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru wa kuwa na maamuzi ya mambo yake
binafsi" alisema Madaha
Kutokana na
hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano ambayo
hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha hivyo
mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha
kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka
Alitoa wito
kwa wasichana hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni
kujiamini na kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na
kutoyaogopa maisha hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya.












Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa
mahututi MOI.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya
Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya
kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea
amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa
tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni
yake ya tano.








Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo
za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa
Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.
Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey
Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba
huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.





