Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).
Saturday, March 09, 2013
RAIS KIKWETE NA ABDULRAHAMAN KINAN WAMJULIA HALI MHARIRI MTENDAJI WA HABARI CORPORATION ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI
Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).
Friday, March 08, 2013
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU MWANZA AUMBULIWA NA PICHA ZA UCHI-BBM
DENTI wa
chuo kimoja kilichopo jijini Mwanza (jina tunalihifadhi) aliyefahamika
kwa jina la Fatma Omar amejikuta akiumbuka kwenye mtandao wa BBM baada
ya picha zake chafu alizokuwa ‘akimfoadia’ mpenzi wake kuvuja.
Picha hizo
zikiwemo zinazomuonesha mwanadada huyo mwenye asili ya Kiarabu akiwa
amevaa nguo ya ndani tu zinapatikana mtandaoni na inadaiwa kuwa mwenyewe
amejikuta akiugua ghafla baada ya kubaini ameaibika.
Baada ya Ijumaa kuzinasa picha hizo na kubahatika kupata namba zake,
mwandishi wetu alimpigia simu Fatma ili kujua kilicho nyuma ya pazia ya
picha hizo ambapo alifunguka:
SAKATA LA JACK PATRICK KUJIUZA LACHUKUASURA MPYA BAADA YA SERIKALI KUVUNJA UKIMYA
BAADA
ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’
kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo
ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon
Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya
shirikisho hilo kilitonya kuwa, Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye
mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo
jijini Dar.
TUME YA UCHUNGUZI WA KUSHUKA UFAULU KIDATO CHA NNE 2012 YAWAOMBA WATANZANIA KUTOA USHIRIKIANO.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya kuchunguza
kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka
2012 Prof. Sifuni Mchome (katikati)akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa zoezi la ukusanyaji wa maoni
kutoka wadau mbalimbali. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) na Bi.Tunu Temu mjumbe wa
Sekretarieti ya Tume hiyo.
…………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa -MAELEZO, Dar es salaam.
Tume
ya Taifa iliyoundwa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda kuchunguza kushuka
kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012
imewaomba watanzania kuipa ushirikiano kwa kutoa maoni yao ili iweze
kukamilisha majukumu iliyopewa kwa muda na ufanisi mkubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo
Prof.Sifuni Mchome ameeleza kuwa tume hiyo ilianza kazi mara baada ya
kuzinduliwa na Waziri mkuu tarehe 2 mwezi Machi mwaka huu na kufafanua
kuwa jukumu lililopo sasa ni kuanza kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa
watanzania ili kubaini sababu za matokeo mabaya ya mtihani huo.
Amesema kuwa
tume hiyo pamoja na mambo mengine imepewa jukumu la kutoa mapendekezo
ya hatua za kuchukua ili kukabiliana na tatizo la mwenendo wa kushuka
kwa kiwango cha elimu nchini huku mapendekezo hayo yakizingatia kipindi
cha muda mfupi , kati na kipindi cha muda mrefu.
Prof.
Sifuni ameeleza kuwa tume hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia
hadidu mbalimbali za rejea zikiwemo kubainisha sababu za matokeo mabaya
ya kidato cha nne 2012, sababu za kushuka kwa kiwango cha
ufaulu, nafasi ya Halmashauri katika kusimamia elimu ya sekondari katika
halmashauri zake.
Rejea
nyingine ni pamoja na pamoja na kuanisha sababu nyingine zinazoweza
kuwa zimechangia hali ya matokeo hayo pamoja na kutoa mapendekezo ya
hatua za kuchukua mara moja kwa wanafunzi 240,903 waliofeli mitihani yao
kwa kupata daraja sifuri.
Amefafanua
kuwa tume katika kutekeleza majukumu yake itapitia mitaala na
mihutasari ya Elimu ya Msingi na Sekondari, kutathimini kiwango na
mazingira ya ufundishaji na ufunzaji, kuangalia mfumo wa upimaji na
tathmini ya mitihani pia usimamizi na uendeshaji.
Pia
pamoja na mambo mengine tume itatathmini mchango wa jamii na wazazi/
walezi katika maendeleo ya wanafunzi, hali ya upatikanaji wa chakula cha
mchana, upungufu wa majengo ya shule,madarasa, maabara na maktaba.
Vilelevile
tume hiyo itafuatilia mwamko wa wazazi katika kufuatilia mkazo wa
eliimu kwa watoto na suala la mmomonyoko wa maadili unaotokana na ukuaji
wa utandawazi hususan teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kutathmini
athari ya mfumo wa ufundishaji wa mikondo miwili iliyopo katika shule
za Zanzibar.
Aidha
mwenyekiti wa Tume hiyo amebainisha kuwa tume itaanza rasmi kukutana na
wadau mbalimbali kwa lengo la kupata maoni kuanzia tarehe 11 mwezi huu
kwa kuanza na mkoa wa Dar es salaam, Zanzbar na maeneo mengine nchini
kwa kukutana na viongozi wa ngazi mbalimbali za Wizara, Mikoa, Wilaya,
Halmashauri, Kata, Shule, Taasisi mbalimbali za kijamii na wananchi kwa
ujumla na pia kuwasilisha maoni kwenye tume kupitia Mwenyekiti wa Tume,
Tume K4-2012, S.L.P 5909 Dar es salaam au kupitia simu 0737206038, Barua
pepe: maoni@tumek4.go.tz au kwa kutembelea Tovuti ya tume ya www.tumek4.go.tz.
DIAMOND ATINGA KWENYE MAULIDI AKIWA KAVAA KANZU HERENI NA CHENI .JIONEE MWENYEWE
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Tandale, Dar ambapo mama yake aliyemtambulisha kwa jina la Aunt Shani aliandaa maulidi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Akiwa mmoja wa waalikwa, Diamond alinaswa akiomba dua sambamba na rafiki yake aitwaye Remeo Jones ‘RJ’ huku akiwa amevaa kanzu safi na balaghashia lakini akaharibu kwa kuvaa hereni na cheni.
Kitendo hicho kiliwachefua Waislam ambapo baadhi walifikia hatua ya kumchana laivu kuwa, alichokifanya kilikuwa kinyume na Uislam.
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: SALMA KIKWETE, DIAMOND, NANCY SUMARI NA WENGINE KIBAO WAFUNGUKA
Leo
ni miaka 99 tangu kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani
iliyoadhimishwa kwa mara ya kwanza March 8, 1914 ambapo mwanzoni ilikuwa
ikijulikana kama ‘Siku ya wanawake wafanyao kazi duniani’.
Ni siku ya kuwapa heshima wanawake, kuwapongeza na kuwaonesha upendo katika jitihada zao kiuchumi, kiasiasa na kijamii.
Katika nchi zingine siku hii
imefunika ile ladha ya kuchanganyika na siasa na kuwa siku ya wanaume
kuelezea upendo wao wanawake kama ilivyo Mother’s Day na Valentine’s
Day. Soma jinsi watu mbalimbali mashuhuri nchini (na kwingineko)
wanavyoizungumzia siku hii.
Mama Salma Kikwete
Leo ni siku ya wanawake
Duniani.,ni siku ya kujitazama kama Taifa juu ya hali ya wazazi hawa na
walezi wa Taifa hili. Ni siku ya kujipima na kutathimini namna gani,
wanawake wamewezeshwa kujitambua na kushirikishwa katika mipango ya
maendeleo ya jamii yetu. Tunapofikiri kama Taifa ni namna gani tunaweza
kujikomboa katika Umasikini tulionao ni lazima mipango hiyo iende
sambamba na mipango na mikakati ya ukombozi kwa wanawake wa Taifa hili.
Nancy Sumari
Even when we are a mess, we still
put on vests with ‘S’ on our chests, Oh yes, we are Super Women, and
today is our day…Happy Womens day!!
Diamond
HAPPY WOMEN’S DAY……. I LOVE MY
MAMA MORE THAN ANYTHING IN THIS WORLD….SHE HAS BEEN THROUGH ALOT WITH
ME…… MUCH LOVE TO ALL WOMEN’S IN THIS WORLD…..!!
Tamko Kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM):Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda
Katibu wa CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye
--
Chama
Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa
na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri
Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia
Jumatano Machi 6, 2013.
Chama
Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom
Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na
Watanzania wote.
CCM
tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na
kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na
kukomesha matukio ya namna hiyo.
Aidha,
Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri,
Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda,
wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi
Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013
Statement by United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt on the Attack on Journalist Absalom Kibanda
United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt
--
We
strongly condemn the attack against Tanzania Editors Forum Chairman and
Group Managing Editor of New Habari Corporation Absalom Kibanda on the
evening of Tuesday, March 5. We also welcome reports that this crime
will be investigated by Tanzania's law enforcement agencies to identify a
motive and the perpetrators.
A free, independent media is fundamental to any democracy. The work of journalists is essential to educate the public and to encourage the free flow of ideas in society. Therefore attacks against media professionals threaten the very foundation of democracy. We call for a thorough investigation, arrest, and prosecution of those involved in this crime.
A free, independent media is fundamental to any democracy. The work of journalists is essential to educate the public and to encourage the free flow of ideas in society. Therefore attacks against media professionals threaten the very foundation of democracy. We call for a thorough investigation, arrest, and prosecution of those involved in this crime.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL YA INDIA BW SUNIL MITTAL IKULU, DAR ES SALAAM
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India
Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Sam Elangallor.
Rais Jakaya
Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Airtel pamoja na Waziri wa
Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw.
Sunil Mittal na ujumbe wake alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana
jioni
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Mkurugeni Mkuu mpya wa Airtel
Tanzania Bw Sunil Colaso na aliyemaliza muda wake Bw Sam Elangallor
(kulia).Picha na Ikulu
WAZIRI WA UTALII ZAMBIA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA MAONYESHO YA (ITB) BERLIN
Waziri
wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia Masebo kipokea
zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki Mara baada ya kutembelea katika banda la Tanzania na kukutana na
viongozi Kadhaa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanya nao
mazungumzo kuhusiano na ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania katika
masuala ya Utalii Bodi ya Utalii Tanzania inaongoza ujumbe wa
Wafanyabiashara ya Utalii zaidi ya 43 kutoka nchini Tanzania katika
maonyesho ya dunia ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin
jijini Berlin UjerumaniWaziri
wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia
Masebo akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya
Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa akizungmuza wakati waziri huyo
alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya (ITB) jijini Baerlin
jana katikati ni Katikati ni Balozi Chiti Balozi wa Zambia nchini
Ujerumani
HII NDIO TAARIFA YA ALIEUWAWA NA SIMBA AKIWA KWENYE TENDO LA NDOA
Mashuhuda wanasema wakati mwanamke huyo akishambuliwa na Simba, boyfriend wake alifanikiwa kukimbia akiwa uchi huku akiwa bado amevaa kinga (Condom)
Mwanaume huyo alikimbia kuomba msaada akiwa mtupu bila nguo lakini wengi hawakumuamini wakijua ana upungufu wa akili.
Baadae ndio watu walimuamini na
kumsindikiza polisi alikopewa msaada wa polisi na askari wa Wanyama
pori Zimbabwe na kuelekea mpaka kwenye eneo la tukio ambako ilifyetuliwa
risasi moja na kukuta mwanamke ameshafariki tayari huku akiwa
ametapakaa damu mwili mzima na kujeruhiwa vibaya mwilini ikiwemo
shingoni ambapo waumini wa kanisa moja karibu na hapo walitoa ushuhuda
wa kuona Simba 7 kwenye eneo la tukio. Wakati huohuo mwili wa mwanaume mmoja ambae hakutambulika kirahisi ulikutwa akiwa ameshafariki karibu na ZESA social club huku My Zimbabwe wakiripoti mwanaume huyo kushambuliwa na Simba muda mfupi uliopita. Tukio jingine liliripotiwa kwamba mwanaume aitwae Musinje pia alishambuliwa na Simba na kufariki dunia wakati akitoka kwenye club ya usiku ambapo mwili wake ndio uligundulika baadae ambapo Wakazi wa Kariba wanasema ni watu watatu wameuwawa na Simba kwenye eneo hilo ndani ya saa 24. |
Vigogo wavuliwa madaraka TBS
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imewavua madaraka wakurugenzi wawili.
Mwenyekiti
wa Bodi hiyo, Profesa Cuthbert Mhilu alisema jana kuwa waliovuliwa
madaraka ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora, Dominic Mwakangale
na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Huduma za Vifungashio, Kezia
Mbwambo.
Profesa
Mhilu alisema hatua hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kufanya usaili kwa
vigogo mbalimbali wa shirika hilo ulioanza juzi asubuhi hadi saa 3:00
usiku.
Katika
taarifa hiyo, Profesa Mhilu ambaye hakutaka kuingia kwa ndani juu ya
hatua hiyo, alisema viongozi hao watapangiwa kazi nyingine.
“Kwa
kipindi kirefu, TBS imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali
yaliyochangia kudhoofisha utendaji wa watumishi na kulifanya shirika
kukosa tija na ufanisi. Bodi imeonelea ikae mara moja kuchambua,
kujadili na hatimaye kufikia uamuzi wenye lengo la kuweka mazingira bora
na kuwezesha kuanza utatuzi wa matatizo ili shirika lifikie malengo
yake.”
HII NDIO DAWA YA WEZI: SIKU HIZI HAKUNA KUWAUWA NI ADHABU KAMA KAWA:
MWIZI WA BETRI YA GARI ANAEJULIKANA KWA JINA MOJA TU SEFA AKISURUBIWA KWA STAILI YA AINA YAKE KWA KUFUNGWA KWENYE NGAZI PAMOJA NA BETRI ALIYOIBA |
MWIZI HUYO AKIENDELEA KUTESEKA KATIKA NGAZI HIYO |
POLISI WAMEFIKA KUMWOKOA MWIZI HUYO KATIKA MATESO HAYO |
BADO WANANCHI WANAHASIRA NA MWIZI WAO WAKIDAI WAACHIWE WAMFUNZE ADABU MAANA AMEWASUMBUA SANA ENEO HILO LA UYOLE |
POLISI WAMEZIDIWA WAMEPOKONYWA MTUHUMIWA WAO KIPIGO KINAENDELEA |
IPO HAJA YA KUJIFUNZA KUTOKA FINLAND- MASELE
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini, Mhe.
Stephen Masele, akimuonesha Balozi wa Finland nchini,Sinikka Antila
ramani ya maeneo ambapo kuna madini na uchimbaji unaendelea.
Serikali
imesema inahitaji kujifunza zaidi kutoka Finland hususan katika
uchimbaji wa madini ili kuwa na uchimbaji wenye tija kwa taifa.Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Stephen Masele
alipokutana na Balozi wa Finland nchini, Sinikka Antila.Masele alisema
Tanzania inahitaji kujifunza masuala ya uchimbaji madini kutoka Finland
kwa kuwa mazingira ya uwekezaji ya nchini humo yanashabihiana na
mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania.“Unajua kampuni kubwa
zinazojishughulisha na uchimbaji madini nchini Finland siyo za hapo
Finland bali ni kampuni kutoka nchi nyingine yani multi-nationals na
hili pia ndilo linalofanyika hapa kwetu Tanzania” alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)