Mhe. Sophia
Simba ( Mb) akichangia ajenda kuhusu Utokomezaji na Umalizaji wa
Unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike wakati wa mkutano wa 57
wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake (CSW). Mkutano huu wa
wiki mbili unaendelea hapa Umoja wa Mataifa na Mhe. Simba anaongoza
ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyeketi nyuma ya Mhe.
Waziri ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi
Makatibu
Wakuu, Kijakazi Mtengwa ( Tanzania Bara) na Fatma Gharib Bilal (
Zanzibar ) wakifuatilia majadiliano kuhusu utokomezaji na umalizaji
unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Mhe. Sophia
Simba akishiriki majadiliano ya mada iliyohusu umuhimu wa Takwimu
katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia, Waziri alikuwa mmoja wa
wazungumzaji wakuu katika mjadala huo. mjadala ulikuwa umeandaliwa na
UNFPA, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 57 wa CSW,kulia kwa Waziri ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Bi Anne -Brigitte Albractsen.
Kutokana na
wingi wa washiriki wa majadiliano kuhusu umuhimu wa Takwimu katika
kushughulikia unyanyasaji kuwa wengi kupitia uwezo wa ukumbi, baadhi ya
washiriki walilazimika kukaa chini kama inavyoonekana katika picha