Friday, November 14, 2014

RAIS KIKWETE ATOKA WODINI, FAMILIA YA NYERERE YATUMA SALAMU

Rais Jakaya Kikwete akiagana na daktari bingwa, Edward Schaeffer baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore nchini Marekani, alikofanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Rais Jakaya Kikwete ametoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“RPP tutashirikiana na familia, marafiki na mamilioni ya Watanzania kumwombea Rais Kikwete aweze kupona haraka. Rais Kikwete ni jirani yetu na mtetezi mkubwa wa kanda hii katika kupata ukombozi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi,” ilisema taarifa ya RPP kwa umma iliyotolewa na Rais wa chama hicho, John V Karuranga.
Aondoka wodini
Wakati Rais Kikwete akiondoka wodini, alikuwa anatembea akiwa amesindikizwa na daktari bingwa, Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins na mkewe Salma.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa juzi ilisema: “Afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea na akiwa katika hoteli hiyo, ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.”
Iliongeza: “Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.”
Taarifa hiyo ilisema: “Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete atakuwa katika hoteli maalumu (haikutajwa), iliyo na uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins.” Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...