Friday, November 14, 2014

NDEGE YA KIJESHI YAANGUKA

Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria.Ndege hiyo ni ya pili kuanguka.
Helikopta ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili .
Ajali ya hivi karibuni imetokea viungani mwa mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa Jihad.
Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa Cameroon . Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji wa Yola wanasema walisikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .
Baada ya kuanguka ikafuatiwa na mfulurizo wa milipuko , kwani inaaminiwa kuwa ilikuwa inasafirisha silaha na zana nyingine za kijeshi kwa wanajeshi wanaopigana Boko Haram. Haijawa wazi ikiwa mtu yeyote aliekuwa ndani ya ndege hiyo amenusurika na kifo .
Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria
Baada ya kusikia kelele , baadhi ya wanafunzi walianza kukimbia wakihofia kuwa wapiganaji wa jihad walikuwa wakiwashambulia Hii ni helikopta ya pili ya kijeshi kuanguka katika mji wa Yola wiki hii.
Wakati huo huo katika eneo la kaskazini kuna taarifa kuwa mji wa Mubi hauko tena mikononi mwa Boko Haram baada ya askari na vikosi vya usalama vya eneo hilo, wakiwemo wawindaji kuurejesha tena.
Lakini katika sehemu hii ya kaskazini ya jimbo la Adamawa bado hali ni mbaya na watu wamekuwa wakiukimbia mji huo ambao makundi ya Jihad yamekuwa yakijaribu kuuteka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...