Wednesday, August 20, 2014

FURSA YA MIKOPO KATIKA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

Serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
" Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu."Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz.na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...