Wakili wa Sheikh Ponda |
Wakili
wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa
Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi
katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor
Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya vyombo vya dola kumuondoa
Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba
ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI) alikokuwa akipatiwa
matibabu na kisha kumwamishia katika gereza la Segerea.
Wakili
Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa
juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka
kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda
aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama
wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba
atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa
Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Kwa
kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana ….ila
tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za
usoni’alisema wakili Jumaa.
Agosti
14 mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamia
katika wodi hiyo ya MOI na wakili wa serikali Tumaini Kweka alimsomea
shitaka Ponda ambaye anakabiliwa na kesi hiyo ya Jinai Na.144 ya mwaka
huu.