Waziri
wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na
Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko
Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao
mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe
ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha
na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
Waziri
wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness
Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa
habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika
Kusini hivi karibuni.
waandishi
wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua
hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima
uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.