Wednesday, June 05, 2013

RONALDO AGOMA KUONGOEZA MKATABA REAL MADIRD

ronaldo 7d195

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameziweka kiporo Manchester United na Paris Saint-Germain baada ya kusema hataongeza Mkataba Real Madrid baada ya 2015.Real imegoma kumuuza Mreno huyo msimu huu wakati United na PSG zinabakiwa mstari wa mbele atakapotiwa sokoni.Alex Ferguson alimuuza Ronaldo kwenda Madrid mwaka 2009, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ameeleza mara kadhaa hivi karibuni kwamba hana furaha sana katika Jiji hilo na Hispania.
Rais wa Madrid, Florentino Perez alisema anatarajia kuona Ronaldo akitungikia daluga zake katika klabu hiyo, lakini inaonekana atatafuta klabu nyingine miaka miwili ijayo.
Ikiwa Ronaldo atakuwa mkweli kwa kauli zake, ataondoka bure, kitu ambacho Madrid hawatapenda baada ya kumsajili kwa Pauni Milioni 80.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...