Monday, February 18, 2013

TASWIRA YA MKUTANO WA CUF MOROGORO, PROF LIPUMBA,MAALIM SEIF HAMAD WAPOKEWA KWA MAANDAMANO.


Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhala uliopewa jina la mchakamchaka mpaka 2015 ambao ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhala wa mchakamchaka mpaka 2015 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
 Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kushoto,
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi kulia wakifuatilia matukio kabla ya viongozi wakuu wa chama hicho kuhutubia wananchi.
 Wafuasi na wanachama wa Cuf wakiwa wamekunja ngumi juu wakati viongozi wakuu wa chama hicho wakihutumia maelefu ya wakazi wa Morogoro.
 Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akisalimia wananchama na wafuasi wa chama hicho mara baada ya kuwasilia katika ofisi za wilaya za chama hicho mkoani hapa.
 Wananchama na wafuasi wa chama hicho wakiwa katika maamandano kutoka katika ofisi za chama hicho mtaa wa Boma kuelekea uwanja wa shule yamsingi Kiwanja cha Ndege katika mkutano wa hadhala.
 Sehemu ya magari kutoka Dar es Salaam ambayo yamebeba wanancha na wafuasi wa chama hicho yakielekea katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege.
 Wanachama wa Cuf wakiwa katika maandamano huku Mwenyekiti wa Cuf Taifa Profesa Ibrahim Lipumba akiwa katika gari huku akiwapungia wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakati akielekea katika ofisi za wilaya hiyo mtaa wa Boma.

Mmoja wa wasanii akitumbuiza kabla ya viongozi kuhutubia.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...