Mwanariadha Oscar Pistorius alipokuwa katika
mashindano ya Olympic mwaka 2012 mjini London.
Mwanariadha na mshindi wa medali za dhahabu wa
Paralympic raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amekamatwa nyumbani kwake mjini Pretoria kwa kosa la kumuua
mpenzi wake baada ya kumpiga risasi moja kichwani na nyingine mkononi ,
majeraha yaliyopelekea kifo cha binti huyo.
Chanzo cha Pistorius kumsuti mpenzi wake bado
hakijaeleweka, japo fununu za awali zinadai uenda Pistorius
alijichanganya na kudhani amevamiwa na mwizi/jambazi kutokana na hali
mbaya ya uhalifu anayoikabili nchi ya Afrika Kusini.
Binti huyo Reeva Steenkamp, (30) mwanamitindo
alilenga kumsuprise Pistorius kwaajili ya valentine.
Msemaji wa Polisi aliliambia shirika la habari
la Reuters “tumekuta pisto ya mm9 eneo la tukio, na mtuhumiwa amepelekwa
kituoni kwaajili ya utaratibu mwingine”.
Pistorius mwenye miaka 26 maarufu kama “blade
runner” amekuwa ni mlemavu wa kwanza kushiriki Olympic mbali na
mashindano yao maalum ya Paralympic , hukimbia riadha kwa kutumia vifaa
maalum vilivyofungwa miguuni kwake, baada ya
kuzaliwa bila miguu yote miwili.
Mpenzi
wa Pistorius, Mwanamitindo Reeva Steenkamp aliyepigwa risasi na
kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment