Zimbabwe kuipigia kura Katiba mpya.
Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai
anasema nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa bunge na urais mwezi
Julai baada ya kupiga kura maoni juu ya katiba
mpya mwezi Machi.
Alisema hayo Jumatano baada ya waziri wa maswala ya katiba Eric
Matunenga kupanga tarehe ya Machi 16 kwa ajili ya
kupiga kura ya maoni.
Katika mkutano na
waandishi wa habari huko Harare , Matinenga alieleza wasi wasi wake kuwa
muda hautoshi na pengine muda zaidi huenda ukahitajika kwa ajili ya
uchaguzi wa Machi.
Baraza la kitaifa la
bunge (NCA) ambalo linajumiwsha makundi ya
harakati za kidemokrasia huko Zimbabwe limesema litapinga tarehe upigaji kura wa maoni hapo
Machi 16 mahakamani .
Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti
NCA Lovemore Madhuku amesema kundi lake linataka
serikali itoe kipindi cha mdahalo cha miezi
miwili hivi kabla ya wapiga kura kufanya uamuzi
wao juu ya katiba mpya.
Chama cha Bw. Tsvangirai
cha MDC na kile cha rais Robert Mugabe cha ZANU
PF wote wanaunga mkono mabadiliko hayo mapya.
Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini inataka katiba mpya iidhinishwe kabla ya Zimbabwe kufanya uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment