Thursday, February 14, 2013

Wabunge wa Tanzania kukomeshwa kwa kufuta Matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni

 

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya kamati kuondolewa pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3 zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (
Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilila akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge amesema Bunge linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja (LIVE) kupitia televisheni kwa  nia ya kukomesha vitendo vya baadhi ya Wabunge wanaokikuka kwa makusudi Kanuni za Bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila na hivyo kutoa picha mbaya katika jamii.
Akasema ili kurejeza maadili kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.
Akasema jamii imeendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi kutokana na kukiukwa kanuni hizo.
Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.
Ameahidi kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge, huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuitumia ipasavyo ofisi yake kupata  taarifa sahihi za kuwasaidia katika uandishi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...