DAR ES SALAAM,
Tanzania
MENEJIMENTI ya NMB imewaonya wateja wake na umma
kwa ujumla kuwa imegundua kwamba kuna taasisi inayojitambulisha kama
Tanzania Loans Society inadai kuwa mshirika wa benki hiyo katika kutoa
huduma za kibenki.
Taasisi hiyo imedaiwa kuwa kwa kutumia mtandao
wake wa intaneti imekuwa ikijinasibu kutoa mikopo ambayo fedha zake
zimeidhinishwa na NMB kupitia kwa mameneja wa matawi.
Aidha, Tanzania Loan Society pia inadaiwa kueleza
kwamba fomu za maombi ya mkopo na malipo ya usajili vinaweza kulipwa
kwa kutumia namba ya simu ya mkononi.
Menejimenti ya NMB imezidi kuwatahadharisha wateja
wake na umma kwa ujumla kwamba haina ushirika au makubaliano yoyote na
taasisi hiyo katika shughuli zake.
Imeongeza kuwa, NMB hutoa mikopo yake kupitia
matawi yake tu, na hakuna namna yoyote ambayo inaweza kusababisha
gharama za maombi ya mikopo au mikopo kutolewa kupitia simu za mkononi.
Menejimenti hiyo imesisitiza kuwataka wateja na
umma kwa ujumla kutojihusisha na taasisi hiyo katika shughuli yoyote
inayoihusu Benki ya NMB na kwamba haitahusika kwa namna yoyote na
matatizo yatakayojitokeza
No comments:
Post a Comment