Tuesday, February 26, 2013

Kocha wa Azam afungiwa na kupigwa faini kwa kuchojoa bukta.


Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
 Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.
Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

MeTL GROUP yapokea tuzo ya ubora na thamani ya nembo ikiwa ni ishara ya kukubalika na walaji.


Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Raha  Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia) aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga ( wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji  akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Na.Mo Blog Team
Taasisi huru ya Superbrands ambayo ni kubwa kuliko zote duniani, inayoratibu ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji, leo imekabidhi vyeti vinavyotambuliwa kimataifa vya utambuzi wa ubora wa bidhaa kwa kampuni zilizofanya vizuri nchini Tanzania kwa mwaka 2013/2014.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya kampuni.
Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake yapata miaka mine iliyopita.
Uamuzi na hatimaye utoaji wa tuzo husika unatoka baraza huru la wataalamu waliobobea katika masuala ya biashara, lakini lengo hasa likiwa ni ni kustawisha na kuhamasisha ari katika utoaji huduma zinazo zingatia ubora.
MeTL imekuwa moja wapo kati ya Makampuni yaliyopokea vyeti vya tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya tatu hapa nchini.

Tigo yaongeza kifurushi cha ziada kwenye huduma za Blackberry!

Tigo Tanzania imezindua kifurushi kipya cha Blackberry ambacho kitawapa wateja  fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwa bei nafuu zaidi kijulikanacho kama Blackberry Social Plan.
Kifurushi hiki kitawawezesha wateja wa Tigo kutumia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Whatsaap na mingineyo  ipasavyo kwa gharama nafuu zaidi. Watumiaji wanaweza kujiunga na kifurushi cha siku, wiki au mwezi kutokana  na matumizi yao.
Ndg. William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo alisema kuwa “Mitandao ya kijamii imezidi kuja juu baada ya watumiaji kuongezeka maradufu na kuitumia kwa matumizi mbalimbali kama kutafuta habari, kutumiana ujumbe n.k.  Mitandao hii hupatikana kiurahisi sana bila gharama yeyote hivyo kuifanya idadi ya watumiaji kukua kwa kasi kubwa sana. Watumiaji wa kifurushi cha blackberry watanufaika na huduma mbalimbali muhimu ambazo zitawasaidia kujiendeleza kibiashara na kikazi kwa kuwaweka karibu na wafanyabiashara au wafanyakazi wenzao pamoja na wateja  wao. Huduma kama BBm na Whatsapp zitawawezesha kujadili mambo mbalimbali kama vile wako mahali pamoja hivyo kupunguza haja ya mikutano ya kila mara. Watumiaji wataweza kufanya haya yote wakiwa majumbani kwao, au kwenye mizunguko yao mbalimbali.”
Mr. Mpinga aliendelea kwa kusema kuwa “tuliamua kuzindua kifurushi hiki  ili kuwapatia wateja wetu huduma mbadala juu ya kifurushi cha Blackberry na hivyo kuongeza thamani ya huduma zetu.”
Kutumia huduma hii mteja inabidi ajiunge kwa kutuma ujumbe kwenda 15518 wenye neno BBS1 kutumia kifurushi cha siku, BBS7 kutumia kifurushi cha wiki, na BBS30 kutumia kifurushi cha mwezi.  Gharama za siku ni shilingi 499, za wiki shilingi 2,999 na za mwezi shilingi 11,999. Kwa kutumia kifurushi hiki wateja wataweza kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo kabisa.

Khadija Kopa, Isha Mashauzi Watoana Kijasho DAR LIVE.

Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, akionesha umahiri wake wa kutikisa nyonga.
Mashabiki wanaomfagilia Isha Mashauzi wakiwa wamevamia steji baada ya kuwadatisha.
Aziza Abul ‘Bonge’ wa TOT Taarab akikamua.
Malkia wa mipasho akiserebuka na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani kumtunza.
Wakali Dancers wakiwajibika jukwaani.
Shabiki akimtunza Malkia wa mipasho baada ya kukunwa na mipasho.
Isha Mashauzi akikamua.
Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.
WAKALI wa miondoko ya muziki wa mwambao nchini, Malkia wa miondoko hiyo, Khadija Kopa akiwa na Kundi la TOT Taarab na Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ jana waliugeuza Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kuwa uwanja wa mapambano baada ya kushindana kutoa burudani kwa kuonesha makali yao na kuwafanya mashabiki kila mmoja kumtaja mshindi wake.
Kabla ya wakali hao kuanza kuhenyeshana jukwaani burudani hizo zilianza kwa kunogeshwa na shoo kali ya washiriki wa shindano la Mic King linaloendeshwa ukumbini hapo kila Jumapili. Baada ya washiriki hao wanaowania gari, kundi la Wakali Dancers lilivamia jukwaa na kufanya vitu vyake pia.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

SIMBA SC WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARURA


Msemaji wa klabu ya simba Ezekiel Kamwaga akizungumza na Waandishi wa Habari  leo mchana 


KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC jana, kimefikia uamuzi wa kuitisha Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu hiyo, ambao ajenda yake itakuwa moja tu, kujadili mwenendo wa timu katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba siku na mahali ambako Mkutano huo utafanyika vitatajwa wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha, Kamwaga alisema kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa Simba SC aliyejiuzulu na kwamba uongozi upo pamoja. “Hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa klabu ya Simba aliyejiuzulu. Uongozi upo pamoja na mambo yote yatajadiliwa kwenye mkutano huo wa dharula,”alisema.
Akiuzungumzia mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kamwaga alisema kwamba timu itaondoka Alfajiri ya Ijumaa kwenda Angola kuwavaa wenyeji wao, Recreativo de Libolo.
Alisema mechi hiyo itafanyika Jumapili mjini Calulo, umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Angola, Luanda.
“Kwa mujibu wa kanuni za CAF (Shirikisho la Soka Afrika) kama umbali wa mji ambao inachezwa mechi unakuwa ni zaidi ya kilomita 200, timu mwenyeji inatakiwa kumsafirisha mgeni kwa ndege, kwa hivyo ni matumaini yetu, wenyeji wetu watakuwa tayari wametutayarishia ndege, kwa kuwa hatuwezi kusafiri kwa basi kwa zaidi ya saa nne,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba, Mkuu wa msafara wa timu atakuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans Poppe, wakati upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utawakilishwa na Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji pia, Muhsin Balhabou.
Kamwaga alisema kikosi kamili cha Simba kitakachokwenda Angola kitatajwa Alhamisi kwa kuwa leo ni mapema sana, kwani wanahofia anaweza kuumia mchezaji yeyote wakati amekwishatajwa kuwemo kwenye safari.
Simba SC ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza na Libolo wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ili isonge mbele, inatakiwa kushinda 2-0.
Mwaka 1978, Simba iliwahi kufanya maajabu ikitoka kufungwa 4-0 na Mufulira Wanderers ya Zambia mjini Dar es Salaam katika michuano hiyo hiyo na kwenda kushinda 5-0 ugenini, hivyo kusonga mbele. 

Baada ya habari kuenea kuwa kakamatwa na MADAWA ,MSANII TIMBULO HUU NDO UJUMBE ALIO UANDIKA BBM


VODACOM MAHELA YAWAKUTA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO


 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina Nkurlu Meneja Uhusiano,Benjamin Michael Maneja wa Huduma za Ziada na Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe,Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

Monday, February 25, 2013

RAGE: TUTAFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MATOKEO HAYA


Na Dina Ismail
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kutoa uamuzi mgumu kuhusiana na mwenendo mbaya ulionayo timu hiyo katika ligi kuu ya Vodacom.
Aidha, Rage amekanusha taarifa za kujiuzulu kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema kwamba kamati ya utendaji ya Simba ilitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao.
Alisema kikao hicho kitajadili kwa kina hali iliyopo sasa ambayo imesabababisha timu yao kupoteza hata matumaini ya kutetea ubingwa wao.
“Tutakuna baadaye leo na kujadili hali hii maana tukiiacha hivi hivi inaweza kutuletea madhara makubwa sana…pia tutatoa maamuzi mazito baada ya kikao chetu,”alisema.
Kuhusu na taarifa za kujiuzulu kwake, Rage alisema anashangazwa na taarifa hizo zinapotoka kwani kama atafikia uamuzi huo ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia hatua hiyo.
“Mimi sijasema nitajiuzulu jamani hata hiyo taarifa yenyewe ukiisoma haileweki, hivyo nawaomba wanasimba kutulia kuona kipi kitakachofuata,”aliongeza Rage
Simba imeonekana kusuasua sua katika ligi hiyo baada ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha sambamba na kuamulia vipigo katika mechi zake.
Hali hiyo ilianza kujitokeza tangu mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambao ulipelekea kutoka kileleni hadi kushika nafasi ya tatu.
Aidha, tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, Simba imeshinda mechi mbili dhidi ya African Lyon 3-1 na Tanzania Prisons 1-0, huku ikitoka sare mbili dhidi ya JKT Ruvu na JKT Oljoro kwa bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar juzi.

MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVA AL MAARUFU KWA JINA LA ''TIMBULO''''' AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO BURUNDI.



Msanii wakizazi kipya, anae ondoka na mitindo ya bongo flava Ally TIMBULO kuna tetesi zinasema kuwa amekamatwa na dawa zakulevya Mjini Bujumbura .......

Habari zinadai kwamba Msanii huyo alikuwa na mpango waku endesha tamasha Mjini Bujumbura mwezi wa 4 baada ya maombi lukuki ya washabiki wake Mjini Bujumbura/nchini Burundi . ......
 

WAZIRI WA MICHEZO AIFUTA KATIBA YA TFF ILIYOTUMIWA NA KINA MTIGINJOLA KUWAFYEKA KINA MALINZI, WAMBURA... AAMURU ITUMIKE KATIBA YA 200

\


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara


SERIKALI imeingilia kati sakata la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya shirikisho hilo na badala yake kuamuru itumike katiba ya zamani (mwaka 2006) baada ya kubaini kuwa iliyopo ina kasoro nyingi.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeeleza kuwa katiba ya sasa ya TFF si halali. Imeelezwa vilevile kuwa msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa. 
Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF umesimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais.
Kamati ya rufani ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo iliyozua balaa lote la sasa baada ya kuwaengua kina Malinzi na mwishowe kumuacha makamu wa sasa wa rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.
Hata hivyo, tayari mchakato wa uchaguzi huo uliozua mabishano makali umeshasimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na maafisa wa chombo hicho cha juu cha mchezo wa soka duniani wameshaanza kuwasili kufuatilia kinachotokea nchini.
Uamuzi wa serikali wa kufuta katiba ya sasa na kutaka itumike ya 2006 unampa ahueni kubwa Wambura ambaye alishasema hadharani kuwa  ataiburuza TFF mahakamani kama isipoachana na katiba mpya na kufuata ya zamani; huku akitoa sababu kadhaa za kupinga matumizi ya katiba mpya, mojawapo ikiwa ni kupitishwa kwake kwa njia ya waraka wa barua pepe (e-mail) kwenda kwa wajumbe badala ya kufuata maelekezo ya katiba yanayotaka mabadiliko kufanywa na wajumbe kupitia mkutano mkuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za FIFA, ni marufuku kwa shughuli za soka kuingiliwa na serikali au mahakama na nchi yoyote inayokwenda kinyume na taratibu hizo hujikuta ikifungiwa kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya.
(CHANZO: straikamkali.blogspot.com)

MIMBA YA SISTER P "YAPOROMOKA



MSANII wa  hiphop hapa Bongo,Happy Peter maarufu kama Sister P , ambaye aliyetamba enzi hizo na ngoma kama "Anakuja" , Amejikuta mimba yake ikiporochoka  kufuatia mazoezi makali ya kujiandaa na wimbo wake mpya.

Uongozi wa Lifeline Music waizuia Ngoma ya MwanaFA isitoke leo

                                                             TAARIFA KWA WADAU

Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.
Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.

Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama  Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.
Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.

Henry Mdimu
PR Strategist
Lifeline Music Inc

PICHA HIZI MTU SAMEHE BURE,HII KANGA MOKO HAIFAI(SHUHUDIA PICHA) SERIKALI LAZIMA IINGILIE KATI


Jamaa alizwa mbela ya mashabiki.

Mzuka ukaanza kumpanda:

ATAKAYE SEMA ALIYEMUA PADRI MUSHI ATAZAWADIWA MILLION 10



WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa kwa
kupigwa risasi Jumapili iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.

Wakati polisi wakitangaza dau hilo, Sheikh Ali Khamis Ali (65) mkazi wa Kitope Kaskazini Unguja, aliuawa jana kwa kukatwa mapanga mjini Zanzibar, baada ya wezi kuvamia shambani kwake.

RAISI KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA BABA MZAZI WA RAISI WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI

Rais Dkt. Jakaya Kikwete juu akiweka shada la maua kwenye jeneza na kutoa heshima zake za mwisho. Chini kabisa akiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta  wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. Kulia ni Mama Janet Museveni
.....................................................

Picha na habari na Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.

 Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu. 

Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake.

Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao. 

 Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo

TUME YA PINDA KUCHUNGUZA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YAPINGWA.

Dk. SLAA ADAI HOJA YA MBATIA ILIKUWA NA MAJIBU YOTE. 
 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA. 
DK SLAA.
James Mbatia, Mbunge mteule katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

SIKU moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume maalumu ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni, wanasiasa na wasomi wamempinga wakidai ni kupoteza muda na fedha kwa kuwa hoja binafsi ya Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ilikuwa na majibu.

USHAHIDI WA PICHA WABONGO WALIVYOJITOKEZA KWENYE SHOW YA ALLI KIBA NA DIMPOZ JIJINI LONDON


Picha:Umati wa Washabiki ulifika Kushuhudia Show ya Ommy Dimpoz na Alli Kiba Huko London,Show hii Ilifanyika katika club moja iitwayo OUTLET....

Pinda akutana na Balozi wa Canada.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Canada nchini, Mhe.Alexandre Leveque kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam leo Februari 25, 2013. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu).
 
 

Rais Kikwete aondoka Addis Ababa kuelekea Uganda kuhudhuria mazishi ya Baba yake Rais Museveni.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam jana, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.
 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya  Februari 24, 2013.(PICHA NA IKULU).
By Freddy Maro, Rwakitura, Western Uganda   
Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana ameungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97)  Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu.
Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake(97).
Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda.
Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.

Juliet Naivasha ajishindia Tsh 5,000,000 Kupitia DStv Rewards.


Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi aliyoishikilia.
Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili.
Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).

Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto), akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo (anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)
DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.
Akiongelea DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na hivyo amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa ili wapate nafasi ya kuibuka washindi.
Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745 622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona “kibox”.

Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!

Mshindi wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati) akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa kutupwa!
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza washindi wote.

Sunday, February 24, 2013

ADEN RAGE MWENYEKITI WA SIMBA KESHO KUACHAIA NGAZI?


Mwenyekiti wa Simba ismail Aden Rage
HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka ndani ya klabu ya soka ya Simba zinasema kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage anatarajiwa kujiuzulu nafasi yake kutokana na kipigo ilichopewa timu yake jioni ya leo na Mtibwa Sugar. 
Taarifa hizo zimedokeza kuwa, Rage atatangaza msimamo huo wa kuachia ngazi Msimbazi kesho atakapokutana na waandishi wa habari.
MICHARAZO imekuwa ikimsaka Rage mwenyewe kusikia kauli yake, lakini simu yake imekuwa haipatikani, hivyo juhudi zinaendelea ili kuthibitisha taarifa hizo na tutawajuvya mara tukibahatika kumpata.

MUIGIZAJI STEVE NYERERE ATUPWA LUPANGO



 
 Eneo la tukio la ajali hiyo.
 Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
 Kushoto ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
 Huu ndiyo waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
 Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
 Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
 Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
 Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
**********
Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.

Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.

Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 

Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.

Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.

Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
 
credits: Sufiani Mafoto

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...