Monday, February 25, 2013

Rais Kikwete aondoka Addis Ababa kuelekea Uganda kuhudhuria mazishi ya Baba yake Rais Museveni.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam jana, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.
 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya  Februari 24, 2013.(PICHA NA IKULU).
By Freddy Maro, Rwakitura, Western Uganda   
Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana ameungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97)  Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu.
Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake(97).
Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda.
Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...