Sunday, February 24, 2013

WAANDISHI WA HABARI WANUSURIKA KUTEKWA WAKITOKA KUHOJI MASWALA YA GESI MTWARA

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara, wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na  mabasi madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo kupeleleza suala la Gesi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA  Na Richard Mwaikenda, Mtwara

WAANDISHI wa Habari 150  kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.

Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.

Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.

Hongera rais Kagame : Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji jana( Feb 23,2013).



Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji  jana( Feb 23,2013): Hongera rais Kagame.

MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


 Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”

SIMBA YAPIGWA KIMOJA NA MTIBWA SUGAR


 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.
 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.
 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.
 
credits: Sufiani Mafoto

Rais Kikwete ashiriki Utiaji Saini Mpango Wa Umoja Wa Mataifa Wa Amani, Usalama na Ushirikiano Katika DRC.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt.  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma akisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Rais Joseph Kabila wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakibadilishana mawazo kwa furaha huku Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazaville) Mhe Denis Sassou Nguesso akiwa kati yao baada ya wote kweka saini  katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim na wajumbe wengine wa ujumbe wa Tanzania wakati wa uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa kuwa mmoja wa viongozi wa bara la Afrika walio mstari wa mbele kusimamia amani baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma.(PICHA NA IKULU).

Naibu Waziri wa Fedha akagua Vitega uchumi vya PSPF Jijini Dar.


SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ambalo linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba za kulala.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa  kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa  ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.
 Watumishi wa PSPF wakizungumza  jambo ndani ya Jengo hilo.
Awali Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.

Nyumba hizo zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.

Dkt. Mwakyembe azindua Bodi ya Wakurugenzi ya TRL jijini Dar.

 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) akizundua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) . Dkt. Mwakyembe amezindua Bodi hiyo leo jijini Dar es salaam ambapo ameitaka kuhakikisha inasaidia kuimarisha reli ili mizigo mingi inayokwenda ndani na nje ya nchi isafirishwe kwa njia ya reli ili kuokoa barabara. (Picha na MAELEZO-Dar)

Saturday, February 23, 2013

YANGA YAJIIMARISHA KILELENI MBELE YA WAUZA LAMBALAMBA AZAM FC, YAIPA 1-0

 Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akimtoka mchezaji wa Azam Fc, Hamis Mcha, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Niyonzima katika dakika ya 32 akiunganisha pasi nzuri kutoka kwa Jerry Tegete, ambaye kwa leo ameonekana kupwaya zaidi  na kukosa mabao kama matatu ya wazi.

Kwa ushindi huo Sasa Yanga inaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya Pointi 39, wakifuatiwa na Azam wenye Pointi 36, nafasi ya tatu inashikiliwa na Simba wakiwa na Pointi 31 nafasi ya nne ni Coast Union wenye Pointi 30, huku Yanga wakiwa na mchezo mmoja kibindoni.

Baada ya mchezo huo kumalizika wachezaji wa Azam, walimzonga mwamuzi wa mchezo huo kwa kile walichodai kuonewa sakata lililookolewa na askari wa usalam kwa kuwaondoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali huku wakipondwa na chupa za mikojo.
 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
 Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (kuli) akijaribu kumchambua kipa wa Azam Fc, Mwadin Ally, wakati wa mchezo huo, ambapo Tegete alikosa baada ya kipa huyo kuudaka mpira huo.
 WATANI WA JADI BWANA!!!!, Mashabiki wa Yanga, wakiwakebehi watani wao Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Azam Fc, kwa Bango lenye Ujumbe huu. ''Msomaji soma mwenyewe''.
 Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga, waliojitokeza kuishangilia timu yao leo, ambao wanakadiliwa kuwa kama 25,0000 hivi.
Kikosi cha Azam Fc, kilichoanza. Katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Prisons na Polisi Moro, zimetoka suluhu 0-0, Mgambo 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.

BREAKING NEWZZ : WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

wpid-Prime-Minister-Mizengo-Pinda
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.

JEURI YA FEDHA,DIAMOND PLATNUM AMJENGEA HEKARU MAMA YAKE LA MILLION 260



Karibu kila mtu anayeufuatilia muziki wa Bongo Flava anajua Diamond ndio msanii anayetafutwa zaidi kwaajili ya show kuliko msanii yeyote Tanzania but nani alifahamu kuwa amemjengea mama yake nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 260?

Lakini hivyo ndivyo alivyofanya msanii huyu kipenzi cha kinadada kwa mujibu wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM kama alivyofunguka jana.

Na kwa mujibu wa interview aliyoifanya hivi karibuni kwenye kipindi kingine cha XXL katika kituo hicho cha radio, hitmaker huyo wa Mawazo yuko booked hadi mwezi July.

“Mtu anasema yeye ananiroga mimi nashuka mwezi mzima ntakuwa na show Europe, Jumamosi nina show Hyatt pale, Jumapili nina show Mombasa wiki inayofuata ninasafiri naenda nje nina show kama kumi yaani ukinibook mimi mpaka mwezi wa saba nimejaa wewe unaniambia mimi nimeshuka vipi,” alisema Diamond.

RAIS KIKWETE AFUNGUA WARSHA KUHUSU MIKAKATI YA UTEKELEZAJI DIRA YA MAENDELEO TANZANIA 2025

8E9U2197Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza  ili kufikia Dira  ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo.
8E9U2260Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(Watatu Kushoto),Waziri Mkuu Mizengo Pinda(wane kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kulia) na,Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.Wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa Warsha Maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza ili kufanikiwa kufikia Dire ya Maendeleo Tanzania 2025 inayofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia(wapili kushoto)(picha na Freddy Maro)
8E9U2192Baadhi ya Washiriki wanaohudhuria Warsha Maalum itakayojadili mikakati ya kutekeleza  ili kufikia Dira  ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam jana. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo

MANENO OSWARD ATAMBA KUMCHAKAZA KASEBA MARCH 2

Bondia Maneno Osward akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam
Bondia Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' akifanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam
Mabondia Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba walipokutana kwa ajili ya kuzungumzia mpambano wao utakaofanyika March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo

Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini 

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

HUYU MTANZANIA AMEKAMATWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU-SONGEA

Picture
Mtuhumiwa aliye kamatwa na kiganja cha Binadamu Denes Fransis Kafinje akihojiwa na Jeshila Polisi Mkoani Ruvuma. (picha ya kiganja imefichwa nyuma ya picha hii, ikiwa una ujasiri, bofya picha kukiona)
Ni jambo la kipumbavu linaloendelea miongoni mwa wanajamii wanaoamini na kutegemea kufanikiwa na kupata faida kubwa katika biashara zao kwa kutumia viungo vya binadamu wengine.

Kwa mujibu wa Songea Habari - Yaliyojiri Mkoani Ruvuma  blog, zipo tTarifa zilizotolewa na RPC Mkoa wa Ruvuma,  Deusdedit Nsimike kuwa kijana mmoja kwa jina la Denes Fransis Kafinje mkazi wa Lizaboni amekamatwa akiwa na kiganja cha mkono wa binadamu akiwa amekihifadhi kwenye boksi.

Kwa kuwa hadi sasa  hazijaripotiwa mkoani humo tarifa za mtu kukatwa kiganja, huenda kimetoka mkoa mwingine.

mama salma kikwete aongoza hafla ya kuchangia wanawake matatizo ya afya,zaidi ya mil 142 zapatikana

Kutoka Kushoto Ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog na Ahmady Michuzi wa Jiachie Blog akifuatiwa na Henry Mdimu wakimuvuzisha matukio wakati wa hafla ya kuchangisha pesa kwaajili ya wanawake wenye mahitaji maalumu Tanzania iliyofanyika Jana Katika Hoteli ya Serena
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...