Friday, November 28, 2014
IKULU YAHUSISHWA NA ESCROW
Bunge
la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais
bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa
kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana
Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika
barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama
ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.
WANAUME 13 WASHTAKIWA KWA UDHALILISHAJI
Wanaume
kumi na watatu wameshtakiwa kwa kujihusisha na vitendo vya
udhalilishaji kwa Watoto mjini Bristol, ikiwemo vitendo vya ubakaji na
kuwalazimisha watoto wa kike kujiingiza kwenye vitendo vya biashara ya
ngono.
Mahakama ya mjini Bristol ilimsikiliza binti wa miaka 16 aliyebakwa na Wanaume watano raia wa kisomali.Halikadhalika mdogo wake mwenye umri wa miaka 14 alibakwa na mmoja wa wanaume hao, Msichana huyo alipofika kumtembelea Dada yake.
Uchunguzi uliofanywa na Polisi ulibaini kuwa genge jingine la wanaume wenye asili ya kisomali liliwadhalilisha kijinsia wasichana wengine wanne.
Wasichana hao walilipwa pauni 30,au kupewa dawa za kulevya, vilevi na zawadi kwa ajili ya kushiriki vitendo vya ngono na wanaume wenye umri mkubwa wa jamii ya kisomali.
Miongoni mwa walioshtakiwa ,Watu sita walihukumiwa kifungo,wengine saba walitiwa hatiani siku ya jumatano. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
WAFANYABIASHARA WA UGANDA WAIONYA KENYA
Wafanyibiashara
wa Uganda chini ya muungano wa Wanabiashara wa mji wa Kampala Uganda
KACITA wamelipa Shirika la ukusanyaji Ushuru nchini kenya KRA wiki mbili
kuitoa mizingo yote inayoelekea Uganda la sivyo waigomee bandari ya
Mombasa.
Ilani hiyo iliafikiwa siku ya Alhamisi baada ya saa
kadhaa za majadiliano kuhusu athari za hatua ya KRA ya kutoza kodi
bidhaa zote zinazoingia katika badari hiyo.Awali ,wafanyibiashara walikuwa wakilipa ada wanayotozwa wakati wanapochukua mizigo yao pamoja na ada nyenginezo.
Hatua hiyo kulingana na KACITA si kinyume na matarajio ya jumuiya ya Afrika mashariki pekee bali pia inawaumiza wafanyibiashara wa Uganda pamoja na uchumi.
Mwenyekiti wa KACITA Everest kayondo amesema kuwa kufikia jumatano kulikuwa na makasha 4,000 yanayozuiliwa katika Bandari ya Mombasa kutokana na ada za mara kwa mara zinazotolewa na KRA.
''Kwa hivyo tunaipa KRA wiki mbili kutoa mizigo yote ya Uganda la sivyo tuhame hadi katika bandari ya Dar es Salaam'',.aliongezea
Wafanyibiashara hao pia walikubaliana kwamba iwapo mahitaji yao hayataafikiwa ,wataishinikiza serikali ya Uganda kuzuia bidhaa za kenya zinazoingia katika soko la Uganda. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
PHILIP HUGHES AFARIKI DUNIA
Bendera
zinapepea nusu mlingoti katika viwanja vya cricket nchini Australia
katika kuomboleza kifo cha mcheza crickte Philip Hughes aliyefariki hapo
jana baada ya kupigwa na mpira. Salaam za rambi rambi zimeendelea
kutolewa kutoka sehemu mbali mbali duniani. Baadhi ya wachazaji wa
cricket wamekuwa wakiacha magongo ya mchezo huo katika mlangoni mwa
nyumba zao kama ishara ya kuomboleza kifo hicho. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Wednesday, November 26, 2014
UKAWA WASAMBARATIKA SERENGETI
Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, umesambaratika baada
ya Chadema kuamua kusimamisha wagombea vitongoji na vijiji vyote ikiwa
ni kinyume na makubaliano ya vyama hivyo.
Novemba 4, viongozi wakuu wa vyama vya Nation
League for Democracy (NLD), NCCR Mageuzi, CUF na Chadema walitiliana
saini ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja kila ngazi ya uchaguzi
kuanzia serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Kusambaratika kwa umoja
huo kulitokana na viongozi wa vyama vya CUF, NCCR Mageuzi na Chadema
kukaa vikao vitatu kupanga jinsi ya kuachiana vijiji, vitongoji na mitaa
kushindikana kufuatia viongozi wa Chadema kuvitaka vyama vingine
kuwaachia vitongoji 24 vya Mamlaka ya Mji Mdogo Mugumu. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
HALIMA MDEE AMKANA MKONO
Siku moja baada
ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu
akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka
kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.
Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi
kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa
ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.
Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema:
“Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na
mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata... awaeleze
Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.
“Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja
(The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona
si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli
watu mbona unawadanganya.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
MKOSAMALI APANDISHWA KIZIMBANI
Mbunge wa Jimbo la
Muhambwe mkoani Kigoma, Felix Mkosamali amefikishwa katika Mahakama ya
Wilaya ya Kibondo akikabiliwa na shtaka la kumzuia karani mwandikishaji
kufanya kazi yake.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai
jana mahakamani hapo kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo juzi, baada ya
kufika Kituo cha Kitongoji cha Nduta, Kijiji cha Kumhasha, Kata ya
Murungu, wilayani Kibondo na kumzuia karani kuendelea kuandikisha wakazi
kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Makala alidai kuwa kitendo cha kumzuia karani huyo
kuendelea kufanya kazi yake ni kinyume na ukiukwaji wa Sheria ya
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia, alidai kuwa kitendo cha kuwazuia wakazi hao
kujiandikisha ni kuwanyima haki yao ya msingi, kwani baada ya kuzuiwa
waliendelea kudai kutaka kujiandikisha lakini mshtakiwa hakusikiliza
kilio chao.
Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Erick Marley
alisema dhamana iko wazi kwa mdhamini kusaini bondi ya Sh4 milioni.
Mbunge huyo alitimiza masharti na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba
29.
Mkosamali alikamatwa juzi jioni baada ya kudaiwa
kumnyang’nya karani vitabu na madodoso na kuyapeleka ofisi ya Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
BOKO HARAM WAFANYA MAUAJI TENA
Watu 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati
washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo
ya akili.Wakati umati wa watu wakienda kutoa msaada, mwanamke mwingine alijitoa mhanga.
Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC anasema Wanaigeria wamekosa Imani na jaribio la serikali ya nchi yao kufanya mazungumzo na Boko Haram, kutokana an kuongezeka kwa ghasia hizo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
ZAIDI YA WATU 60 WAUAWA SYRIA
Zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa na Jeshi la serikali ya Syria.
Raia wengi waliuwawa katika mashambulio tisa yaliyolenga ngome kuu za kundi la wapiganaji wa Islamic State.Wakereketwa wameiambia BBC kuwa Hospitali kuu ya Raqqa imesalia bila huduma kwani HAKUNA chakula na umeme. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
KLABU BINGWA BARANI ULAYA
Usiku
wa kuamkia leo kindumbwe ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani
Ulaya kiliendelea na kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi
mbele ya mashabiki wa Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia
magoli 5 bila majibu.
Manchester City ya England nao wakawabamiza
wababe wengine wa Ujerumani Bayern Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2
na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku magoli
yote matatu ya Man City yakitiwa kimiani Sergio Aguero.Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1 huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1
Burudani hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Tuesday, November 25, 2014
MKONO ASIMULIA ALIVOLISHWA SUMU LONDON
Mbunge wa Musoma
Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ambaye hivi karibuni alinusurika kifo
akidaiwa kulishwa sumu akiwa London, Uingereza amesimulia jinsi tukio
hilo lilivyomkuta.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkono
alisema endapo uchunguzi wa suala hilo utakamilika na kuthibitisha
kwamba alilishwa sumu, atapambana na wahusika kwa kuwa wamehatarisha
maisha yake.
Mkono ambaye pia ni wakili maarufu nchini, alitoa
kauli hizo jijini hapa jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuelezea mwenendo wa afya yake.
Alidai kwamba, lengo la kumlisha sumu ni kuharibu figo zake ndani ya saa 72 wakati alipokuwa katika ziara ya nchini humo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
ULINZI MKALI MDAHARO WA JAJI WARIOBA LEO
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema
ulinzi utaimarishwa kabla, wakati na baada ya mdahalo maalumu wa Katiba
ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), kwenye Ukumbi wa
Mlimani City, Dar es Salaam mzungumzaji mkuu akiwa Mwenyekiti wa
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Hatua ya Kova imekuja baada ya kuibuka kwa vurugu
zilizosababisha kuvunjika mdahalo wa kwanza uliofanyika Novemba 2,
kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Dar es Salaam. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)