Sunday, November 16, 2014

MTOTO ANAYEDAIWA KUGEUKA NYOKA AZUA KIZAA ZAA

Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani ya roho yake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE AILIPUA SERIKALI KUHUSU BANDARI BUBU NCHINI

 
Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. PICHA|MAKATBA  

Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa uwepo wa bandari bubu zinazopitisha bidhaa kwa magendo kutoka nje ni miongoni mwa sababu zinazoua viwanda vya sukari hapa nchini.
Amesema kuwa viwanda vya miwa vinapokufa, wanaoumia siyo wenye viwanda bali wakulima wa miwa. Mbowe alisema hayo juzi alipohutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho mjini Turiani , Mkoa wa Morogoro katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

Ziara hiyo ni ya Operesheni Delete CCM (ODC) yenye lengo la kuvihamasisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuiondoa CCM madarakani kuanzia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PINDA AHIMIZA KUCHANGIA ELIMU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. PICHA|MAKTABA 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kwebwe aliyezungumza kwa niaba ya Pinda katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam.
“Urithi pekee kwa watoto wetu ni elimu, unaweza kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi pekee…: Watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo tunafanya katika sherehe,” alisema Kebwe akiongeza:
“Utamkuta mtu anachangia fedha nyingi katika harusi na kama tunavyojua harusi moja, ukianza na ‘send off’, ‘kitchen part’ na harusi yenyewe ni fedha nyingi, lakini mtu huyo huyo ukimwambia achangie masuala ya elimu, hutamwona.”
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence-Makoka wamiliki wa shule hiyo, Padre Evarist Tarimo, alisema kuwa malengo ya sherehe hiyo ni kuchangisha Sh250 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana ili kuondoa adha wanayoipata kwa sasa.
“Hivi sasa vyumba vya madarasa tunavitumia kama mabweni, hivyo wanasomea humo na kulala humo humo, jambo ambalo kitaaluma si zuri. Tunatarajia tutakapomaliza ujenzi huo tutawawezesha wanafunzi wetu kusoma na kulala katika mazingira mazuri na nina hakika juhudi za wadau zitaweza kukamilisha ujenzi huu,” alisema. Habari tulizozipata baadaye zilisema jumla ya Sh41.2 milioni zilikusanywa. Fedha taslimu ni Sh13.3 milioni. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 16, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
. 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, November 15, 2014

BUTIKU AMKINGIA KIFUA WARIOBA

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere , Joseph Butiku 

Taasisi ya Mwalimu Nyerere imesema kuwa wanaotaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akae kimya kuhusu Katiba Inayopendekezwa hawana hoja.
Imesema kuwa wanaosema hivyo hasa wale wa chama tawala (CCM) wanatakiwa kujiuliza kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita wamefanya nini kuhusu Katiba, ikisisitiza kuwa itaendelea kufanya midahalo ya kuwaelimisha Watanzania kuhusu mchakato wa Katiba ili utakapofika wakati wa kura ya maoni waelewe kipi wanatakiwa kukifanya kwa mustakabali wa taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema hayo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu kazi na majukumu ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere tangu ilipoanzishwa hadi sasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

G20 YAMUONYA PUTIN AONDOKE UKRAINE

Viongozi wa mataiifa ya magharibi wanaohudhuria mkutano wa mataifa tajiri, G-20 mjini Brisbane, Australia, wameionya Urusi ifuate makubaliano ya kusitisha mapigano Ukraine, ama sivyo itakabili vikwazo zaidi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alimwambia Rais Putin kuwa uhusiano baina ya Ulaya na Urusi utabadilika iwapo wanajeshi wa Urusi watabaki Ukraine.
Rais Obama alisema hatua za Urusi zinachusha.
Urusi inakanusha kuwa ina wanajeshi wake ndani ya Ukraine.
Msemaji wa Bwana Putin alitoa maanani ripoti kuwa kiongozi wa Urusi anapanga kuondoka mapema kwenye mkutano. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

EBOLA YAISHA DRC, YAONGEZEKA S-LEONE

Jamhuri ya Demokrasi ya Congo imejitangaza kuwa haina tena virusi vya ebola baada ya virusi kuambukiza watu kwa miezi mitatu na kuuwa wagonjwa karibu 50.
Virusi vya Ebola vilivyoathiri Congo ni tofauti na vile vya Afrika Magharibi.
Lakini Waziri wa Afya, Felix Kabange Numbi, amewasihi watu bado kuwa macho - kwamba kumalizika kwa ugonjwa, haimaanishi kuwa nchi haiko kabisa hatarini.
Na Daktari wa Sierra Leone ambaye ameambukizwa Ebola amepelekwa Marekani kwa matibabu.
Martin Salia, ambaye ana kibali cha makaazi Marekani na ambaye ameoa Mmarekani, atatibiwa wakati ametengwa kwenye kitengo maalumu katika jimbo la Nebraska.
Haijulikani iwapo Dr Salia, daktari wa upasuaji, aliuguza wagonjwa wa Ebola Sierra Leone.
Hospitali alikofanya kazi haina kituo cha kuuguza wagonjwa kama hao.
Dakta Salia atakuwa mgonjwa wa 10 wa Ebola kuuguzwa Marekani.
Hadi sasa watu zaidi ya 5,000 wamekufa kutokana na Ebola Afrika Magharibi.
Juma hili iliripotiwa kwamba wakati idadi ya maambukizi ya Ebola yanapungua Liberia na Guinea, bado yanaongezeka nchini Sierra Leone.
Na katika tukio jengine, Ufaransa imewashauri raia wake wasiende katika sehemu fulani za Mali baada ya watu watatu kufariki huko kwa sababu ya Ebola.
Raia wa Ufaransa walioko Mali wameambiwa wafuate ushauri wa serikali ya Mali. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 15, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

GUINEA IKWETA KUANDAA AFCON 2015


Guinea ya Ikweta inaandaa michuano ya AFCON mwakani

Shirikisho la soka la Afrika CAF limeichagua na kuipatia nafasi Guinea ya Ikweta kuandaa fainali za kombe la Afrika 2015 kuchukua nafasi ya Moroko iliyojitoa wiki iliyopita. Awali Rais wa CAF Issa Hayatou alikuwa na majadiliano yenye manufaa na Rais wa nchi hiyo tajiri ya mafuta Teodoro Obiang Nguema mjini Malabo kabla ya kufikia hatua ya kuikabidhi nchi yake dhamana hiyo.
Taarifa ya CAF imethibitisha leo ijumaa kuwa Guinea ya Ikweta mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika imepewa jukumu hilo kubwa la kuokoa jahazi la michuano hiyo na itashiriki fainali hizo kama ilivyo kawaida ya mwenyeji. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, November 14, 2014

MCHUNGAJI AFARIKI AKIJARUBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU


 
Mchungaji kutoka Nigeria, Frank Kabele akizama alipojaribu kutembea juu ya maji kama Yesu.
 
...Akiomba msaada kutoka kwa waumini wake bila mafanikio.
Mchungaji kutoka Nigeria, Frank Kabele (35) amesombwa na maji katika mto mmoja nchini hiyo na kufariki alipojaribu kutembea juu ya maji kama Yesu.
Frank Kabele aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani.
Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.
Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya mchungaji huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi na kufariki dunia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TAZAMA TASWIRA ZA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA JANA


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa siku ya jana.
Msafara wa magari kuelekea makaburini.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MOTO WAZUKA JENGO LA MACHINGA COMPLEX LEO

 
Moto waibuka jengo la Machinga Complex jijini Dar wazimwa kabla haujaleta madhara makubwa. 
 


Moshi ukiwa umetanda angani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE AMTAKA KIKWETE AVUNJE BARAZA LA MAWAZIRI


Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Picha na Maktaba 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri na kuunda jipya kutokana na tuhuma za ufisadi.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari baada ya mikutano yake katika mikoa ya Magharibi alisema ni lazima hatua hiyo kuchukuliwa ili kukabiliana na mafisadi ambao hakuwataja, vinginevyo alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni anayoiongoza, itaanza maandalizi ya kuwasilisha bungeni, hoja ya kutokuwa na imani naye.

Alisema Serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua za ufisadi ambazo zinawakabili watendaji wake: “Kambi ya Upinzani Bungeni inamtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mawaziri wake na kuunda Serikali mpya.” Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UTAFITI WA TWAWEZA WATIKISA NCHI

Mkurugenzi Mstaafu waTaasisi ya Utafiti ya Twaweza, Rakesh Rajan (kulia) akiwaelezea jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu (kushoto) na Mkurugenzi wa Compass Communication Limited, Maria Sarungi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kabla ya taasisi hiyo kutangaza matoke ya utafiti wao kuhusu Tanzania Kuelekea 2015, jijini Dar es Salaam juzi.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza kuhusu maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa nchini, umeibua madai mapya ambayo yanauhusisha na jitihada za kukisaidia chama tawala CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Dar es Salaam juzi, inaonyesha kuwa kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika sasa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angeshinda urais kwa asilimia 13, akifuatiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa asilimia 12, huku Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa akiibuka na asilimia kumi na moja.
Mbali na wanasiasa hao, wengine waliotajwa katika ripoti hiyo na asilimia zao kwenye mabano ni Profesa Ibrahim Lipumba (6%), Dk John Magufuli (3%), Freeman Mbowe (3%), Samuel Sitta (4%), Bernard Membe (5%) na Zitto Kabwe (1%). Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE ATOKA WODINI, FAMILIA YA NYERERE YATUMA SALAMU

Rais Jakaya Kikwete akiagana na daktari bingwa, Edward Schaeffer baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore nchini Marekani, alikofanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Rais Jakaya Kikwete ametoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...