Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania
kutokurupuka kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando
maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au
kuikataa.
Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake
Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia
Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu
masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya
Harrieth, Jaji Warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje Katiba
Inayopendekezwa na iwapo CCM imemgeuka kwa nini asihame chama?
Akijibu maswali hayo, Jaji Warioba alisema Katiba
hiyo haina maoni yote ya wananchi kama Bunge Maalumu lilivyojinadi, bali
yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika Katiba ya sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz