Kikosi Kazi cha
Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10,
msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa
aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana
na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza
kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika
Kusini.
Nzowa alisema baada ya kuhojiwa, Masogange aliruhusiwa na kwamba yupo huru, ameachiwa bila masharti yoyote.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi
Selemani naye alithibitisha kuhojiwa kwa msanii huyo akisema: “Hapa kuna
kikosi kazi, kila mmoja alimhoji kwa wakati wake lakini kwa upande wa
polisi tulimpekua na kumhoji lakini tumemwachia.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz