Friday, July 10, 2015

KIKWETE: "NILIACHA KUANGALIA MPIRA ILI NISIONEKANE NINA MKOSI"


Raisi Kikwete akipeana mkono wa mchezaji wa zamani wa Real Madrid walipoitembelea Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliacha kwenda uwanjani kuiangalia timu ya taifa Stars kwa kuwa alionekana kuitia mkosi wa kufungwa timu hiyo kila ilipocheza.

Akiongea wakati wa kuvunja bunge na kuwaaga wabunge, Rais Kikwete alisema zamani alihudhuria sana mechi za Stars na baada ya kuonaa inafungwa mara kwa mara, aliamua kuacha kwenda uwanjani .

“Mwanzoni nilikuwa navaa hadi jezi kuishangilia timu yetu ilipokuwa inafanya vizuri, tulipoanza kufungwa fungwa wakasema mzee unaitia timu mkosi, nikaamua kuacha”, alisema Rais Kikwete huku akicheka katika hali ya mzaha.

Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

“Lakini hata baada ya kutokwenda uwanjani, timu imeendelea kufungwa tu, tusikate tamaa”, alisema Rais Kikwete mpenda michezo. Taifa Stars imetolewa michuano ya kufuzu ya CHAN na Uganda na sasa ina kibarua cha kufuzu fainali za AFCON mwaka 2017.

Hata hivyo, Rais Kikwete amewataka Watanzania kutokata tamaa na kufanya vibaya kwa sekta ya michezo na badala yake jitihada za kuendeleza sekta hiyo ziendelee na ipo siku sekta hiyo itafanya vizuri kimataifa.

Amesema serikali yake imefufua michezo ya mashuleni ili kukuza vipaji kwa ajili ya taifa hapo baadae na pia serikali yake imeingia ubia na makampuni ya kimataifa yay a Symbion Power na klabu ya Sunderland ya Uingerteza kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambacho kinategemewa kuanza kazi mwezi Septemba.

“Tujitahidi, tusikate tama, tutafika tunapopakusudia”, alisema Rais Kikwete katika hotuba hiyo ambayo aliitumia kulianga bunge akijiandaa kuachia madaraka mwezi Oktoba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Rais na wabunge.

Rais Kikwete amesema serikali yake pia imechukua jitihada za makusudi kuendeleza sekta ta muziki na filamu kwa kuwaalika wataalamu kutoka Marekani kutoa mafunzo ya sekta hizo kwa wasanii wa Tanzania ili wafanye kazi nzuri itakayotambulika kimataifa.

Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...