Wednesday, May 28, 2014

AL-SHABAAB WAKIRI KUSHAMBULIA DJIBOUTI

Hali ilivyokuwa baada ya kushambuliwa kwa Bunge nchini Somalia
Al Shabaab wamesema katika taarifa kuwa kwa kushambulia mgahawa huo, walikuwa wakiwalenga raia wa mataifa ya Magharibi wanaopendelea kuutembelea Djibouti.
Kundi hilo liliwalaumu Wafaransa - walio na kambi kubwa ya wanajeshi nchini Djibouti - kwa kuwadhulumu Waislamu katika Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR) na kwa kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Djibouti walio katika kikosi maalumu cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika, AMISON, nchini Somalia.
Al Shabaab pia walilaumu Djibouti - ambayo ni mwenyeji wa vituo kadhaa vya kijeshi vya mataifa ya Magharibi, kukiwemo Marekani - kwa kuruhusu mataifa ya Magharibi kutumia taifa lao kama sehemu ya kushambulia Waislamu.
Al Shabaab wamepunguzwa makali nchini Somalia tangu kuanzishwa kwa msukumo wa kijeshi wa kukabiliana nao wa Serikali ya Somalia na wanajeshi wa AMISOM.
Hata hivyo kundi hilo halijaishiwa na uwezo wa kushambulia. Mnamo Jumanne wanajeshi kadhaa wa Ethiopia waliuawa baada ya kuvamiwa na Al Shabaab katika eneo la Bakol.
Na Jumamosi, walishambulia Bunge katika mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa kuwa kundi hilo tayari linaweza kushambulia nchini Kenya na sasa limechipukia Djibouti, ni ishara kamili kuwa limeanza kuwa tatizo katika eneo zima, mbali na kushambulia taasisi mbalimbali nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Tuesday, May 27, 2014

BAJETI YA MWAKYEMBE YATIKISA BUNGE, YAPITA...!!!

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/15 bungeni Dodoma, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi      

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana usiku alikuwa katika wakati mgumu wakati Bunge lilipoketi kama Kamati ya Matumizi, kiasi cha kutishia bajeti ya wizara yake kukwama. Hata hivyo, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 yalipitishwa.
Wabunge wa vyama vyote walimbana Dk Mwakyembe na kutoa shilingi karibu katika kila kifungu wakihoji mambo mbalimbali hasa juu ya mgogoro wa umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), usafiri wa majini hususan usalama wa meli ya Mv Victoria.
Sakata la Uda
Sakata hilo la Uda lilisababisha mvutano baina ya Naibu Spika, Job Ndugai na Dk Mwakyembe ambaye alilalamikia mjadala wa Uda kuruhusiwa katika hotuba ya wizara yake. Hata hivyo, Ndugai alipangua hoja hiyo akisema mbali na kwamba Uda inagusa wizara nyingi, lakini ni suala linalohusu uchukuzi hivyo ilikuwa sahihi kujadiliwa katika mjadala huo.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla ndiye aliyeibua suala hilo kwa kuhoji sababu ya Serikali kutoa taarifa zinazokanganya kuhusu Uda, hali kamati anayoiongoza ilishakaa na pande zote husika wakiwamo wataalamu na kuwa na hitimisho kwamba Kampuni ya Simon Group Ltd ni waendeshaji halali wa shirika hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

'OCEAN ROAD WAMENISUSA, NAHAMIA TIBA ZA JADI'


Majengo ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba.

Mgonjwa wa saratani ya titi aliyepewa dawa feki za mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) amejikuta katika wakati mgumu baada ya wahudumu wa hospitali hiyo ya Serikali kumtelekeza alipokwenda kupata tiba.

Mgonjwa huyo, Pendo Shoo ambaye anahofu kwamba saratani imempata katika titi lake la pili, anasema hatakwenda tena katika hospitali hiyo na badala yake ameamua kusaka tiba kwa waganga wa tiba asilia.

Hivi karibuni gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mtumishi wa OCRI, Almasi Matola alivyomtibu Pendo kwa dawa feki baada ya kumtoza kiasi cha Sh1.34 milioni kinyume na taratibu za tiba katika hospitali hiyo.

Almasi akizungumza na gazeti hili wiki mbili zilizopita, alikiri kuwekewa fedha katika akaunti yake ambazo ni zaidi ya Sh300,000, lakini akakanusha kwamba fedha hizo ni kama ujira wa kumpa mgonjwa huyo dawa.

Kwa mujibu wa taratibu za OCRI, wagonjwa wanaokwenda hospitali hapo kwa rufaa kutoka hospitali nyingine hawapaswi kutozwa fedha zozote kwa ajili ya matibabu. Pendo alipata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba mwaka jana.

Alibaini kuwa alipewa dawa feki baada ya kutokupata nafuu yoyote wiki kadhaa tangu alipoanza kupewa tiba na baada ya kuripoti tukio hilo kwa madaktari walimwanzishia upya tiba husika. Wiki moja tu baada ya kuchapishwa habari hizo, mgonjwa huyo alifika OCRI kuendelea na matibabu lakini alijikuta katika mazingira magumu kiasi cha kuondoka bila kupewa huduma. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NI TIMU NANE TU ZIMETWAA KOMBE LA DUNIA

Vijana wa Brazil  

London, England. Kwa kipindin cha miaka 83, fainali za Kombe la Dunia zimefanyika mara 19, lakini hadi sasa ni timu nane tu ambazo zimeshatwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.
Fainali hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1930 nchini Uruguay na zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka minne, isipokuwa mwaka 1942 na 1946 kutokana na Vita Kuu ya dunia .
Brazil inaongoza kwa kutwaa Kombe la Dunia baada ya kutwaa taji hilo mara tano. Brazil ilitwaa taji hilo nchini Sweden mwaka 1958, nchini Chile (1962), Mexico (1970), Marekani (1994) na Korea/Japan (2002). Brazil pia ndiyo nchi pekee iliyoshiriki fainali zote za Kombe la Dunia tangu zilipoanzishwa mwaka 1930 na imefunga jumla ya 210 katika fainali 19.
Italia imetwaa ubingwa huo mara nne. Ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ilipoandaa mwaka 1934, baadaye nchini Ufaransa (1938), Hispania (1982) na Ujerumani (2006). Italia imeshiriki fainali hizo mara 17 na kufunga mabao 126. Kati ya 1950 na 1990, Ujerumani Magharibi (sasa Ujerumani) ilitwaa ubingwa mara tatu. Ilitwaa ubingwa nchini Uswisi 1954, na baadaye ilipoandaa fainali hizo mwaka 1974 na nchini Italia (1990). Kati ya 1930 mpaka 2010 Ujerumani imeshiriki fainali hizo mara 17 na imefunga mabao 206.
Mwaka 1978, Argentina ilikuwa ni taifa la tano kutwaa ubingwa wa dunia. Ilitwaa tena ubingwa wa dunia mwaka 1986. Tangu 1930 mpaka 2010, Argentina imeshiriki fainali hizo mara 15 na kufunga mabao 123.
Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kutwaa kombe hilo wakati ilipoandaa fainali hizo 1930. ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pilimwaka 1950 nchini Brazil. Uruguay imeshiriki Fainali za Kombe la Dunia mara 13 na kufunga mabao 76. Ufaransa imetwaa ubingwa wa dunia mara moja mwaka 1998 walipokuwa wenyeji. Ufaransa imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 13.
Pamoja na utajiri wa vipaji na kuwa na klabu bora, Hispania ilisubiri hadi mwaka 2010 kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza na ndio mabingwa watetezi. Hispania imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 88.England iliandaa na kutwaa ubingwa mwaka 1966. Imeshiriki mara 13 na kufunga mabao 77. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 27, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

JESHI NIGERIA 'TUNAJUA WALIPO WASICHANA'

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linajua wanakozuiliwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara majuma sita yaliyopita lakini likasema haliwezi kutumia nguvu kuwakomboa.
Afisa wa cheo cha juu jeshini - Mkuu wa Jeshi Alex Badeh - aliwambia waandamanaji jijini Abuja kuwa hangeweza kufichua waliko wasichana hao lakini akaahidi kuwa wanajeshi watawarejesha nyumbani wasichana hao.
"Habari nzuri kwa wasichana ni kuwa tunafahamu waliko lakini hatuwezi kuwambia. Hatuwezi kuja na kuwambia siri za kijeshi hapa," mkuu wa wanahewa Alex Badeh aliwambia waandamanaji jijini Abuja.
Alisema anaamini kuwa watawarudisha wasichana hao nyumbani hivi karibuni lakini akaeleza masikitiko yake kwa kile alichosema watu kutoka nje ya nchi wanaochochea ghasia na maandamano.
Bwana Badeh alisisitiza kuw kutumia nguvu kujaribu kuwakomboa wasichana hao ni hatari.
"Wapiganaji hawa wanataka kupigana na kwa hivyo wasichana watakuwa hatarini ikiwa kutatokea mkabiliano makali kati ya wapiganaji hao na jeshi la Nigeria," Alex Badeh alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

MISRI WAMCHAGUA RAIS MPYA

Mabango yanayotangaza uwaniaji wa aliyekuwa Mkuu wa jeshi la Misri, Abdel Fatah al-Sisi, kama Rais
Raia wa Misri wanapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama.
Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .
Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.
Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo: BBC

Saturday, May 24, 2014

MBUNGE NA BIBI HARUSI MTARAJIWA VICY KAMATA AUGUA GHAFLA SAA 36 KABLA YA HARUSI...!!!

Mbunge Vicky Kamata akiwa amelazwa Hospitali ya Tabata General, Dar es Salaam jana. Picha na Florence Majani 

Dodoma/Dar es Salaam. Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni.
Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.
Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

LIGI YA MABINGWA: SAMATA, ULIMWENGU KUIONGOZA TP MAZEMBE DHIDI YA MAHASIMU WAO AS VITA MJINI LUBUMBASHI


1
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samata na Thomas Emmanuel Ulimwengu kesho jumapili wanatarajia kuiongoza TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao wakubwa, AS Vita mjini Lubumbashi.
Timu hizi hasimu zitakutana katika mchezo wa kesho zikiwa na kumbukumbu ya kusababisha maafa ya vifo vya watu zaidi ya 15 katika mchezo wao wa ligi kuu ya DR Congo wiki za karibuni.
Tukio hilo baya lilitokea mjini Kinshasa baada ya mashabiki wa AS Vita kutoridhishwa na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzania wao TP Mazembe.
Mchezo wa kesho umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka, kwani timu hizi zinapokutana, upinzani unakuwabmkubwa mno nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
TP Mazembe wataingia katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupigwa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi A na Al Hilal ya Sudan mnao mei 17 mwaka huu.
Mei 18 mwaka huu, AS Vita walitumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuilaza Zamalek ya Misri mabao 2-1, hivyo wataingia katika mchezo huo wa kundi A wakiwa na morali kubwa ya kusaka ushindi wa pili.
Mechi nyingine ya kesho jumapili itakuwa ya Kundi B kati ya wenyeji ES Setif ya Algeria dhidi ya SC Sfaxine ya Tunia.
Mei 18 mwaka huu SC Sfaxine waliifumua Al Ahly Benghazi ya Libya mabao 3-1, wakati mei 17, 2014, ES Setif waliifunga mabao 2-1 Esperance ya Tunisia.
Mbali na mechi hizo za kesho, leo hii mitanange mingine inaendelea ambapo kundi A, wenyeji Zamalek watawakaribisha Al Hilal kutoka nchini Sudan.
Huu utakuwa mchezo muhimu kwa Mafarao waliopoteza mechi iliyopita. Al Hilal wao watakuwa wanahitaji ushindi wa pili katika michuano hiyo.
Mechi ya kundi B leo hii, wenyeji Al Ahly Benghazi ya Libya waliopoteza mechi ya kwanza kwa mabao 3-1 watakabiliana na miamba ya soka la Tunisia, Esperance ambao nao mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

CECAFA NILE BASIN CUP, MBEYA CITY FC KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA LEO

IMG_1150 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan , Mbeya City fc wanaanza kutupa karata yao ya kwanza leo hii majira ya 11:30 jioni kwa saa za Sudan dhidi ya Academie Tchite ya Burundi. Kuelekea katika mechi hii itakayopigwa uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum, ushinidi ni muhimu kwa Mbeya City fc ili kupata morali ya mashindano haya yaliyoanza jana kwa mechi tatu kupigwa viwanja viwili tofauti. Kocha Juma Mwabusi ameuambia mtandao huu kwa njia ya simu kutoka nchini Sudan kuwa kikosi chake kipo salama na kipo tayari kwa ajili ya mechi ya leo jioni. “Tumewasili salama mjini Khartoum. Tulichelewa kufika huku ili angalau kuzoa hali ya hewa. Lakini haimaanishi hatuwezi kushindana. Sisi tumejiandaa vizuri na tulikaa Dar kwenye joto ingawa hailingani na Sudan”. “Mashabiki wetu wawe na imani na timu yao. Tunaiwakilisha nchi na tutapambana kwa nguvu zote. Wachezaji wana morali ya kufanya vizuri”. Alisema Mwambusi. Mbali na mchezo huo wa jioni, mechi nyingine ya usiku itakuwa baina ya AFC Leopard ya Kenya dhidi ya Enticelles ya Rwanda. Katika mechi zilizopigwa jana, kwa mujibu wa msemaji wa CECAFA Rodgers Mulindwa, Victoria University ya Kenya iliilaza Malakia FC ya Sudan kusini bao 1-0. Wenyeji Al-Merreikh waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi ya visiwani Zanzibar. Nao Al-Shandi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dkhill ya Djibouti. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

CCM: "HATUWEZI KUWAVUMILIA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOKWAMISHA UTEKELEZWAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI"

Katibu wa CCM wilaya ya kilolo Bw. Raphel Mahumba mwenye pama, akimuagiza Diwani wa kata ya ukumbi afuatilie nani anaye kwamisha ujenzi wa zahanati ya kitowo na hatua zichukuliwe haraka, aliye vaa skafu ni katibu mwenezi wa chama.
Wananchi waliongozana na katibu wa CCm wilaya ya Kilolo kuangalia ujenzi wa zahanati ya Kotowo ambayo imesimama bila sababu za msingi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ZIJUE KANUNI ZA SAYANSI ZA KUSAIDIA MTU KUISHI MAISHA MAREFU


Nyama nyekundu inaelezwa kuwa ni moja ya vyakula vinavyopunguza urefu wa maisha. 

Na Clifford Majani, Mwananchi


Kwa miaka mingi sana binadamu wa karne zote wamekuwa wakitafuta siri za maisha marefu, kuzuia uzee na hata kuzuia kifo. Lakini pamoja na jitihada nyingi mambo haya yameendelea kuwa changamoto kubwa kwenye maisha ya mwanadamu katika nchi mbalimbali duniani.  Kwa Tanzania, inakadiriwa kuwa umri wa kuishi kwa wanaume ni takriban miaka 58.2 na kwa wanawake ni miaka 60.5.
Muda huu wa kuishi ni mfupi sana ikilinganishwa na wenzetu katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako wastani wa kuishi ni unakadiriwa kuwa ni miaka 78.2. Wanasayansi wamekuwa na nadharia nyingi kuhusu sababu zinazosababisha binadamu azeeke na kufa mapema. Ila wengi hufikiri kuwa tunazeeka mapema kutokana na sababu za maumbile na vinasaba tunavyorithi kwa wazazi wetu.
Wengine husema kuwa tunazeeka haraka kutokana na kuwa na mtindo usiofaa wa maisha. Mtaalamu wa Afya, Dk Mark Stibich  anasema kwamba kuzeeka haraka na kuishi maishi mafupi ni suala mtambuka na linahusisha mambo kama vile vinasaba, kemia, fiziolojia ya mwili pamoja na tabia zetu kwa mujibu wa makala yake ya Mei 10, 2014 liyowekwa kwenye tovuti ya longevity.about.com.
Mtaalamu wa maabara nchini Ujerumani, Dk James Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya kuzeeka haraka hutokana na mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 24, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ALIYEZAA MTOTO WA AJABU HANDENI ALONGA


Mwajuma Seif (50). PICHA|MAKTABA 



Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya upandikizaji. Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.

Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia ya upandikizaji. Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13. Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa .

Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi. Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound (kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

UN: VATICAN INAPUUZA HAKI ZA WATOTO

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la unyanyasaji wa ngono ndani ya kanisa hilo.
Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatican kwa kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .
Utawala wa Vatican uliithinisha mkataba dhidi ya unyanyasaji , ukatili na matendo yaliyo kinyume na utu.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Vatcan ni sehemu ya uchunguzi wa mara kwa mara wa kamati hiyo dhidi ya nchi wanachama ili kuhakikisha mikataba inatekelezwa. Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatcan umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayaendani na vitendo.
Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.
Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatican ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo: BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...