Sunday, May 18, 2014

ARSENA BINGWA KOMBE LA FA

BAO la dakika ya 109 la Aaron Ramsey limeipa Arsenal ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuichapa Hull City 3-2 ikitoka nyuma kwa 2-0 Uwanja wa Wembley.
Ramsey alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Olivier Giroud na kuondoa uwezekano wa mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Arsenal waliuanza kichovu mchezo huo na kujikuta wanafungwa mabao mawili ndani ya dakika nane, Chester akianza kufunga la kwanza dakika ya nne na Davies akafunga la pili dakika ya nane.
article-2630209-1DF2D11300000578-658_964x520
Santi Cazorla aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 17 kwa shuti la mpira wa adhabu kabla ya Koscielny kufunga la pili dakika ya 72 na Ramsey la ushindi dakika ya 108.
Ushindi huo ni furaha kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hajatawaa taji lolote kwa miaka tisa.
Mara ya mwisho Arsenal walitwaa taji mwaka 2005, ambalo lilikuwa Kombe hilo hilo la FA wakiendeleza mafanikio ya msimu wa 2003-2004 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Ramsey, Cazorla/Wilshere dk105, Ozil/Rosicky dk105, Podolski/Sanogo dk61 na Giroud.
Hull: McGregor, Chester, Bruce/McShane dk67, Davies, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Meyler, Rosenior/Boyd dk103, Quinn/Aluko dk74 na Fryatt.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ATLETICO MABINGWA WA LA LIGA

atletico_187be.jpg
Atletico Madrid imenyakua kombe la ligi kuu ya Hispania La liga baada ya kutoka sare ya 1 – 1 dhidi ya Barcelona na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 90 huku Barcelona ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 87.
Real Madrid iliyoshinda mechi yake dhidi ya Espanyol kwa 3 - 1 ikishika nafasi ya tatu kwa kumaliza ligi ikiwa na pointi 87 lakini ikizidiwa na Barcelona kwa tofauti ya goli moja.
Barcelona wana tofauti ya magoli 67 wakati Real Madrid ikiwa na tofauti ya magoli 66.
Katika mechi hiyo ya Barcelona dhidi Atletico Madrid ambayo ilikuwa ni ya kuamua ni timu ipi itanyakua ubigwa wa La Liga msimu huu, Barcelona ndio waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Atletico Madrid kwa goli lililofungwa na Alexis Sanchez katika ya 34 kipindi cha kwanza.
Baadae Atletico Madrid walikuja juu na kuanza kulishambulia goli la Barcelona ambapo Diego Godin katika dakika ya 49 kipindi cha pili aliIsawazishia timu yake kwa goli safi alilolipachikwa wavuni kwa njia ya kichwa na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike kwa jumla ya goli 1 - 1 .
Atletico Madrid inakuwa mabingwa wa La Liga tangu baada ya kulikosa kombe hilo tangu mwaka 1996. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Saturday, May 17, 2014

MSANII NA MUONGOZAJI WA FILAMU 'ADAM KUAMBIANA' AMEFARIKI DUNIA GHAFLA ASUBUHI YA LEO...!!!

Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukitolewa nje ya Hospitali  ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana huu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HOMA YA DENGUE, MABASI 600 KUPULIZIWA DAWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kuhakikisha mabasi yote 600 yanayofanya safari zake mikoani yanapulizia dawa ya kuondoa mazalia ya mbu wanaoeneza ugonjwa wa dengue.

Manispaa za Dar es Salaam zimetengewa Sh. milioni 218 kwa ajili ya kununua dawa na vifaa vya kupulizia mazalia ya mbu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki alisema kuwa tayari serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa ili usienee kwa wengine. Alisema mabasi yatakayokaidi agizo hilo yatafungiwa safari zake lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha ugonjwa huo hausambai katika mikoa mingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki alisema kuwa tayari serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa ili usienee kwa wengine.

Alisema mabasi yote yanatakiwa kuhakikisha yanapulizia dawa ili yanapoanza safari zake ili yasiondoke na mbu hao katika mikoa mengine. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

FILAMU YA JOTI SANDUKU LA BABU KUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI

Msanii Lucas Mhavile 'Joti'baada ya kukaa kimya kwa mda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika husika tofauti tofauti.
Filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na Kampuni yaproin promotions ya jinini Dar es salaam akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingini kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo haijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasinia hii ya filamu nchini hivyo wapenzi wangu wakae mkao wa kula tu kwani wakati wowote kuanzia sasa itakuwa inaingia sokoni kwani filamu hii si yakukosa mana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala alisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka' filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia luninga sasa ameludi tena katika filamu yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la Joti sanduku la babu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

PROFESA LIPUMBA AWASHANGAA VIJANA WA IRINGA

Baadhi ya vijana waliohudhuria mkutano huo

Lipumba wa CUF akisisitiza jambo

Mchungaji Msigwa wa Chadema
Danda Juju wa NCCR-Mageuzi
 Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ASKOFU DALLU KUSIMIKWA RASMI KESHO


dalu_1b119.jpg
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla, anataraji kuongoza Misa Takatifu ya kusimikwa kwake Askofu Mpya wa Jimbo Kuu la Songea, Mhashamu Damian Dennis Dallu (Pichani).

Tukio hilo litafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba la Jimbo Kuu la Songea hapo kesho. Leo hii baadhi ya waumini wamesafiri mpaka katika mpaka wa Mkoa wa Ruvuma na Njombe kwa ajili ya kumpokea Askofu Dallu anayeingia Jimboni Songea na leo Jumamosi atafanyiwa Ibada ya kukabidhiwa Kanisa.

Tukio hilo linalotaraji kuhudhuriwa na Viongozi wengi wa Madhehebu ya dini, litahudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. (PERAMIHO PUBLICATIONS)
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATU 10 WAUAWA KATIKA MILIPUKO NAIROBI

Haijulikani na nani aliyesababisha milipuko ingawa washukiwa tayari wamekamatwa
Milipuko miwili ilitikisa Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi na kuwaua watu 10 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa..
Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa.
Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea ndani ya soko.
Soko la Gikomba ni maarufu kwa nguo za mitumba
Milipuko hiyo ilitokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wawu wenye uhusiano na kundi la wanamgambo la kiisilamu nchini Somalia la Al Shabaab. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC Swahili

USALAMA WA NIGERIA KUANGAZIWA UFARANSA

Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anaanda mkutano hii leo mjini Paris kuangazia hali ya usalama nchini Nigeria.
Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi kutoka nchi za Nigeria,Benin,Cameroon,Chad na Niger ili kutafuta njia za kukabiliana na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko haram.

Wawakilishi wa Marekani muungano wa Ulaya na Uingereza wataangazia kazi iliofanywa na wataalam wa Uingereza, Ufaransa na Marekani waliotumwa nchini humo ili kuisaidia mamlaka ya Nigeria kuwanusuru zaidi ya wasichana 200 waliotekwanyara na kundi hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo: BBC Swahili

Friday, May 16, 2014

BIRTHDAY YA RAY, JOHARI AMPA SALAMU TATA..... ISOME HAPA....!!!

http://jambotz8.blogspot.com/
Leo ni birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa
Leo mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray anasherehehea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa wenzie. Moja ya watu wa kwanza kwanza kumpa salamu hiyo ni swahiba na rafiki yake mkubwa, JB akifuatiwa Johari ambaye salamu yake inadaiwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni kwa namna flani inamponda mpenzi wa sasa wa Ray, Chuchu Hans, kutokana na maneno yaliyotumika ya salamu hiyo ambayo Johari anadaiwa kuwahi kuyatumia kumponda Chuchu siku za nyuma.

JB ameandika
''Happy birth day mdogo wangu Ray. Mungu akupe haja ya moyo wako.''

Na huku Johari akiandika 
''Happy birthday director wa RJ na swaiba wangu Mungu akuongoze akupe maisha marefu na akuepushe na ‘’mabarazuri’’
Jambo Tz inakupongeza sana Ray kwa kutimiza miaka kadhaa siku ya leo na  Mungu akupe maisha marefu zaidi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WASSIRA AWATISHA UKAWA


Stephen Wassira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ATOA KAULI YA KUWABAGUA WANZANZIBAR BUNGENI...!!!

weremapx_89c87.jpg
Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema 'amelikoroga na kulinywa mwenyewe', baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.

Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15. Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.

Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo. "Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu," alisema Werema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATALII TOKA UINGEREZA WATOROKA MOMBASA


Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya. Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba zikihofia usalama wao.

Gazeti la The Telegraph linasema kuwa takriban watalii 500 kutoka Uingereza wataathirika na kauli hiyo. Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya. Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.

Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa. Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.
Al Shabab
Al-Shabab imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi punde kundi hilo likisisitiza kuwa linalipiza kisasi vitendo vya majeshi ya Kenya nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 16, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...