Saturday, May 17, 2014

PROFESA LIPUMBA AWASHANGAA VIJANA WA IRINGA

Baadhi ya vijana waliohudhuria mkutano huo

Lipumba wa CUF akisisitiza jambo

Mchungaji Msigwa wa Chadema
Danda Juju wa NCCR-Mageuzi
 Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Frank Nyalusi (Diwani wa Kata ya Mivinjeni
“Mbona vijana mmezeeka kabla ya wakati?” hilo lilikuwa swali la mshango la Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba.


Profesa Lipumba aliuliza swali hilo mara tu baada ya kupanda jukwaani katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa kuhutubia mkutano wa Ukawa uliolenga kufafanua mchakato mzima wa katiba ulivyo hivisasa na kutafuta ushawishi wa wananchi kupinga kile kinachoendelea katika bunge hilo.

“Vijana mnaonekana kama wazee kwasababu ya hali ngumu ya maisha na leo mnahujumiwa kupata Katiba mpya itakayoletea matumaini kwa watanzania wote; itakayozungumzia haki za msingi, haki za kupata elimu, afya, kazi na zingine” alisema

Alisema uamuzi wao wa kuanzisha Ukawa ulikuja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuteka nyara mchakato mzima kwa kutupilia mbali mapendekezo ya wananchi kupitia rasimu ya pili ya Katiba na kuingiza mambo yao kwasababu ya wingi wao katika bunge hilo.

Awali Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alisema hawatarudi katika bunge hilo mpaka pale wabunge wa bunge hilo watakapokuubali kuijadili Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba iliyowasilishwa bungeni hapo badala ya mapendekezo mapya kutoka kwa CCM.

“Mapambano ya kudai katiba sio ya watu wanaojificha, sio ya watu waoga, ni ya watu walio tayari kujitoa kwa gharama yoyote ile,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Mchungaji Msigwa alisema kama Zanzibar wana nchi yao na hakuna mtu aliyepiga kelele kwa maamuzi hayo kwanini Tanganyika isiwe na nchi yake.

Alisema muungano wanaoutaka Ukawa ni ule wa serikali tatu uliopendekezwa na wananchi kwa kupitia maoni yao waliyotoa kwa tume hiyo.

Profesa Lipumba alisema suala la Katiba sio suala la mzaha kama linavyofanywa na wabunge wa CCM kwasababu linazungumzia haki za msingi za watanzania.

Alisema CCM na wabunge wake wamekuwa wakipinga mapendekezo ya serikali tatu yaliyotolewa na tume hiyo kwa kisingizio cha gharama jambo ambalo halina utafiti wa kutosha.

Alisema: “tatizo la nchi hii sio serikali tatu, tatizo la nchi hii ni matumizi mabaya ya fedha za umma, rushwa, ufisadi, misamaha holela ya kodi na ukubwa wa serikali.

Alisema hayo yote yakifanyiwa kazi kama ambavyo wabunge wapinzani wamekuwa wakipiga kelele bungeni, kisingizio cha kwamba serikali tatu zitaongeza gharama hakitakuwepo.

Alisema rasimu ya Katiba iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kujadiliwa na bunge hilo kabla ya kupelekwa kwa wananchi ina mambo mengi yanayolenga kuboresha ustawi wa taifa hili lakini inapingwa na baadhi ya wanaCCM kwa nguvu za mafisadi.

“Ndugu zangu tunazunguka nchi nzima kuwaeleza watanzania jinsi mchakato ulivyohujumiwa na wanavyotakiwa kujipanga kukataa hila hizo; ni lazima tuwe macho, nchi imekamatwa na mafisadi na wala rushwa ambao hawataki mianya hiyo izibwe kwa kupitia katiba mpya,” alisema.

Alisema rasimu hiyo inazungumzia uadilifu  ambao ni changamoto kubwa kwa baadhi ya viongozi tulionao, inazungumza kupunguza madaraka ya Rais, ukubwa serikali na umuhimu wa wabunge kutokuwa mawaziri, mambo ambayo hayakubaliki na wengi wa CCM.

Awali Sheikh Rajab Kitimba wa Shura ya Imam alisema wameamua kuingia katika kundi la Ukawa ili kusaidia kumaliza kilio cha wananchi.

“Ni sawa na kufanya ibada za kijamii, ibada nje ya nyumba za ibada, kwasababu huko ndiko kwenye asilimia 75 ya watu wa dini mbalimbali wenye msiba tunaotaka kuumaliza kupitia ukawa,” alisema.

Alishangaa sababu ya tume ya Warioba kupewa ridhaa na kutumia fedha nyingi za walipa kodi kwa kazi ambayo mwisho wa siku inakataliwa na wachache.

“Zanzibar, Tanganyika na serikali ya shirikisho ndio mpango mzima; Ukawa ni matumaini yetu na nyinyi mkiiunga mkono kazi ya kupata katiba ya wananchi badala ya ile ya wachache itakuwa nyepesi, tukatae hila, na ghiriba zinazopinga maoni ya wananchi,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Danda Juju wa NCCR-Mageuzi alisema pamoja na mchakato huo kuhujumiwa bado watanzania wana uwezo wa kukataa na hatimaye kupata katiba wanayoitaka. (CHANZO: BONGO LEAKSBLOG)

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...