Sunday, May 18, 2014

ARSENA BINGWA KOMBE LA FA

BAO la dakika ya 109 la Aaron Ramsey limeipa Arsenal ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuichapa Hull City 3-2 ikitoka nyuma kwa 2-0 Uwanja wa Wembley.
Ramsey alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Olivier Giroud na kuondoa uwezekano wa mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Arsenal waliuanza kichovu mchezo huo na kujikuta wanafungwa mabao mawili ndani ya dakika nane, Chester akianza kufunga la kwanza dakika ya nne na Davies akafunga la pili dakika ya nane.
article-2630209-1DF2D11300000578-658_964x520
Santi Cazorla aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 17 kwa shuti la mpira wa adhabu kabla ya Koscielny kufunga la pili dakika ya 72 na Ramsey la ushindi dakika ya 108.
Ushindi huo ni furaha kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hajatawaa taji lolote kwa miaka tisa.
Mara ya mwisho Arsenal walitwaa taji mwaka 2005, ambalo lilikuwa Kombe hilo hilo la FA wakiendeleza mafanikio ya msimu wa 2003-2004 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Ramsey, Cazorla/Wilshere dk105, Ozil/Rosicky dk105, Podolski/Sanogo dk61 na Giroud.
Hull: McGregor, Chester, Bruce/McShane dk67, Davies, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Meyler, Rosenior/Boyd dk103, Quinn/Aluko dk74 na Fryatt.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...