Saturday, May 17, 2014

PROFESA LIPUMBA AWASHANGAA VIJANA WA IRINGA

Baadhi ya vijana waliohudhuria mkutano huo

Lipumba wa CUF akisisitiza jambo

Mchungaji Msigwa wa Chadema
Danda Juju wa NCCR-Mageuzi
 Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ASKOFU DALLU KUSIMIKWA RASMI KESHO


dalu_1b119.jpg
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla, anataraji kuongoza Misa Takatifu ya kusimikwa kwake Askofu Mpya wa Jimbo Kuu la Songea, Mhashamu Damian Dennis Dallu (Pichani).

Tukio hilo litafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba la Jimbo Kuu la Songea hapo kesho. Leo hii baadhi ya waumini wamesafiri mpaka katika mpaka wa Mkoa wa Ruvuma na Njombe kwa ajili ya kumpokea Askofu Dallu anayeingia Jimboni Songea na leo Jumamosi atafanyiwa Ibada ya kukabidhiwa Kanisa.

Tukio hilo linalotaraji kuhudhuriwa na Viongozi wengi wa Madhehebu ya dini, litahudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. (PERAMIHO PUBLICATIONS)
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATU 10 WAUAWA KATIKA MILIPUKO NAIROBI

Haijulikani na nani aliyesababisha milipuko ingawa washukiwa tayari wamekamatwa
Milipuko miwili ilitikisa Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi na kuwaua watu 10 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa..
Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa.
Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea ndani ya soko.
Soko la Gikomba ni maarufu kwa nguo za mitumba
Milipuko hiyo ilitokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wawu wenye uhusiano na kundi la wanamgambo la kiisilamu nchini Somalia la Al Shabaab. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC Swahili

USALAMA WA NIGERIA KUANGAZIWA UFARANSA

Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anaanda mkutano hii leo mjini Paris kuangazia hali ya usalama nchini Nigeria.
Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi kutoka nchi za Nigeria,Benin,Cameroon,Chad na Niger ili kutafuta njia za kukabiliana na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko haram.

Wawakilishi wa Marekani muungano wa Ulaya na Uingereza wataangazia kazi iliofanywa na wataalam wa Uingereza, Ufaransa na Marekani waliotumwa nchini humo ili kuisaidia mamlaka ya Nigeria kuwanusuru zaidi ya wasichana 200 waliotekwanyara na kundi hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo: BBC Swahili

Friday, May 16, 2014

BIRTHDAY YA RAY, JOHARI AMPA SALAMU TATA..... ISOME HAPA....!!!

http://jambotz8.blogspot.com/
Leo ni birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa
Leo mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray anasherehehea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa wenzie. Moja ya watu wa kwanza kwanza kumpa salamu hiyo ni swahiba na rafiki yake mkubwa, JB akifuatiwa Johari ambaye salamu yake inadaiwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni kwa namna flani inamponda mpenzi wa sasa wa Ray, Chuchu Hans, kutokana na maneno yaliyotumika ya salamu hiyo ambayo Johari anadaiwa kuwahi kuyatumia kumponda Chuchu siku za nyuma.

JB ameandika
''Happy birth day mdogo wangu Ray. Mungu akupe haja ya moyo wako.''

Na huku Johari akiandika 
''Happy birthday director wa RJ na swaiba wangu Mungu akuongoze akupe maisha marefu na akuepushe na ‘’mabarazuri’’
Jambo Tz inakupongeza sana Ray kwa kutimiza miaka kadhaa siku ya leo na  Mungu akupe maisha marefu zaidi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WASSIRA AWATISHA UKAWA


Stephen Wassira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ATOA KAULI YA KUWABAGUA WANZANZIBAR BUNGENI...!!!

weremapx_89c87.jpg
Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema 'amelikoroga na kulinywa mwenyewe', baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.

Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15. Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.

Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo. "Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu," alisema Werema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATALII TOKA UINGEREZA WATOROKA MOMBASA


Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya. Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba zikihofia usalama wao.

Gazeti la The Telegraph linasema kuwa takriban watalii 500 kutoka Uingereza wataathirika na kauli hiyo. Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya. Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.

Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa. Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.
Al Shabab
Al-Shabab imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi punde kundi hilo likisisitiza kuwa linalipiza kisasi vitendo vya majeshi ya Kenya nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 16, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Thursday, May 15, 2014

MWANAMKE AHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUASI DINI...!!!

Serikali imesema kuwa Sudan sio nchi ya kwanza kutekeleza sheria za kiisilamu
Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo. Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.
Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Maafisa wakuu wanasema kuwa licha ya Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake. Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikasalia.
Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo. SShirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
'Kesi ya kwanza'
Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan , kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu. Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao kuihusu. Maafisa hao wamewataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.
Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi zingine zinazofuata sheria za kiisilamu. Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC 

IJUE HISTORIA YA KAMPUNI YA MABASI YA SCANDINAVIA EXPRESS ILIYOLETA HESHIMA KWA TAIFA...!!!


Kampuni ya mabasi ya Scandinavia Express ni kampuni pekee ya kitanzania iliyowahi kutokea kwa kuwa na huduma za uhakika na za viwango vya hali ya juu kabisa kulinganisha na huduma zinazotolewa na kampuni za sasa. Kampuni hii ilijijengea jina kubwa na sifa nzuri ndani na nje ya nchi kwa huduma bora walizokuwa wakizitoa kwa abiria wake na pia kuliletea sifa taifa la Tanzania kwa kujulikana kuwa na mabasi ambayo ni quality na high class.

Kampuni ya Scandinavia ilianzishwa zaiidi ya miaka thelathini na tano (35) iliyopita ikiwa na mabasi machache tu aina ya LEYLAND  na ilipofika mwaka 1982 kwa mara ya kwanza Scandinavia walinunua basi lao la kwanza la kisasa kutoka kampuni ya SCANIA TANZANIA COACHES aina ya SCANIA ambalo kutokana na ubora  wake na uzuri wake kwa kipindi hicho waliamua kulitumia kwa safari yao mpya waliyoianzisha ya Dar es salaam hadi Iringa.
BASI LA KWANZA LA KISASA KUNUNULIWA NA SCANDINAVIA 1982
Kadiri mahitaji ya usafiri yalivyokuwa yakiongezeka ndipo michirizi ya rangi ya BLUU,KIJIVU na NYEKUNDU ikaanza kuonekana katika mabasi mengi zaidi yaliyokuwa yakisafirisha abiria karibia kila kona ya Tanzania.
Ilipofika mwaka 2001 kampuni ya Scandinavia walianzisha safari yao ya kwanza kabisa kutoka nje ya nchi kwa safari ya Dare es salaam hadi Nairobi nchini Kenya,ambapo mafanikio ya ruti hiyo yalipelekea kuzaliwa kwa ruti nyingine kati ya Nairobi hadi Mombasa na Mombasa hadi Dar es salaam. Katika mwaka wa 2002 kampuni ya Scandinavia walipanua wigo wa huduma zao kwa kuanza ruti mpya ndani ya Afrika mashariki kwa safari za Dare es salaam hadi Kampala nchini Uganda.
Ilipofika mwaka 2003 kampuni ya Scandinavia ilipanua wigo zaidi kwa kuanza kwenda katika mji mkuu wa nchi ya Zambia Lusaka. Wakati huo wote kampuni ya Scandinavia ilikuwa chini ya mkurugenzi na mwanzilishi wake MR.MUHAMED ABDULLAH. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

UTALII WA NGONO WANAWIRI MALINDI NCHINI KENYA...!!!

jambotz8.blogspot.com
Utalii wa Ngono wanawiri Malindi Kenya
Unapouzuru mji wa Malindi uliopo kwenye mwambao wa Kenya unaonekana kama paradiso.
Hata hivyo mji huu ni kitovu kilichojificha cha biashara ya ngono ya watoto. Watoto wadogo wenye umri wa miaka hata 12 hutumiwa katika ukahaba na filamu za ngono na watalii ambao huwa tayari kulipa pesa nyingi kwa ajili ya ngono katika maeneo yaliyojificha. Maafisa wanasema biashara hii imependwa sana na wasichana hao wadogo na wavulana kiasi kwamba wengi wao huacha shule.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba ameiambia BBC kuwa aliacha shule kutokana na ufukara. Alivutiwa kuingia katika biashara ya ngono baada ya rafiki yake aliyekuwa akifanya kazi hiyo kukutana na mtalii aliyempeleka bara Uropa na sasa anaishi maisha ya ustaarabu. Maisha ni hayo hayo pia kwa wasichana.
jambotz8.blogspot.com
Utalii wa Ngono wanawiri Malindi Kenya
Msichana mmoja ameiambia BBC kuwa alianza biashara ya ngono akiwa na miaka 15, bila mamake kujua. Anaeleza ugumu wa biashara hiyo na jinsi wasichana wanavyogeuzwa kuwa watumwa wa ngono na hata kulazimishwa kushiriki tendo hilo na wanyama kama mbwa.
Hatahivyo anasema haoini ubaya wowote kwani ndiyo njia pekee inayomuwezesha kujimudu kimaisha.
Juhudi za mamake kumshawishi aiache biashara hiyo zimeambulia patupu. Ni suala linalowasumbua viongozi katika jamii hii. Naibu chifu wa kata ndogo ya Shela, Mayele anasema watu wengi hawatoi ripoti kwa serikali. Sasa Chifu huyo ameanzisha harakati kwa jina ''rudi shule'' ambapo watoto wakipatikana mjini wakati wa shule wanakamatwa na kupelekwa nyumbani, kisha wazazi wao kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Anaamini kwamba mambo yataimarika, lakini changamoto bado ni nyingi.  
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MTOTO AANGUKA TOKA GHOROFA YA 11 ANUSURIKA...!!!

Mtoto aanguka toka ghorofa ya 11 anusurika
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani. Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia kuishi. Musa aliteleza katikati ya mianya inayozingira sebule yao katika ghorofa ya 11 ya mjengo huo wenye nyumba na makazi ya watu.

Muuguzi mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya kuanguka katika eneo lisilo kavu sana. Jamaa na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio hilo. Tukio hilo lilizua mjadala kama ni muujiza au la kuwa amenusurika kifo lakini watafiti wameelezea kuwa mtoto ananafasi nzuri zaidi ya kuishi hata baada ya kuanguka ama kupatwa na janga lolote lile kwani mwili wao bado ni mwororo na mifupa ya mtoto huwa bado ni laini kinyume na mtu mzima ambaye tayari mifupa yake ni kavu na mwili wake ni mkubwa na mzito.

Abdirizak Bihi alisimulia muujiza huo kwa gazeti la The Star-Tribune. "baada ya kushuhudia yaliyotendeka hapa ninahofia usalama wa wazazi wa mtoto ambao hadi kufikia sasa wamepigwa na bumbuazi hawazungumzi na yeyote."
Dakta Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo. Bila shaka huu ni muujiza wa Mwenyezi mungu kwa familia hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC

SEVILLA MABINGWA WA EUROPA

Sevilla ndio mabingwa wa ligi ya bara Uropa mwaka 2014.
Vigogo hao wa ligi kuu ya Uhispania la liga waliwalaza Benfica kutoka Ureno mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti.
Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu suluhu bin suluhu katika muda wa kawaida na ziada katika mechi hiyo iliyochezewa mjini Turin Italia.
Ushindi huo ulidhibitishia mashabiki wa kandanda kote duniani ufanisi wa ligi kuu ya Uhispania La Liga kwani ulikuwa ushindi wa tatu kwa timu hiyo ya Sevilla katika kipindi cha miaka mitatu .
Kwa upande wake Benfica sasa itasubiri muda zaidi kwani hawajashinda katika fainali nane sasa.
Mara ya mwisho timu hiyo kushinda taji lolote barani Uropa ilikuwa ni miaka 50 iliyopita 1962 .
Mechi hiyo iliishia sare tasa na ulipowadia wakati wa kuamua kupitia mikwaju ya penalti ni kipa wa Sevilla Beto aliyeamua taji hilo litaenda Uhispania wala sio Ureno.
Beto aliokoa mikwaju miwili ya Oscar Cardozo na Rodrigo na kuitunuku Sevilla taji la Europa kwa ushindi wa mabao 4-2.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...