Thursday, September 19, 2013

MATOKEO KAMILI LIGI KUU TANZANIA

1111 1e313
YANGA 1 - 1 Prisons,
SIMBA 6 - 0 Mgambo
Kagera 2 - 1 JKT Oljoro (HM)
Azam 1 - 1 Ashanti
Coastal 1 - 1 Rhino
Mtibwa 0 - 0 MBEYA City
Ruvu Shooting 1 vs 0 JKT Ruvu. Chanzo: Shaffihdauda

ANGALIA VIDEO YA LINAH AKIFUNGUKA JUU YA PENZI LAKE NA AMINI




Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa ni mjasiriamali pia Anasteria Sanga Linah au muite Ndege Mnana amefunguka kuwa producer wa studio ya Bhitz Pancho Latino ndiye mwenye siri nzito ya penzi lake na msanii mwenzake Amini ambaye kwasasa penzi lao limekuwa stori ya kale baada ya kuachana. Linah amesema tokea wanaanza mapenzi yao Pancho ndiye alikuwa mtu pekee anayejua mambo mengi kuwahusu wao na jinsi walivyotumbukia katika penzi ambalo anasema yeye binafsi ndiye hasa alikuwa akimpenda Amini kupita kiasi japo baadaye akagundua kuwa hata mwenzake naye anamzimika na hivyo penzi likawa linasonga.

"Yaani we muulize Pancho yule ndio ana siri kubwa sana ya penzi langu na Amini,yaani jamani nilimpenda sana Amini mpaka nikakubali kuingia kwenye mapenzi na nilimpenda hasa kutoka moyoni,kuna vitu vingi nyuma yake ambavyo Pancho anajua",alisema Linah.

Msanii huyo mwenye sauti tamu kiasi cha kupachikwa jina la Ndege Mnana na msanii mkongwe Patricia Hillary ameendelea kufunguka kuwa wakati ameangukia katika penzi la Amini alikuwa anawachomolea wanaume wengi waliokuwa wanamtokea tena wenye pesa zao na wengine ni watu wazito lakini aliamua kutoka moyoni kwa dhati kuwa na Amini kwahiyo akawa anamtunzia heshima yake.

RIPOTI YA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNES MASOGANGE NA MELISA HUKO AFRIKA KUSINI..!!

WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.
 
Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
 
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
 
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

NAPE AWACHONGANISHA CHADEMA NA WAKULIMA WA PAMBA

blog_756b7.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya Sabasaba. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira.
-Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema.
-Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.

Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu. Alisema hoja kuwa ambayo imewakera na kuwasumbua Chadema ni hatua zinazochukuliwa hivi sasa kwa pamoja kati ya Serikali ya CCM na Serikali ya China ambayo hivi sasa inaelekea kuzaa matunda ya kutoa mwanya wa ajira zaidi ya elfu- 25 viwandani.

WABUNGE WA NIGERIA WAPIGANA BUNGENI

nigerian-parliament_bc42b.jpg
Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake.


Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya mwenyekiti wa mrengo wa wabunge waliojiondoa kutoka kwa chama tawala, Kawu Baraje, kuingia bungeni akiandamana na magavana wanaomuunga mkono.
Inaarifiwa spika wa bunge la waakilishi ,Aminu Tambuwal, aliambia wabunge kuwa Baraje aliomba ruhusa kuwahutubia wabunge wa mrengo wake kabla ya bunge kuanza vikao vyake.
Lakini kuwepo kwa wabunge hao bungeni kuliwaghabisha mno wafuasi wa chama tawala, PDP,kiasi cha kuzuka sokomoko bungeni kati ya pande hizo mbili na kumlazimisha bwana Baraje kukatiza hotuba yake kutokana na kelele bungeni.
Chama tawala PDP kina wabunge wengi zaidi bungeni wakiwa 23 kati ya wabunge wote 36
Aidha chama hicho kimetawala Nigeria tangu kupata uhuru mwaka 1999 lakini hivi kribuni kimezongwa na migogoro ya ndani ya chama pamoja na kukabiliwa na upizani wenye ushawishi.
Wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mwaka 2015, lakini wadadisi wana wasiwai ikiwa chama tawala kitakuwa kimesuluhisha migogoro yake, huku kikikabiliwa na upinzani mkali.
Mgogoro huu umekuwa ukitokota kwa miezi kadhaa huku baadhi ya wabunge wakitofautiana kuhusu ikiwa Rais Goodluck Jonathanaidhinishwe na chama kugombea urais kwa mara nyingine wakati kuna wanasiasa wengine wanaotaka kugombea urais.
Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa Nigeria kurushiana ngumi bungeni.

Wednesday, September 18, 2013

TANZANIA YAMEGWA EAC

*Rwanda, Kenya, Uganda na Burundi zaungana kuunda Shirikisho la Kisiasa
*Waziri Sitta asema zina ajenda ya siri, ashangaa marais kuwaburuza wananchi wao

HATIMAYE Tanzania imewekwa kando rasmi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika kuunda Shirikisho la Kisiasa litakaloziongoza nchi hizo.

Tayari marais wa nchi hizo, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamekwishafikia makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC, bila kuishirikisha Tanzania.

Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki, yalifikiwa Septemba 12 mwaka huu, mjini Kampala na marais wa Rwanda, Kenya na Uganda na hivi karibuni Rais wa Burundi ambaye alialikwa katika mkutano huo na kushindwa kuhudhuria, naye sasa amethibitisha ushirika wake katika shirikisho hilo jipya.

Gazeti la The Sunday Times la Rwanda, limemnukuu Waziri Musoni kuwa marais wa nchi hizo wamekubaliana kukamilisha rasimu hiyo ndani ya muda mfupi.

SERIKALI YATOA ONYO KALI KWA BALOZI WA CHINA ALIYEHUDHURIA MKUTANO NA WA CCM

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imehadharisha mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini, kuepuka kujihusisha na mambo ya ndani.

Hadhari hiyo imetolewa jana katika taarifa ya wizara hiyo kwa vyombo vya habari, baada ya Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lu Younqing, kuonekana katika mkutano wa hadhara wa CCM, akiwa amevalia kofia yenye nembo ya chama hicho.

“Wizara inaelekeza kwamba kitendo cha Balozi yeyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, na kuvaa sare zenye nembo ya vyama vya siasa, sio sahihi na kinakiuka Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa 
kidiplomasia.

“Mkataba huo wa Vienna unazuia wawakilishi wa nchi za nje kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi, ikiwemo siasa wanapofanya kazi zao katika nchi za uwakilishi,” ilieleza taarifa hiyo iliyotumwa na msemaji wa wizara hiyo, Mkubwa Ally.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa hata Sheria ya Diplomasia ya Tanzania ya Mwaka 1986, ambayo ni zao la Mkataba wa Vienna, pia hairuhusu Balozi au mfanyakazi wa Ubalozi, kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 18, 2013

DSC 0013 c0ea2
DSC 0014 12cc6

MSEMAJI WA BROTHERHOOD AKAMATWA MISRI

misri b89cf
Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali
Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.
Taarifa zinazohusianaMisri
Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.
Serikali ya Misri imekuwa ikifanya msako dhidi ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Awali, mahakama ya uhalifu mjini Cairo, iliamua kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na lile la Gamaa Islamiya kupigwa tanji.
Viongozi wa mashtaka waliwaekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie, Shater na wengine wengi mnamo mwezi Julai.
Wengi wao wamezuiliwa kuhusiana na madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Mamia ya watu wanataka Bwana Morsi kurejeshwa mamlakani , wengi wakiwa wanachama wa Brotherhood .
Aidha makabiliano yaliyotokea mwezi jana kati na polisi na wafuasi wa Morsi yalisababisha vifo vya wanachama wengi pale polisi walipovamia kambi zao mbili walipokuwa wanataka Morsi kurejehswa mamlakani. Chanzo: bbcswahili

BABU WA MIAKA 95 AMUOA BABU MWENZIE WA MIAKA 65



Wanaume wawili wazee ambao ni maaskari wakongwe walioshiriki vita ya pili ya dunia, ijumaa iliyopita (September 13) walifunga ndoa ya jinsia moja (mashoga) baada ya kuwa katika uhusiano kwa miaka 20 kabla ya kufikia uamuzi wa kuoana.
gays-1

John Banvard mwenye miaka 95 alimuoa Gerald Nadeau mwenye miaka 67 huko Diego, California Marekani.

RPF CHAIBUKA NA USHINDI NCHINI RWANDA

zkagame_32c2c.jpg
Chama tawala nchini Rwanda, RPF kimeibuka mshindi katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumatatu.
Chama hicho chake Rais Paul Kagame kimeshinda uchaguzi huo kwa asilimia 76 ya kura zote zilizopigwa .
Aidha chama hicho kiliingia mamlakani baada ya mauaji ya kimbari yaliyofanyika mwaka 1994 na kimepata viti 40 kati ya 53 vilivyokuwa vinawaniwa.


Chama cha upinzani, FDU-Inkingi, ambacho kiongozi wakeVictoire Ingabire yuko jela, hakikushiriki uchaguzi huo kwani hakijasajiliwa rasmi.
Vyama vingine viwili vya kisiasa vinavyosemekana kuwa washirika wa RPF, vilipata asilimia 13 na asilimia tisa ya kura.
Shughuli ya kupiga kura ilifanyika siku mbili baada ya vifo vya watu wawili kutokana na shambulio la maguruneti mjini Kigali.

MAGUFULI AAGIZA VITUO VYA MIZANI YA BARABARANI MKOANI IRINGA VICHUNGUZWE


Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (pichani) ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu utendaji wa vituo vya mizani mkoani Iringa. Agizo hilo lilitolewa katika mkutano ambao Waziri huyo wa Ujenzi alikutana na wafanyakazi wa taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi mkoani humo.

Wakati akisomewa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya kila taasisi mkoani humo ndipo lilipojitokeza suala la tozo iliyokusanywa kwa magari yaliyokamatwa yakiwa yamezidisha uzito kwa kipindi cha mwezi mmoja wa Julai mwaka huu wa 2013 katika kituo cha mizani cha Wenda kilichopo kati ya Iringa na Ifunda katika barabara kuu ya TANZAM.


Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Iringa Injinia Poul Lyakurwa alimtaarifu Waziri Magufuli kuwa kiasi cha Shilingi milioni 31.9 kilikusanywa katika kipindi hicho cha mwezi mmoja.
 
Akishitushwa na kiwango hicho Waziri Magufuli  alibainisha kuwa, kiasi hicho kilichosomwa katika taarifa kimetokana na magari 735 yaliyokamatwa kati ya magari 20,700 yaliyopimwa sawa na asiliamia 3.5. “Takwimu hizi sizikubali kwani wastani wa magari yanayokamatwa katika nchi nzima unakaribia asiliamia 40 iweje barabara kuu kama hii iwe na kiwango kidogo kiasi hicho cha magari yaliyokutwa na makosa” hapa ni lazima pafanyike uchunguzi” alisisitiza Mheshimiwa Magufuli na kueleza kuwa hali hiyo hawezi kuiruhusu hata kidogo kuendelea.

KIGOGO WA MAGARI YA WIZI TZ ANASWA....!!!


Jengo ambalo linadaiwa ndiyo kiwanda hatari cha kubadilisha magari ya wizi, kimefumuliwa na mmiliki wake sasa hivi yupo nyuma ya nondo akingoja kufikishwa mahakamani.
 
Kigogo wa magari ya wizi, Benovilla Luhanga baada ya kunaswa.
Benovilla Luhanga, 43, ametajwa kuwa ndiye mmiliki wa kiwanda hicho na siku ananaswa, alikutwa na magari ya kihafari matano ambayo yote inadaiwa ni ya wizi.
Vilevile, Luhanga alikutwa na Bajaj moja ambayo imedaiwa nayo ni ya wizi na kwamba alikuwa tayari ameshaibadili rangi.
Luhanga alikamatwa akiwa na mkewe ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
 
Moja ya gari alilokutwa nalo mtuhumiwa.

KESI YA MAKAMU WA RAIS KENYA, SHAHIDI WA KWANZA ATOA USHAHIDI ICC

zruto_fecef.png
Shahidi wa kwanza kutoka upande wa mashtaka, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi dhidi ya naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake.
Ruto anakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008
Kesi dhidi ya Ruto na mshtakiwa mwenzakeJoshua Arap Sang, ilianza tarehe 10 mwezi Septemba, baada ya wawili hao kutuhumiwa katika kuhusika na ghasia hizo za mwaka 2007.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mashahidi kujiondoa kwenye kesi hiyo wakihofia usalama wao. Mwishoni mwa wiki, mashahidi wanne walijiondoa katika kesi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwa watatoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Wiki jana mkuu kwenye kesi hiyo, aliakhirisha kesi hiyo kwa sababu mashahidi hawakuwa wamefika kwenye mahakama hiyo kutoa ushahidi wao.
Rais Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba kwa mashtaka sawa na hayo.

MADEREVA WA BODABODA DAR WAUA JAMBAZI

MAJAMBAZI wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti Dar es Salaam akiwamo mmoja aliyeuawa na madereva wa pikipiki katika eneo la Vingunguti karibu na kituo cha mafuta. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa majambazi wapatao wanne walimvamia mfanyabiashara Abas Mussa (47) wa Vingunguti wakiwa na bunduki na mapanga.

Alisema mfanyabiashara huyo akiwa dukani kwake, ghafla walifika vijana wawili, mmoja akiwa na bunduki fupi na mwingine akiwa na panga na kumpora mwenye duka Sh 1,400,000.

Pia walimpora simu moja ya Nokia na ufunguo wa gari na alipotoka nje ya duka alisikia mlio wa bunduki na kumuona mfanyakazi wake Ally akiwa chini na watu wengi wakiwa wamejikusanya.

Alisema baada ya tukio hilo kutokea madereva wa pikipiki waliwaona majambazi hao na kuwafukuza na walipofika njia panda ya Tabata Relini walimkamata jambazi mmoja na kuwashambulia hadi kumjeruhi.

Kamanda alisema polisi walipata taarifa na walipofika eneo la tukio walimkuta jambazi huyo akiwa na hali mbaya. Walimchukua na kumpeleka hospitali lakini alifariki dunia akiwa njiani.

Alisema jambazi mmoja alikimbia baada ya kuacha pikipiki ya Sunlag na polisi waliweza kuwakamata waliokimbia baada ya tukio hilo.

Katika tukio jingine, jambazi mmoja aliuawa na polisi wakati majambazi sita walipojaribu kupora mamilioni ya fedha katika mtaa wa Jamhuri Kitumbini.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...