Wednesday, August 14, 2013

PONDA: RISASI ILINICHANGANYA....!!!


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema alichanganyikiwa kiasi cha kushindwa kujielewa kwa muda baada ya kupigwa risasi.
 
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi kwenye wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alikolazwa jana, Sheikh Ponda alisema kutokana na hali hiyo hakumbuki matukio yaliyofuata baada ya hapo.
“Sikumbuki hata nilipata huduma ya kwanza hospitali gani kwa sababu sikuwa katika hali ya kawaida. Mambo mengine yaliyotendeka kabla ya kujeruhiwa ninayakumbuka vizuri,” alisema Ponda ambaye inasadikiwa kwamba alipigwa risasi ya begani, Ijumaa iliyopita mjini Morogoro.
Alisema alihutubia katika Kongamano la Waislamu kwa muda mfupi akizingatia muda uliokuwa umetolewa kumaliza mkutano huo na baada ya hapo alishuka na kupanda kwenye gari binafsi ambalo lilizingirwa na polisi ndipo akaamua kushuka na kuanza kutembea kabla ya kujeruhiwa.

Tuesday, August 13, 2013

NDAUKA AANZA KUNG'AA ANGA ZA MUZIKI.....!!!

MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo ya aina yake ya nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG, katika tamasha la sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa single inayoenda kwa jina la  'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.


 
 Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na kazi ya filamu ambayo ameizoea.

Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.

"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema Ndauka.

TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI )


Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.

 
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.

 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
 

-Bongo5

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AUGUST 13, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

MWINGEREZA ADAKWA NA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SH 118,314,900

 (Picha na maktaba)

RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.

Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.

Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.

Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.

CRDB YAKABIDHI WODI YA WAZAZI NA VIFAA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA META-MBEYA


 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki. 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.

Monday, August 12, 2013

HII HAPA BARUA RASMI YA MWINYI KAZIMOTO KWA TFF AKIOMBA MSAMAHA KWA KITENDO CHA KUTOROKA



MWINYI KAZIMOTO

AL MARKHIYA SPORTS CLUB
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM 
TANZANIA

YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA MPIRA TANZANIA
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya cha kuondoka kambini timu ya taifa na kuiacha nchi yangu katika kipindi kigumu hali ya kuwa walikuwa na mechi ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa lengo langu kuidhoofisha nchi yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza mpira nje ya nchi ndiyo iliyonifanya niondoke katika kipindi hicho, na nashukuru mungu nimefanikiwa kupata team nchini Qatar, naamini watanzania wataipokea habari hii kwa vizuri.
Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia watanzania na chama cha mpira kwa ujumla kwamba naahidi nitaitumikia nchi yangu muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu

MWINYI KAZIMOTO,,chanzo shafih dauda.

MASIKINI WASTARA ALA IDD MAKABURINI...!!!

STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, yeye ameamua kula Sikukuu ya Idd El Fitr kwa staili ya tofauti na watu wengine ambapo alikula kaburini kwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Ishu hiyo ilijiri Ijumaa iliyopita siku ya sikukuu hiyo ambapo Wastara alitundika picha zake zikiwa zinamuonesha akiwa ameshika tama na nyingine akiwa analifanyia usafi kaburi la marehemu Sajuki lililopo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
 
Wastara alikiri kuwa aliitendea haki Sikukuu ya Idd kwani alipata nafasi ya kuzuru kaburi la mumewe na kujisikia faraja japo kimwili hayupo naye lakini kiroho wako pamoja.
“Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu milele,” aliandika Wastara.
 
Mashabiki wake na wadau mbalimbali walimpa pole huku wengine wakimpongeza kwa hatua hiyo kwani wasanii wengine waliotumia sikukuu hiyo kujiremba, kwenda klabu na kujirusha. Sajuki alifariki dunia Januari 2, mwaka huu na kuacha mtoto mmoja wa kike.

PETE NA CHENI ANAZOVAA DIAMOND ZINA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 24...!!!


Akihojiwa juzi kwenye kipindi cha The Trend cha NTV, mtangazaji wa show hiyo Larry Madowo aliuliza thamani ya bling alizokuwa amevaa.
“It’s a bit expensive,” alijibu Diamond huku akizishika bling hizo.

“Kama hii na hii it’s about dola 2000 something au 1,500, hii peke yake dola 2,000.”

Hata hivyo zingine alishindwa kukumbuka bei yake japo kwa kuangalia saa yenye diamond aliyokuwa nayo, pete zingine mbili za dhahabu na almasi na cheni mbili kubwa za dhahabu gharama yake kwa ujumla inaweza kufika dola 15,000 ukijumlisha na hizo zingine alizotaja gharama yake.

“Zina rates tofauti lakini ni gharama kidogo,” alisema staa huyo.

“Zina ishara? Maanake wengine wanaweza kusema ni Illuminati ama nini,” aliuliza Larry.

“Sidhani mimi navaa tu hii diamond ni jina langu, hii crown as mtu anayelead, kuna diamond nyingi hapa, hii ina alama flani kama ya batman as am flying,” alijibu Diamond.

Aidha Diamond alimtaja Usher Raymond kama msanii anayemtazama na kufuata nyayo zake zaidi.

“I don’t know men, namuona kama anajua sana anachokifanya, tangia nilipokuwa nikimfuatilia mpaka leo. Unajua wanamuziki wengi akitoka mwanamuziki flani yeye anapotea, Usher Raymond yupo. Ukiangalia vitu vyangu mimi namuiba sana. MSIKILIZE HAPO CHINI

FLAVIANA MATATA AENDELEA KUITOA KIMASOMASO TANZANIA, AFRIKA NA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu
NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na  wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.
Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya  uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models.
Akizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.

MGOSI: NARUDI UPYA MSIMU UJAO LIGI KUU...!!!



Mussa Hassan Mgosi.
 
Na Martha Mboma
 
MSHAMBULIAJI mkongwe hapa Bongo, Mussa Hassan Mgosi, amesema amerudi upya, hivyo mashaibiki wake watarajie mambo mapya katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo amejiunga na Mtibwa Sugar hivi karibuni akitokea JKT Ruvu. Kabla ya hapo alikuwa akiichezea timu ya DC Motema Pembe ya DR Congo ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema kwa sasa anaendelea na maandalizi ya nguvu, hivyo mashabiki watarajie vitu vipya kutoka kwake.
 
“Nimerudi kivingine katika soka, hivyo mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu, ninaamini nitafanya vizuri.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AUGUST 12, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


SHEIKH PONDA NA UAMSHO WAHUSISHWA NA SHAMBULIO LA TINDIKALI, ZANZIBAR


Victims Kirstie Trup and Katie Gee
Gazeti la kila siku la Telegraph la hapa Uingereza linaripoti kuwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislam visiwani Zanzibar wanaamini kuwa shambulio la tindikali dhidi ya mabinti wawili wa Kiingereza, Kirstie Trup na Katie Gee lilifanywa na wafuasi wa kikundi cha UAMSHO, ambacho kinataka Zanzibar ijitenge na Tanzania Bara na kisha kuanzisha sheria kali za Kiislam.

Huko nyuma kumeshatokea mashambulizi dhidi ya viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo, ikiwa ni pamoja na mashambulio ya tindikali na mauaji.


"Ofkoz, itakuwa kazi ya Uamsho," alinukuliwa Sheikh Fadhil Soraga, aliyeshambuliwa kwa tindikali Novemba mwaka jana, na anaamini wahusika katika tukio hilo dhidi yake walikuwa UAMSHO.



Wiki mbili zilizopita, vipeperushi vya vyenye wito mkali wa uchochezi dhidi ya Wakristo vilisambazwa sehemu mbalimbali huo Zanzibar, tukio linalohusishwa na harakati za UAMSHO.



"Siku 10 tu zilizopita, walikuwa wanasema wanaandaa kitu kikubwa. Tukio hili, ambalo Waislamu wote twapaswa kulilaani, ni kazi ya kundi hilo (UAMSHO)," alisisitiza Sheikh Soraga.

MWANAUME AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI NA MPENZI WAKE JIJINI DAR....!!!

MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude. 

Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi. Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali. 
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa. 

Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana. Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.

MAN UNITED WAIBUKA VINARA WA NGAO YA HISANI BAADA YA KUITUNGUA WIGAN KWA MAGOLI 2 KWA O KATIKA DIMBA LA WEMBLEY




 Meneja Mpya Wa Man U David Moyes akiwa ameshika ngao ya Hisani pamoja na Mchezaji wa Man U mara baada ya kukabidhiwa leo katika uwanja wa Wembley baada ya kuitungua Wigan Kwa Magoli 2 kwa 0. Hili ni Kombe la Kwanza kwa Kocha Mpya huyo wa Man United david Moyes




Wachezaji wa Man U wakishangilia Mara baada ya Kuibuka Kinara kwa kuitungua Wigan 2 kwa 0 katika Mchezo wa Kuwania Ngao ya Hisani uliofanyika Katika Dimba la Wembley Uingereza

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...