Monday, August 12, 2013

MGOSI: NARUDI UPYA MSIMU UJAO LIGI KUU...!!!



Mussa Hassan Mgosi.
 
Na Martha Mboma
 
MSHAMBULIAJI mkongwe hapa Bongo, Mussa Hassan Mgosi, amesema amerudi upya, hivyo mashaibiki wake watarajie mambo mapya katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo amejiunga na Mtibwa Sugar hivi karibuni akitokea JKT Ruvu. Kabla ya hapo alikuwa akiichezea timu ya DC Motema Pembe ya DR Congo ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema kwa sasa anaendelea na maandalizi ya nguvu, hivyo mashabiki watarajie vitu vipya kutoka kwake.
 
“Nimerudi kivingine katika soka, hivyo mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu, ninaamini nitafanya vizuri.
“Ninaamini msimu ujao timu yetu ya Mtibwa itafanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi chetu kinachoundwa na vijana wengi chipukizi wenye uwezo mkubwa.
“Kikubwa nahitaji ushirikiano, kitu ambacho ni muhimu katika kupata mafanikio ya timu katika msimu ujao,” alisema Mgosi.
 
Mgosi aliwahi kuichezea Simba kwa mafanikio. Msimu wa 2009/10 aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku yeye akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 16.CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS BLOG              

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...