Saturday, June 15, 2013

POLISI WAMTIA MBARONI MAMA ALIYEMTUPA MTOTO BAADA YA BABA WA MTOTO KUMKANA KISA ANA NYWELE ZA KIARABU



Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Khadija Idd anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro akidaiwa kumtupa barabarani mtoto wake mwenye umri wa miezi 6 baada ya mwanaume aliyezaa naye kumkataa.

Shuhuda wetu ambaye ni dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Shabani, alisema tukio hilo lilitokea Juni 11, mwaka huu maeneo ya Mafiga karibu na Msikiti wa Mahita ambapo Khadija alichukua uamuzi huo baada ya mwanaume aliyezaa naye kumgomea mtoto kwa madai ana nywele za Kiarabu hivyo si wake.


“Huyu dada alifika kwenye kijiwe chetu akiwa amembeba mtoto mgongoni na kukodi pikipiki ili nimpeleke mjini.

“Tulipofika kwenye msitu uliopo karibu na mashamba ya SUA, aliniambia niendeshe spidi kuna mtu anamuwahi.

Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.

RAIS OBAMA AHAIRISHA ZIARA YAKE YA KUZITEMBELEA NCHI ZA AFRICA IKIWEMO TANZANIA...!!!


WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
 
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.

Taarifa iliyonaswa na kutoka katika mitandao mbalimnali  nchini Uingereza na Marekani  zinaeleza kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi Barani Afrika.
 
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
 
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Katika msafara wa Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi, kwa ajili ya kulinda ndege ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo pea maalum za magari zitakazo sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia ndege za jeshi kwa ajili kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo" alisema Mseaji wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.

Nakala ya taarifa hiyo  pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
 
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni 96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.

LOWASSA ATANGAZA NDOTO YAKE, ISOME HAPA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono walimu walioshiriki katika hafla ya harambee ya kuchangia Saccos ya walimu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi, jana. Picha na Dionis Nyato. 
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa ana ndoto kwamba siku moja sekta ya elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini na kuzikomboa rasilimali za taifa la Tanzania zinazowanufaisha wageni na kuacha wananchi wakiambulia faida kidogo.Huku akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake, Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani. 
Akizungumza wakati wa kuchangia SACCOS ya walimu ya Moshi Vijijini, Ushirika wa Stadium jana, Lowassa alisema kuwa katika ndoto yake anawaona viongozi wakikubali kwamba elimu bora ndiyo italisaidia taifa kuumiliki utalii na kunufaika nao, badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao, huku Watanzania tukiambulia makombo.Wakati Lowassa akieleza ndoto yake hiyo, Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo Augustine Mrema amesema: “Biashara ya urais imenishinda namwachia Lowassa kwani mimi nimeamua kurudi kwenye biashara ya rejareja.”

MSANII WA VICHEKESHO MASELE APATA AJALI YA GARI...!!!

 


Habari za uhakika ni kuwa muigizaji wa vichekesho hapa nchini maarufukwa jina la ''Masele cha Pombe'' ni mzima wa afya na hajafariki kamabaadhi ya tetesi zilivyoanza
kuenea kwa kasi.tetesi kuwaMasele amepata ajali ya gari
maeneo ya barabara ya 14 jijini Tanga, Wasanii wenzake walipatwa na mshtuko mkubwa, ilibidi kundi zima la VITUKO SHOW litie tim Eneo la tukio na kumkuta masele mzima wa afya,Ukweli ni kwamba masele 
alimgonga mtu baada ya kumgonga mtu
alisogeza gari mbele ili apaki aongee na raia mara gafla mawe yakaanza kurushwa na watu asiowatambua! kwa kuokoa uhai

wake akawasha gari na kuwatoka raia wenye hasira kali mara akajikuta amemgonga mtu mwingine ambaye kwa bahati nzuri hakuumia, pale ndipo raia walivamia gari la masele na kulipiga mawe wakapora simu hela na baadi ya vitu vilivyokuwemo kwenye gari ilifikia hatua mtu mmoja asiejulikana alichoma kisu tairi la gari la masele na kulitoboa toboa!
 wengine walipiga mawe kioo pamoja na taa za nyuma, na kutaka
kumuua. Jeshi la police lilitia tim eneo la tukio na kumchukua masele mpaka kituo cha police Mabawa, Mpaka sasa masele yuko poa.

MREMA AKABIDHI URAIS KWA LOWASSA MWAKA 2015...!!!


Augustine Mrema (kushoto) na Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema amesema biashara ya kugombea urais mwaka 2015 haiwezi kamwe na ametaka ifanywe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Mrema alisema hayo jana kabla ya harambee ya Saccos ya Walimu wa Wilaya ya Moshi Vijijini, iliyoongozwa na Lowassa katika uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Alisema kugombea urais mwaka 2015 ni biashara kubwa kwake kwani amezoea kufanya biashara ndogo ya rejareja yaani ubunge na kumwomba Mungu mwaka huo ufike kwani atakuwa tayari kumwunga mkono Lowassa kwenye kinyang’anyiro hicho.
‘’Nasema biashara ya urais ni biashara kubwa kwangu kwa sasa na biashara hiyo namwachia Lowassa na niko tayari kumwunga mkono kwa hali na mali,’’ alisema Mrema

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 15.06.2013

.
.

Friday, June 14, 2013

IJUE HISTORIA YA MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'


Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.

HII NDIO MAKALA YA KWANZA YA LWAKATARE BAADA YA KUTOKA JELA '"MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"

Sina budi kumshukuru sana mwenyenzi Mungu kwa kunitendea mema na zaidi ya yote kunipa uhai na afya hadi sasa. Wanasema “shukuruni katika yote” na mimi nalazimika kushukuru kwa yale yote niliyofunuliwa na kuwa sehemu ya ushuhuda wangu katika maisha niliyobakiza hapa duniani.

Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.

Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;

“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”

SIMBA, YANGA NA SUPER FALCONS KAZI KWAO, ZARUHUSIWA KWENDA DARFUL....!!!

amos

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kukataa kuziruhusu timu tatu za Tanzania, Simba , Yanga na Super Falcons ya visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Kagame, leo hii Serikali imeziruhusu klabu hizo kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiongea na waandishi wa habari kanda ya kati Dodomo asubuhi ya leo amesema wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko yanayoedelea Sudan.

BAADA YA KUPATA TUZO MBILI ZA KILI DIAMOND AMSUTA ‘MGANGA WAKE’

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
STAA anayeng’aa katika Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemsuta mganga aliyejitokeza na kudai kwamba mwaka huu staa huyo hatapata mafanikio yoyote na  atapotea katika fani.
Mganga huyo ambaye alidai utaalamu wake ndiyo uliompandisha chati Diamond alisema  mwaka huu staa huyo hatapata tuzo, atafifia na jina lake litasahaulika kutokana na kukiuka masharti yake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisisitiza kutomtambua mganga huyo na anamshangaa kwa kuwa mwaka huu amepata mafanikio tofauti na alivyosema.
“Hebu angalieni, mganga alidai mwaka huu nitafutika katika fani, mbona nimepata tuzo mbili kwenye Kil na nimechaguliwa kuwa balozi wa Cocacola na shoo zinajaza kinoma?” alihoji Diamond.
Aidha, alisema shoo zake bado zinajaza watu wengi huku akiitolea mfano ya mwisho iliyofanyika Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar hivi karibuni iliyojaza nyomi ya watu.
 
NA GPL

WANAFUNZI WA CHUO KIMOJA MKOANI MTWARA WAFANYA PARTY YA KIFUSKA

Pombe  iko  kichwani  hapo....Kila  kitu  kwake  ni  sawa ..

Katika hali isiyokuwa ya kawaida,  wanafunzi wa chuo kimoja maarufu Mkoani Mtwara hivi karibuni walifanya party ya ufuska na kuwaacha watu midomo wazi kwa mambo yaliyokuwa yanatendeka.
Party hiyo ambayo  ilifanyika ndani ya pub moja  mkoani  humo  ilihudhuriwa  kwa  wingi  na  wanafunzi wa chuo  hicho  ambao  wengi  wao  walikuwa  wamevaa  kihasara ...

 Huyu  ni mmoja wa wanafunzi hao aliyefahamika kwa jina la Zaitun ambae anasoma mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

KINANA AMBURUZA KORTINI MBUNGE MSIGWA BAADA YA KUMWUITA JANGILI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.
Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba radhi.
Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Aidha alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014. Katika hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma hizo ameharibiwa tabia yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na kumfanya achukiwe na kudharauliwa katika jamii.
Anadai jina lake na heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu, vimharibiwa na Msigwa kwa nia mbaya, pia kwa tuhuma hizo anazosisitiza kuwa ni za uwongo, licha ya kumsababishia maumivu ya kisaikolojia, pia zimemsababishia hasara ya fedha.
Anadai kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha mboga na mwekezaji kutoka kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha kampuni hiyo kuvunja majadiliano hayo.
Kinana anadai kuwa sababu iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo ni kutajwa kwake na mbunge huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na biashara hiyo.

TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA LANGA NA RATIBA YA MAZISHI...!!


Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini wakianza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi uliopita, leo wametoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
971547_562592510448211_1469657651_n
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha aliyezungumza na Clouds FM, Langa amefariki leo June 13, saa 11 jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Hata hivyo amesema kutokana na maadili na taratibu za hospitali asingeweza kutoa chanzo cha kifo cha Langa na jukumu hilo ni la ndugu zake.
Hata hivyo taarifa za awali zilidai kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana jioni.
Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni(Anna Peter).

MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2013 NA KAMBI ZA JESHI WALIKOPANGIWA...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 MWEZI HUU

TANGAZO
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.


Zifuatazo  ni  selection  za  kambi  walikopangiwa
 Attached Files

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 14, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...