Augustine Mrema (kushoto) na Edward Lowassa. |
Mwenyekiti
wa TLP, Augustine Mrema amesema biashara ya kugombea urais mwaka 2015
haiwezi kamwe na ametaka ifanywe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa.
Mrema
alisema hayo jana kabla ya harambee ya Saccos ya Walimu wa Wilaya ya
Moshi Vijijini, iliyoongozwa na Lowassa katika uwanja wa Ushirika mjini
hapa.
Alisema
kugombea urais mwaka 2015 ni biashara kubwa kwake kwani amezoea kufanya
biashara ndogo ya rejareja yaani ubunge na kumwomba Mungu mwaka huo
ufike kwani atakuwa tayari kumwunga mkono Lowassa kwenye kinyang’anyiro
hicho.
‘’Nasema
biashara ya urais ni biashara kubwa kwangu kwa sasa na biashara hiyo
namwachia Lowassa na niko tayari kumwunga mkono kwa hali na mali,’’
alisema Mrema
Mrema
kwa kauli hiyo alishangiliwa na umati wa walimu katika uwanja huo na
kusema anamheshimu Lowassa kwa uchapakazi wake uliotukuka.
Alisema
viongozi wa aina ya Lowassa ni wachache katika nchi hii na penye ukweli
“tunapaswa kuusema” hivyo atamwunga mkono mwaka 2015 kwani yeye
atajitoa.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema
na kukumbushia kipindi cha uwaziri mkuu wa Lowassa alikuwa akichukua
uamuzi wa papo hapo wa kujenga nchi.
Makamba
alisema na kueleza kuwa ujasiri wa aina hiyo ya Lowassa, umekuwa adimu
kwa muda mrefu hivyo kusema kitendo cha walimu kumkaribisha Lowassa kama
mgeni rasmi hawakukosea hata kidogo.
‘’Ninaunga
mkono kwa kumkaribisha Lowassa kuwa mgeni wenu rasmi kwani hamkufanya
makosa na mnatakiwa kuendeleza mema ambayo ataanzisha hapa,’’ alisema.
Peter
Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM) alisema bila walimu hakuna
maendeleo nchini hivyo “sote tunapaswa kuwaunga mkono kwa mustakabali
wa nchi na si vinginevyo.”
Serukamba
alisema yanayofanywa na walimu wa Moshi Vijijini yanapaswa kuigwa na
walimu wote nchini kwani ni maendeleo tosha ya kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment