Friday, June 14, 2013

TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA LANGA NA RATIBA YA MAZISHI...!!


Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini wakianza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi uliopita, leo wametoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
971547_562592510448211_1469657651_n
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha aliyezungumza na Clouds FM, Langa amefariki leo June 13, saa 11 jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Hata hivyo amesema kutokana na maadili na taratibu za hospitali asingeweza kutoa chanzo cha kifo cha Langa na jukumu hilo ni la ndugu zake.
Hata hivyo taarifa za awali zilidai kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana jioni.
Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni(Anna Peter).

 Langa alikuwa ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha akiwa pamoja na Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwijage `Witness’ ambapo walitamba na nyimbo kama Unaniacha Hoi na Kiswanglish. Langa alizaliwa Desemba 22, 1985 jijini Dar es Salaam katika familia ya wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.

Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma (Global Publishers).
Wasanii na watu mbali wameendelea kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia ya Langa na kuomboleza kifo hicho.
Joh Makini
Wiki mbili nyuma tulipanga kufanya trak kwa Dunga tukaisogeza mbele kupisha msiba wa Ngwea nakumbuka mpaka session alipanga alhamis aliamplz tumalize msiba lkn kumbe yeye ndio alikua anafata daah! Mara ya mwisho kuongea ni uliponiambia nichek beat kwenye email alaf tuchangie mawazo kutakufuta idea daaah! Baadae tena ukanitext umepata idea mbili platinum ideas tukienda studio tunaua! Sasa umeondoka ghafla mimi na dunga tumebaki na beat tu sasa #RIP LANGA.
 

THE CITY of PHD ‏
DAAAAAAAH MUNGU TUSAIDIE!!MI NIMESHAKOSA AMANI KABISA HAPA NILIPO!!!HAYA NI MAJONZI MAKUBWA!!REST IN PEACE LANGA!!GONE TOO SOON!!DAAAAAH
Nick Mweusi
PopoutKAMA HIZI HABARI ZA LANGA NI KWELI SHOW YANGU NA GNAKO CLUB KAKALA HAiTAfANyIKA. RIP LANGA
Afande Sele The’King
Tunavyotaka sisi, sivyo anavyotaka yeye (Mungu) mapenzi yake ni zaidi.
Mungu akupumzishe pema LANGA KILEO
K Wa MaujanjaSaplayaz
Kapumzike na amani zote hatuta acha kukukumbuka daima
Mad Ice
Oh lord shed light on these dark moments of the Tanzanian Music Industry! Its not even a week since we buried Ngwea and another one is down :( … R.I.P Langa!
Cpwaa
Another Brother, Another Soldier, Another buddy,another talented Tanzanian Hip Hop Artist gone!……bado siamini.. #RIPLanga #BongoFlavaStayCalmAndUnited
Fina Mango ‏
RIP Langa. Pole sana Mama na Mzee Kileo Mungu awake nguvu Kwa wakati huu mgumu
D knob ‏
Rip Langa. Sijui cha kuongea kiukweli Dah.
Nikki Mbishi
Langa unaenda wapi kichaa wangu?Mwanao bado nalia na Ngwea halafu unasepa badala ya kubaki tuanue matanga.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...