Sunday, June 09, 2013

MBUNGE WA MTWARA MJINI AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA VURUGU ZA MTWARA

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo kwenda jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Advera Senso zinaeleza kuwa Murji alikamatwa jana jioni nyumbani kwake maeneo ya Shangani mjini Mtwara.

Kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja ikiwa zimepita siku tano tangu viongozi wanne wa vyama vya upinzani mkoani Mtwara, kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Juni 4, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa hao ni Katani Ahmed Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF, Hassan Uledi (35) wa NCCR Mageuzi na Hamza Licheta (51) wa TLP, wote wakazi wa Mtwara.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa baada ya polisi kumkamata mbunge huyo, walifanya upekuzi katika nyumba yake kwa saa kadhaa na baada ya kujiridhisha walikwenda kupekua na ofisi yake.


“Amekamatwa kwenye saa 11:00 jioni, hata hati ya kukamatwa kwake imeeleza kuwa anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi inayopatikana mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam,” alisema Katibu wa Mbunge huyo, Meckland Millanzi.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 9, 2013

2 b911e

3 21fb8

Saturday, June 08, 2013

WENGI WANACHANGANYA MAMBO, ILA HUU NDIO UHUSIKA WA BIG BROTHER NA FREEMASON

WATU WANASEMA MANENO UUMBA, INAWEZA KUA KWELI AU SI KWELI. JIONI HII WAKATI NIKIZUNGUKA ZUNGUKA NIMEKUTANA NA PICHA HAPO JUU IKIICHAMBUA LOGO MPYA YA BIG BROTHE. KAMA UNAVYOONA HAPO JUU KATIKA PICHA UTAONA KUA LOGO HIYO INAHUSISHWA NA MAMBO YA FREEMASON. UKIANZA NA HILO JICHO PAMOJA NA VITU VINGINE.

 SO KAZI KWAKO KUCHAMBUA PUMBA ZIPI NA MCHELE UPI.

HII NDO NYUMBA YA MASANJA MKANDAMIZAJI ALIYO JENGA KIJIJINI KWAO

Aliyekuwa na Ngwair "M 2 The P" Aongea na Kusema Haya...!!!

 'M 2 the P' ambaye awali naye aliripotiwa kuwa amefariki kabla ya taarifa hizo kukanushwa, alisema jana kuwa hadi sasa hajui nini kiliwatokea.
Msanii huyo alisema kwamba hakumbuki kilichotokea hadi wakazidiwa na kukimbizwa hospitali wakiwa hawajitambui.

Alisema pia bado anajisikia anaumwa hadi sasa licha ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya St. Hellen Joseph ya Afrika Kusini alikokuwa amelazwa.
chanzo:Nipashe
Msanii 'M 2 the P' ambaye alikuwa na marehemu Albert Mangweha nchini Afrika Kusini wakati rapa huyo anafariki na yeye pia kuzidiwa hadi kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, alihudhuria mazishi mjini Morogoro juzi.

MAGARI MATANO YALIYOWAHI KUTUMIWA NA HAYATI BABA WA TAIFA ENZI ZA UHAI WAKE

Leo tupo katika utalii wa ndani kwa kutazama baadhi ya  magari aliyotumia Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za Uhuru na baada ya Uhuru mpaka alipofariki Oktoba 14,1999. Maelezo ya makala haya ni kwa mujibu wa nyaraka zilizopo Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam hasa kuhusiana na magari na miaka ya magari yalipotumika. Fuatana nasi.
1.AUSTIN MORRIS A-40

AUSTIN MORRIS A-40

 Gari aina ya  Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 8, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.

SHOW YA SNURA YAACHA WANAUME MIDOMO WAZI, KWELI MAJANGA


 

Naamini kwapicha hizi uwezi kosa show yake jumapili hii NEW MAISHA CLUB atazindua video yake ya majanga kuwa mjanja kuwa wa kwanza kuiona, atasindikizwa na WEMA SEPETU atakata utepe wa video ya majanga,MIRROR,SAMIR,ALI NIPISHE,TIMBULO,BAUCHA,MENINAH, na MADEE kiingilio 10,000 tu hii show sio yakukosa kabisa.
 

MWIGIZAJI WA KIKE WA BOLLYWOOD “JIAH KHAN” AJIUA IKSA MAPENZI


Muigizaji maurufu ambae ni mmoja kati ya wanadada warembo nchini India anaejulikana kama “Jiah Khan” amekutwa amekufa juzi kwa kujiua baada ya kujua Boyfriend wake ana mwanamke mwingine….

Mama yake na Khan amesema kua alirudi na kukuta mwili wa mtoto wake akiwa ameshakufa huku Police wakiwa bado wanachunguza chanzo cha kifo cha mrembo huyo ila baadhi ya majirani walizungumza na Mtandao wa BBC na kusema kua wanachujua mwanadada Khan alikua na mkwaruzano na BF wake…..

Jiah Khan amefariki wakiwa na Miaka 25 na alijipatia umaarufu mkubwa Inchin india baada ya kuigiza na mkongwe wa tasnia ya movie anaijulikana kama Amitah Bachchan na pia aliweza kuigiza na Aamir Khan na Akshay Kumar kwa wale mnaofatilia Bollywood Movies hakika mnawatambua hawa.

mwili wa Jiah Khan ulipelekwa Hospital kwa uchunguzi zaidi…..


Khan alizaliwa New York na akakulia London kabla ya kwenda Mumbai India na kujiingiza kwenye mambo ya sanaa ya uigizaji wa filamu…

Filamu yake ya Mwisho kuigiza inaitwa Housefull ambayo ilitoka mwaka 2010..

TAZAMA VIDEO YA MAZISHI YAKE HAPA

Popout

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amekiri kuwepo kwa vitendo ngono UDOM.

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amekiri kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na hivyo kukataa mwongozo wa mbunge akisema hali iko hivyo.


Makinda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati Bunge likiwachagua wawakilishi wake katika mabaraza ya vyuo na SADC-PF, ambapo Naibu Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu aliuliza swali hilo la uwepo wa vitendo vya rushwa ya ngono.


Mwalimu alimuuliza mmoja wa wagombea, Murtaza Mangungu (CCM) kuwa UDOM imekithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike kuombwa rushwa ya ngono na baadhi ya wahadhiri wasio waadilifu.

Naibu waziri huyo alitaka kujua, Mangungu ataondoshaje kero hiyo kwa wanafunzi wa kike chuoni hapo, endapo atachaguliwa kuwa mjumbe wa baraza.

Katika majibu yake, Mangungu alisema kuwa atashirikiana na wenzake kuhakikisha wanaondosha kero hiyo kwa wanafunzi wanaofanyiwa vitendo hivyo.

HOUSE GIRL AJINYONGA KISA PENZI LA CHRISTOPHER...!!






Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 
Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi. 
Devotha alikuwa katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua uamuzi huo. 
Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea Njombe kwa mazishi.

Friday, June 07, 2013

NGONO ZAANZA KUTAWALA JUMBA LA BIG BROTHER.....VIDEO YA BOLT NA BETTY YANASWA WAKIFANYA MAPENZI LIVE


Mpaka sasa tayari tumeshuhudia couple 4 za housemates katika Big Brother ‘The chase’ , lakini couple ya mu Ethiopia Betty na mu Sierra Leon Bolt ndio ilikuwa ya kwanza kufahamika katika wiki ya kwanza toka mchezo uanze (May 26).


bolt & betty


Couple ya Bolt na Betty ndio ilikuwa ya kwanza pia ku’kiss kama uthibitisho wa ‘love at first sight’. Baada ya hapo maisha ya mjengoni yaliendelea vizuri huku mapenzi ya ‘love birds’ hawa yakizidi kukua kila kukicha japo waliamua kupeleka mambo taratibu.


Lakini wiki hii inaonekana kiu ya toka (May 26) iliwakaba ‘love birds’ hawa na kuamua kuikata kwa kufanya kile wanachofanya wapenzi wanapokuwa faragha (watu wazima naamini mnanielewa) yes , they did it! Bolt iliifunga nut ya Betty usiku wa manane wakati washiriki wenzao wakiwa wamelala!!


Ikiwa ni sehemu ya kujaribu kuyaokoa mapenzi yao, wiki hii baada ya Betty kutwaa ukuu wa Diamond House (HOH) aliweza kupata mamlaka ya kumuokoa mshiriki yeyote anayekuwa ameingia kikaangoni. 
Hivyo aliitumia nafasi hiyo kuliokoa penzi lake kwa kumuokoa Bolt ambaye alikuwa amependekezwa kuingia kikaangoni, na kumchagua Feza Kessy wa Tanzania aingie kikaangoni badala ya kipenzi chake.


video  mbili  za  uchafu wao...


video
video

TANGAZO KWA WAKAZI WA MBEYA

Nafasi za Kazi na Mafunzo

SIFA:


>>> Elimu ya kidato cha nne au zaidi.
>>> Taaluma ya uandishi wa habari ni added advantage.
>>> Uwezo, ufahamu, utundu, uzoefu, na ujuzi katika matumizi ya "Mitandao ya Kijamii" ndio kigezo kikuu.
>>> Umri miaka 18 na kuendelea.
>>> Uchapakazi, kujituma, creativity na ubunifu katika masuala ya mitandao ya kijamii ni vigezo muhimu.
>>> Awe mkazi wa Mbeya Mjini.


NAFASI ZILIZOPO NI NNE KAMA VIGEZO VITAKIDHIWA.

FIKISHA MAOMBI YA KAZI OFISI YA JIGAMBE (MbeyaCity.com) ILIYOPO KATIKA YA SAE NA ILOMBA OPPOSITE/MKABALA NA MASHOKO BAR.

The Boss lady Huddah Monroe na Prezzo Mapenzi Tele, Diva Aamua Kuweka Picha ya Nusu Uchi Kupoteza Soo

Prezzo akiwa na huddah jana muda mchache baada ya lady boss kutua katika  ardhi ya kenya.. ahahahahahah  prezzo kajiachiajeee!!!
Baada ya huddah kuweka picha yake akiwa na prezzo na kuzua gumzo ndani ya mtandao huo wa twirraa, dada yetu akaamua kuweka picha yake ya.....(sijaielewa sijui AVI na hii ahahahha samahani lakini) ili kupotezea soo hilo..
ahahahahah Sasa bado hatuelewi  kama ile LOVE AT THE FIRST SIGHT IMEISHIA WAPI maana presidente anaongea kwa vitendo tu!! #okeee

Source: Zeddylious blog

HUYU NDO MBUNGE ALIYEHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI KUMI, HILI NDO KOSA ALILOFANYA

 

MBUNGE wa Mbarali, Modestus Kilufi (CCM) amehukumiwa kifungo cha miezi 10 baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kuua, Mbunge huyo (51) alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Oktoba 10 akidaiwa kutishia kumuua Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa, Mbarali, Jordan Masweve.


Kabla ya kusoma hukumu hiyo leo Mbunge aliomba Mahakama impunguzie adhabu, kwani ana watoto watano kati yao wawili wanasoma Chuo Kikuu na wananchi wanamtegemea kuwasilisha matatizo yao bungeni.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite, alisema ameridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Epimack Mabrouk na Griffin Mwakapeje, pia mawakili wa upande wa mashitaka walimwomba Hakimu Mteite kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

"Kutokana na maelezo hayo na ushahidi ulioletwa mahakamani, ninakuhukumu kifungo cha miezi 10" alisema Hakimu Mteite.

Mbunge akihojiwa katika chumba cha mahakama alisema unajuwa siku hizi haki inatendeka pale tu iwapo mwanaCCM ametiwa hatiani, lakini kama ni mpinzani ametiwa hatiani utasikia ooh kaonewa au hii ni hukumu kutoka ikulu, hata hivyo alisema atakata rufaa katika hukumu hiyo

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...