Friday, April 26, 2013

Lema kufikishwa Mahakamani juma tatu

 Lema akiongozana na wanafunzi wa chuo cha uhasibu baada ya wanafunzi hao kumpokea juzi chuoni hapo
Arusha,Tanzania

MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.
Mwanadishi wa Habarimpya.com mjini Arusha anasema kwamba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa ArushaLiberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili" alisema Sabas.
Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo. Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbunge huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.

WEMA AKODI NDENGE KUTOKA DAR KWENDA ARUSHA KWAAJILI YA MAPUMZIKO

 Habari Habari za uhakika zilieleza kuwa Wema na timu ya wafanyakazi katika kampuni yake ya Endless Fame Production, alikodisha ndege ya kifahari kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya mapumziko tangu Aprili 18 hadi 20, mwaka huu.

Ilifahamika kuwa ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na kampani yake tu.

CHANZO CHA YOTE NI DIAMOND

Ilibumburuka kuwa timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.

Ilielezwa kuwa stresi alizokuwa nazo zilitokana na ile ishu ya kudaiwa kurekodiwa akibembeleza penzi kwa aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku mkali huku jamaa akiwa amelala na mpenziwe wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Baada ya kutokea kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza mawazo.
“Unajua ile ishu ilimchanganya sana bidada maana hakutegemea kama Diamond anaweza kufanya kitu kama kile so (kwa hiyo) alikwenda kutuliza akili na kweli sasa hivi walau yupo fresh (vizuri),” alisema sosi wa karibu wa Wema.
 
AINGIA ARUSHA KWA ULINZI MKALI
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege) hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo chetu,

PROFESA LIPUMBA AIPONDA CHADEMA NA KUDAI KUWA NI VINARA WA VURUGU NA HAWANA HOJA

Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya. 


“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.

HII NI BARUA YA WAZI KUTOKA MBEYA ILIYOANDIKWA KWA DIAMOND IKIMPONDA KWA MABAYA ANAYOYAFANYA.

BARUA KWA DIAMOND PLATINUMZ na MAMA YAKE MZAZI mbeya region P.O.BOX 1021 MBEYA 
dear diamond.... 
sina imani we ni mzima wa afya kutokana hasa na mambo unayofanya kiukweliii katika wasanii wakali mpaka kupitiliza hapa tz wew ni mmoja wapo.. napenda sana vibonzo vyako hasa kile cha " nani amenuna nani amenuna eti nani amenuna" najua utakua umemalizia WEMA... katika kila shoo zako unazofanyaga mara nyingi huwa unataja kumheshim sana mama yako mzazi kutokana na malezi aliyokupa toka kipindi kile unauza 
MITUMBA.. lakini saiz unafanya mama wa watu aonekane alizaa toto zinzi ambalo kama limetumwa kuzini na kuumiza wanaume wenzie.. ivi unajua mke anauma kias gani hata kama wanajileta we ni mtu mzima ambaye unatakiwa kupembua mambo.... hasa kuhusu jambo la HILI MBURULA LENZIO UWOZO or SORY I mean UWOYA.. unajua kabisa   kaka yetu NDIKU ambaye anafanya kazi ngumu ya kukabana na wakina NSAJIGWA NFUSO uwanjani ili apate chochte cha kulisha family yake lakini wew bila huruma una ramba asali yake... ivi unajua mtoto wa uwoya "krish" atakopukua njiani kwenda shule wenzie watakua daily wakimuambia " mtoto wa kambo wa DOMO huyo' ivi dear diamond mbna unataka mama yako asipewe heshma sababu ya wew hujui ka unamfanya awe despsd infrnt of da pple... najua hujaelewa coz elimu kwako ni tatizo utampigia wema akufafanulie ila usi mrecord coz anakusaidia ww.... au umea athirika unafanya kusambaza.. hawa wanawake wapo toka enzi za ma dinossaurs,,, mwambie penny akuambie maANA ya dinossaurs.. huu mda unaoangaika na wanawake ungejiendeleza ata kielimu iyo 4m four itakufksha wap.. na wew mama diamond ivi huoni anachofanya mwanao unashindwa kumshauli au unataka uje kumwambia akishaanza kuharisha na kumvisha visepe.. ERIC SHIGONGO naomba ukiiona hii itupie kwenye ijumaa wikienda ili babu yangu wa ileje Ambaye hatumiii fb asome mana kila siku amekua akiipenda nyimbo ya mbagala bila kujua uovu wa aliyeimba kwa leo yatosha ila TACAIDS naamini itakutemblea diamond siku si nyingi kkupa matumizi saHII YA arv

wako shabiki nambA MOJA DUNIA NZIMA....... via mbele kuchungu 
From:http://www.facebook.com/pachito.edd

WASANII WALIPONDA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

BUNGE la Jamhuri la Muungano wa Tanzania limeonekana kuwachosha baadhi ya wasanii kutokana na kukosa hoja za maana za kujadili ndani ya bunge hilo na matokeo yake kuwa kama kijiwe kwa kutumia lugha chafu zilizokosa tija kwa taifa

Kutokana na hali hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa lugha na sera zenye tija wawapo bungeni baadhi ya wasanii wanaliona hilo ni moja ya changamoto inayosababisha watanzania kuzidi kuwa na hari ngumu ya kimaisha kwa kukosa watetezi wenye umakini

Mmoja wa wasanii hao akizungumza na jarida hili Ben Pol alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi  kwenye kujadili hoja na matokeo yake wanashindwa kupata muafaka wa wanayo yajadili

Alisema kuwa bunge limekosa muelekeo na ameacha kulisikiliza bunge hilo kwa sababu ya kukosa mueleko na kujaa lugha chafu za matusi huku wakishindwa kuyajadili yale ya msingi kwa taifa lao

Kutokana na hali hiyo nchi ya Tanzania itaendelea kubaki maskini na vitu kuendelea kupanda bei kila siku huku kipato cha wananchi kuwa duni kwa kukosa watetezi

Alisema kuwa bunge halijafika sehemu nzuri na kuonekana halina tija kwa wananchi wake na hali hiyo linasababisha wananchi kushindwa kupata ukombozi kwa yale wanayoyakusudiwa

Kwa upande wake msanii wa filamu nchini Rose Ndauka alisema kuwa bunge limekuwa si la wastaarabu na matokeo yake wanajadili vitu ambavyo havina tija kwa jamii

Alisema kuwa Tanzania ni nchini ya wastaarabu na wajadili vitu vya ustaarabu kwa kufikia muafaka hali hiyo imekuwa tofauti sasa kwa baadhi ya wabunge kujadili vitu kwa lugha chafu hali inayoshangaza taifa

"Wananchi tumewachagua wabunge huku tukiamini kuwa watafanya hilo tulilowaagiza ila hali imekuwa tofauti na mika mingine baadhi ya wabunge kuanza kujadili vitu visivyo na tija kwa wananchi wao" alisema Ndauka

LEMA ATUMIWA UJUMBE WA VITISHO NA MKUU WA MKOA

Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”

Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

MAGAZETI YA LEO APRIL 26 2013.

.
.
.
.
.
.

Madawa ya kulevya yakamatwa katika basi la ziara la mwanamuziki Justin bieber.


Polisi wa nchini Sweden wamedai kupata dawa za kulevya katika basi linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za kimuziki.
Msemaji wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.

WANAWAKE WAASWA KUUNGANA NA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND

Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !
Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi. Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke"  kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kuielekeza jamii kuishi
kwa kufuata na kuheshimu maadili, lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na Bi. Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi. Penny, kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamamana kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video, vcd, cd pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanywa na mwamuzikiNasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wotewa kitanzania popote pale walipo.

Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke" 
Wanawake wote ambao wamempa like au ad katika mitandao kama facebook kujiondoa mara moja na kogemea kununua jarida au gazeti lolote lile litakalo mpamba mwanamuziki huyo.

GODBLESS LEMA AKAMATWA....POLISI WAVUNJA MLANGO NA KUMTIA PINGU

Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku  wa manane, Mh. Lema alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.

Kukamatwa  kwake  kulikuja  baada  ya polisi  kuvunja mlango na kuingia ndani  na  kuendesha  msako  wa  nguvu  humo  ndani .Vitu  kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police.
 
Wananchi wengi walijitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.

Safari ya Lema  kuelekea  polisi  ilisindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza kumsupport kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa ndani.  Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Baada ya  kumtupa  ndani,polisi waliwafukuza wafuasi  hao wa Chadema  hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo. 
.......

MH. LEMA AMEKAMATWA KUFUATIA KILE KINACHOTAJWA NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUWA YEYE NDO CHANZO CHA VURUGA NA KUZOMEWA KWAE NA WANAFUNZI ALIPOFIKA CHUO CHA UHASIBU NJIRO BAADA YA TUKIO LA KINA MMOJA ALIYEUAWA KWA KUCHOMWA KISU.
source mpekuzi

HUYU NDIO MSHKAJI AMBAYE AMEFUKUZWA HUKO SAUDI ARABIA KUTOKANA NA KUWA HANDSOME KUPITA KIASI

Huyu ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko Dubai ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza (Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
Omar alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika tamasha ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za Ngamia, Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri, na baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa kutokana na mualiko wa msanii wa kike maaruku kutoka Falme za Kiarabu ambaye walihofia angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine wakisema ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao. 

CHANZO : SAM MISAGOBLOG

WATAALAMU WA MAMBO WAMETHIBITISHA KUA HUYU NDO MWANAMKE MREMBO KULIKO WOTE DUNIANI

the most beautiful woman in the world saudi arabia
 
the most beautiful woman in the world
They say beauty is in the eye of the beholder but this type of natural beauty is very exceptional.
Meet the most beautiful woman in the world 2013, Saudi Arabian queen Fatima Zohar-Godabari.
Before now, the beautiful lady is used to covering her whole face with a Niqab but she is ready to show the world what she is made of.

Thursday, April 25, 2013

WIMBI LA MAKAHABA LAZIDI KUONGEZEKA JIJINI DAR, COCO BEACH YAGEUZWA 'GUEST BUBU' NYAKATI ZA USIKU...!!

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai  alivyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha. Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).
BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.
ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.
MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.
MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungw

a alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.
INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea.
Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.

LULU AINGIA MZIGONI RASMI NA KUFYATUA FILAMU YAKE........!!!

HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.

Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.
 

Mara baada ya kutupia picha hizo mtandaoni, watu mbalimbali walimtumia ujumbe kumsifia kwa kumwambia kuwa ana kipaji cha kazi hiyo.

Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo naye alichangia mada hiyo na kumsifu Lulu kwa uwezo wake wa kuigiza.
Lulu amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kupata msala wa kumuua bila ya kukusudia staa mwingine wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka jana, hivi sasa yuko nje kwa dhamana.

Diamond ashindwa kutamba tunzo za Kili 2013, hawa ndio waliotajwa


Msanii bora wa hiphop
Fid Q, 
Joh Makini, 
Kala Jeremiah, 
Profesa J, 
Stamina

Wimbo bora wa Mwaka: 
Dear God Kala Jeremiah,
Leka Dutigite

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...