Friday, March 29, 2013

P FUNK AMCHANA MAKAVU MSANII NAY WA MITEGO

Producer maarufu bongo na mmiliki wa studio za bongo record P funk Majan ametoa makavu kwa watu wanaochonga kuhusu maendeleo yake husasani wale wote ambao wanapiga majungu kuwa mkali huyo amepotezwa na vijana wadogo kwenye soko la mziki bongo.
“Kuna watoto wadogo siku hizi wanakurupuka wanajiona wao baabkubwa juzi kati nikiwa kwenye club moja naskia kiproducer kinachonga kuhusu mimi kenyewe kana sijui nyimbo moja au tatu zimehit mimi nina yimbo zaidi ya 100 ambazo zimehit na hadi akina Mhe Mkapa enzi hizo, wametukubali we utaniambia nini” P funk alifunguka.

Majani amefunguka kuwa kuna watu wanamtafuta chuki ili kumpachika skendo akitolea mfano msanii wa kizazi kipya Ney wa Mitego kuwa haelewi kitendo cha rapper huyo kumtukana kwenye nyimbo yake kulikua na lengo gani kwasababu msanii huyo hamkaribii hata kidogo kwa level zake.

JACK PENTZEL ALONGA KUHUSU KUOLEWA KWAKE

MSANII wa bongo movie 'star 'wa bongo asiyekauka vituko' Jackline Pentzel a.k.a Jack wa Chuzi ameibuka na kuwataka mashabiki wake kuamini ameolewa na hajakurupuka kufanya maamuzi hayo kwani ni jambo ambalo alikuwa akilifikiria kila wakati

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni Jack alisema kuwa anawataka mashabiki kuamini na kutowasikiliza watu wengine wanaotoa maneno ya uzushi juu yake kuwa maamuzi ya kuolewa ameyapanga na ameolewa na mwanaume wake wa siku nyingi hivyo anaamini anachokifanya ni sahihi kwake


Alisema kuwa watambue mwanaume aliolewa naye si mume wa mtu bali ni mchumba wake wa muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja kbala ya kuoa na ndipo maamuzi ya kufunga ndoa yalipokuja kwa kutotaka kuendelea kufanya uzinifu wakati uwezo wa kufunga ndoa walikuwa wanao


"Mimi nawashangaa kwani kuolewa ni kitu gani cha ajabu mpaka watu wasiamini mimi kufunga ndoa nimeamua kuolewa kwa sababu nampenda mwanaume wangu na nilikuwa naishi naye kwa kalibu hivyo tunajuana vizuri sijakulupuka" alisema Pentzel


Akizungumzia sababu za kutotangaza harusi yake alisema ameamua kutofanya hivyo ili kuepusha maneno na vizuizi vya ndoa yake ambavyo vingeweza kuibuka na kupoteza mawazo ya mumewake huyo


Alisema kuwa hakutaka hali hiyo itokee ndio maana akaamua kufanya iwe siri na ya kushutika ili wambaya wake wakose nafasi ya kufanya jambo lolote baya na kwa sasa baada ya harusi hiyo ndio vikao kwa ajili ya kufanya sherehe hiyo vinapangwa

PICHA ZAIDI YA HALI ILIVYO SASA KWENYE JENGO LA GHOROFA LILILOANGUKA KATIKATI YA JIJI, DAR


Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.

BEAKING NEEEEEWZZZZZZZZ!!!!! GHOROFA LIMEANGUKA MITAA YA ILIGANDI K/KOO

Mpaka sasa watu watu 12 wameshapoteza maisha,limedondokea msikiti wa SHIA.
Mpaka sasa eneo la tukio kuna mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na meya,Mmiliki wa jengo hilo bado hajajulikana.Ndani ya jengo hilo kulikuwa na watu wasio pungua 60 wakiendelea na ujenzi.Watu zaidi ya 14mpaka sasa wameshakimbizwa hospitali. Tutaendelea kuwajulisha zaidi.
Chanzo bado hakijajulikana waokoaji wako wanaendelea na shughuli za uhokoaji zinaendelea..
Limeangukia msikiti na ndani kulikuwa na watoto,mpaka sasa watu 10 wameshakimbizwa hospital.Jengo hilo lilikuwa linaendelewa kujengwa lina golofa 16.
              
Picha kutoka K/KOO eneo la tukio. Picha Irene Mwamfupe

UZINDUZI WA TAWI LA YANGA MAREKANI


TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.

TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013 

MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT

ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902

MUDA:  4:00 PM

KWA MAWASILIANO: 
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685

YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAMSHUSHIA PONGEZI WEMA SEPETU..


SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13 alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo.

LEO NI IJUMAA KUU

INAPOFIKA saa tisa alasiri, siku kama ya leo, maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba za ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni siku ya majonzi.

 http://www.topnews.in/usa/files/jesus-crucifixion-full.jpg
Ijumaa Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu baada ya kusulubishwa msalabani yapata zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa kuitangaza kuwa ya mapunziko.

Siku hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristo.

FILAMU YA SISTER MARRY KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE.

Ray amesema kuwa filamu yake ya SISTER MARRY iliyozua kasheshe na viongozi wa kidini kutoka kanisa katoliki hivi karibuni haijazuiliwa kabisa bali ameambiwa arekebishe baadhi ya vipande katika filamu hiyo hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula filamu hiyo itaingia sokoni kila kitu kikikamilika. The film stars Vicent Kigosi(Ray), Irene Uwoya, Blandina Chagula(Johari) and Grace Mapunda.

CAG akabidhi Ripoti ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Kikwete.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Bwana Ludovick Utouh akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).

Thursday, March 28, 2013

Mwanafunzi wa Kidato cha IV Kibaha Sekondari akamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa meno ya Tembo.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo.
Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17.
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari.
Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.
Na.Mo Blog Team

Nelson Mandela hospitalini tena

 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.
Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.

Pengo: Polisi nchini wanafuga uhalifu

 Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amelitupia lawama Jeshi la Polisi kwa kile alichosema kwamba limeshindwa kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Kadhalika kiongozi huyo alihoji ulipofikia upepelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Zanzibar aliyepigwa risasi mwezi uliopita huku akisema, “Siwezi kusema naridhika au siridhiki lakini tulitegema kwamba polisi wangetegua kitendawili cha wauaji wa padri huyo.

MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI

MENEJA wa Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya Fastjet Emma Donovan, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.
Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.
Katuga alidai Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.

Hakimu Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.

Alitaja masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini wawili ambao ni Watanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali.

BREAKING NEWS. MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI AFARIKI DUNIA.

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis (CUF),amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.
jambotz8.blogspot.com INATOA POLE KWA FAMILIA, WABUNGE, NDUGU NA JAMAA WA SALIM HEMED KHAMIS
CHANZO: ITV

KIKWETE ASIMULIA ALIVYOIBA WALI JKT......!!!!

RAIS Jakaya Kikwete amesimulia maisha yake ya jeshini, huku akikumbuka namna alivyokamatwa na mkuu wa jiko (afande ubwabwa) akiiba wali. Rais Kikwete alitoa ushuhuda huo wakati akifunga mafunzo maalumu ya uongozi kwa wabunge na kuzindua mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

Hafla hiyo ilifanyika juzi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha 832 KJ, kilichopo Ruvu, Kibaha mkoani Pwani, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Rais Kikwete aliwakumbusha vijana hao kwamba yeye ni miongoni mwa watu waliochukua mafunzo ya JKT kambini hapo akiwa katika Operesheni Tumaini mwaka 1972.

Rais Kikwete alisema katika mafunzo hayo alijengwa vizuri, ingawa hadi leo bado anakumbuka matukio mawili ya kufurahisha na kusikitisha akiwa kambini hapo.

Alisema tukio la kwanza ambalo hawezi kusahau ni pale alipokamatwa akiiba wali na tukio jingine ni kuhusu kifo cha askari mwenzao aliyefariki dunia baada ya kukanyagwa na trekta.

“Nawashukuru kwa kunialika katika shughuli hii, nimetembelea na kujionea miradi mbalimbali inayoendelea kufanywa hapa kambini.

“Wakati tukiwa kule nilikuwa naangalia kwa makini, hasa nilikuwa naangalia lile bweni letu, sisi tuliokuwa Kombania A mwaka ule, nimepakumbuka ingawa sasa pamekarabatiwa vizuri.


“Yapo matukio mawili ninayoyakumbuka siwezi kuyasahu hadi leo wakati nikiwa hapa kambini…(kicheko) jeshi si mchezo, nawaeleza haya mjue maisha ya jeshi hayana mzaha.

“Nakumbuka namna nilivyokamatwa na bwana ubwabwa nikiiba wali kule katika bwalo la chakula,” alisema Rais Kikwete huku wananchi na askari wanafunzi (kuruta) waliokuwapo wakiangua kicheko.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...