Wednesday, March 13, 2013

MAPOZI" YA LULU MICHAEL AKIWA KITAA.


Lulu back to basics how sweet

MUONEKANO MPYA WA WEMA SEPETU BAADA YA KUZITIA MKASI NYWELE ZAKE



Mrembo na Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu ameamua kubaki natural baada ya kuzinyoa nywele zake. Kupitia Instagram, Wema ameshare picha hizo na kuandika, ‘me apa nimenyoa nywele’. Ingia ndani kusoma maoni aliyoyapata baada ya kunyoa.

Mh. Pinda kubariki Tamasha la Pasaka jijini Dar

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imeshathibitisha kuhusiana na ujio wake kwenye tamasha hilo.

“Tunafurahi kwamba tamasha letu mwaka huu Dar es Salaam mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mwaka jana alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe,” ilisema taarifa hiyo ya Msama.

Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo, ambapo wan je ya nchi ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda.

Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro, Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
 
 

Mbunge wa Bumbuli-CCM na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba Aula World Economic Forum(WEF) Young Global Leader 2013



MOSHI MWEUSI WAFUKA VATICAN KUASHIRIA KUWA BADO PAPA HAJAPATIKANA....


Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye  dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.

Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana  ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita. 

Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.

Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.

Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi  mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Mama Salma Kikwete akitaka kituo cha utamaduni cha Bujora kuhifadhi utamaduni wa mtanzania.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza kituo cha utamaduni cha Bujora kwa kutunza na kuhifadhi  utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo (WAMA) ametoa pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.
Amesema kuwa kituo hicho kimeonyesha mfano wa kuigwa kwani amejionea na kujifunza mambo mbalimbali ambayo hakuwa anayafahamu hapo awali kuhusiana na kabila hilo jambo la muhimu wahakikishe kuwa wanaendelea kutunza utamaduni wao.
Akisoma taarifa ya kituo hicho Padre Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugezi amesema kuwa kituo kilianza mwaka 1954  kikiwa na lengo la kuhifadhi na kuendeleza tunu bora ya maisha ya watu ili waweze kumfahamu Mungu na kuishi kadiri ya mpango wake kwa kutumia utamaduni.
Amesema kuwa wanajihusisha  na shughuli za kutunza  na kuendeleza urithi wa utamaduni wa mtanzania kwani kupitia kituo hicho wameweza kutangaza utalii na utamaduni ndani na nje ya nchi kupitia ngoma , nyimbo na michezo mbalimbali.
Kituo hicho kimekuwa kikiandaa tamasha la Bulabo ambapo Rais Dk. Jakaya  Mrisho Kikwete amekuwa akichangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kukusanya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Mchakato wa kumpata Papa mpya huko Vatican bado hakijaeleweka makadinali leo waingia siku ya pili ya kupiga kura.


Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye  dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.
Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana  ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi  mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican. 

WASTARA AAGWA.............!!!!!


WASTARA Juma amabaye ni mke wa marehemu Juma Kilowoko “Sajuki” Jumpili jioni alisindikizwa na ndugu na jamaa katika uwanja wa ndege wa Kimataita wa Mwalimu Nyerere katika safari yake ya kuelekea Oman.
Wastara ambaye amekwenda Oman kwaajili ya mapumziko ya miezi miwili ikiwa ni pamoja na kumaliza eda ya mumewe alipelekea huzuni nyingi kwa watu waliomsindikiza kuanzia nyumbani hadi Airpot.
Zifuatazo ni picha mbali zilizopigwa nyumbani, barabarani na uwanja wa ndege zikimuonyesha Wastara katika pilika za safari hiyo.

KOCHA WA TAIFA STAR ATAJA TIMU YA KUIVAA MOROCCO



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.

Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Tuesday, March 12, 2013

ROSE NDAUKA KUANZISHA KIPINDI KATIKA TV CHINI YA ‘NDAUKA ENTERTAINMENT'

Muigizaji wa filamu aliyepo kwenye orodha A kwenye tasnia ya filamu nchini, Rose Ndauka anatarajia kuanzisha kipindi chake cha televisheni alichokipa jina la 'The Family Talk'
Rose amesema dhumuni la kipindi hicho kitakachoandaliwa na kampuni yake ya Ndauka Entertainment ni kuzungumzia masuala mbalimbali ya kifamilia yakiwemo matatizo yanayozikumba.
ROSE NDAUKA
“Nimechagua kuielimisha jamii kuwaburudisha na vitu vingine, kwahiyo nimeona nikianzisha TV show ambayo itakuwa inahusu familia, inaongelea matatizo ya familia kwa ujumla pia itakuwa ni njia moja ntakuwa nimeweza kuielimisha jamii na inawezekana wakaweza kuburudika kwenye hicho kipindi pia,” amesema Ndauk

Kamati mpya za Bunge kuanza kazi Machi 18, 2013


 Kamati za Kudumu za Bunge zinatarajiwa kuanza  kukutana na kutekeleza majukumu ya Kibunge  jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 18, ikiwa ni kipindi cha nusu muhula wa  uhai wa Bunge.
Vikao vya kamati hizo vitaanza mara baada ya kukamilika kwa uundwaji wa Kamati Mpya za Bunge pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati hizo utakaofanyika Ijumaa ya wiki hii.
Mwishoni mwa mkutano wa 10 wa Bunge mwezi uliopita, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza mabadiliko ya kamati hizo, huku akiifuta Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitafanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo itaendelea na jukumu lake la msingi la kuchambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pia kwa Serikali Kuu.
Kamati nyingine iliyofutwa ni ile ya Sheria Ndogo, huku zikiundwa kamati mpya tatu na kuzifanyia marekebisho nyingine ikiwa ni hatua ya kuimarisha usimamizi wa Bunge kwa shughuli za Serikali.
Katika mchakati huo, kamati mpya zilizoundwa ni Kamati ya Bajeti, Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo imetenganishwa kutoka katika Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  
Kwa mujibu wa Spika Makinda, majukumu ya kamati mpya ya bajeti ni kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya Serikali na sera za fedha pamoja na kuainisha na kupendekeza vyanzo vya mapato ya Serikali na kufuatilia mwenendo wa uchumi.
Kamati hiyo ya bajeti pia imepewa jukumu la kushauri kamati nyingine zote kuhusu bajeti.
Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Ofisi ya Bunge iliyolenga kuufahamisha umma juu ya kuanza kwa kamati hizo nyeti za Bunge.
“Baada ya uundwaji wa kamati mpya na uchaguzi wa wenyeviti, litafuatia zoezi la wajumbe wapya wa Kamati hizo kuhudhuria semina maalumu kuhusu majukumu ya Kamati pamoja na kupitia mpango wa kazi (work plan)” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema ratiba iliyopo inaonyesha kuwa kamati za kisekta zitatembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyokasimiwa na utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2012/13 kuanzia Machi 18 hadi Machi 23 mwaka huu.
“Tarehe 25 mwezi huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitoa muhtasari kwa wabunge wote kuhusu mkutano wa 11 wa Bunge ikifuatiwa na kupokea Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2013/14 kutoka serikalini pamoja na mwongozo wa matazamio na upeo wa Bajeti ya 2013/14,” iliongeza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema kuanzia  Machi 26 hadi Aprili 5, Kamati za kisekta zitafikiria na  kuchambua maombi mapya ya fedha kwa Bajeti ya Wizara zilizo chini yake kwa mwaka wa fedha 2013/14 ikifuatiwa na Serikali kufanya majumuisho kwa kuzingatia ushauri wa kamati za kisekta.
Iliongeza taarifa hiyo kuwa baada ya shughuli hizo za kamati, Mkutano wa 11 wa Bunge ambao ni Mkutano wa Bajeti utaanza mjini Dodoma Aprili 9.
“Mzunguko wa Bajeti unakusudiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni, 2013 ili kuipa Serikali muda wa kutosha kutekeleza majukumu yake,” ilibainisha taarifa hiyo.
Kutokana na mabadiliko hayo, taarifa hiyo iliwataka wabunge kufika Dar es Salaam keshokutwa ili kuanza shughuli za kamati mapema kama zilivyopangwa katika ratiba mpya.

Je, wamjua mwanamke mwenye miguu mirefu zaidi Duniani? Huyu hapa.........!

Svetlana Pankratova pichani ametajwa kama mwanamke mwenye miguu mirefu kuliko wote duniani kwa mujibu wa Guinness world Records.Mwanamama huyu anatokea Russia ana umri wa miaka 41.

ANGALIA PICHA YA MUUWAJIA ALIYE MUUA PADRI EVARIST MUSHI

Name:  killer.jpg
Views: 0
Size:  11.8 KB

POLISI WASAMBAZA MCHORO WA ALIYEMUUA PADRI MUSHI

                                  Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa 
MWANANCHI
Polisi Zanzibar imesambaza picha ya mchoro ya mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki mwezi uliopita. Mchoro huo uliosambazwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, unamwonyesha mtu aliyevaa kofia ya baraghashia. Katika taarifa hiyo, Polisi ilisema kwamba mtu atakayesaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo atazawadiwa Sh10 milioni... “Mwananchi yeyote ambaye anamjua mtu aliyefanana na mchoro huo atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi na iwapo atakuwa ndiye mhusika
atapewa zawadi hiyo.”
Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa hakupatikana jana kutoa maelezo zaidi juu ya hatua hiyo, lakini Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Abdallah Hanna alithibitisha kuwa taarifa hiyo imetoka Polisi.
Hata hivyo, Kamanda Hanna hakuwa tayari kutoa ufafanuzi zaidi kwa maelezo kwamba upelelezi wa suala hilo unafanywa na Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Kuuawa kwa Padri Mushi lilikuwa tukio la tatu kubwa la kushambuliwa kwa viongozi wa dini baada ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Soraga na kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki.
Kitendo cha kutoa picha hiyo ni hatua kubwa katika upelelezi wa kifo cha Padri Mushi, ambacho kilitikisa visiwani Zanzibar.
Pia hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kutua kwa maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), ambao wanasaidiana na Polisi wa Tanzania kuchunguza tukio hilo.
FBI wana kawaida ya kutumia picha na michoro pale wanapochunguza matukio makubwa ya uhalifu au ugaidi.

Mathalan, pale wanapotaka kupeleleza kwa kutumia michoro ya sura za wahalifu wasiowafahamu, hufanya mahojiano na watu waliokuwapo kwenye tukio na wakati wakipata maelezo hayo, huwa na wataalamu wao wa uchoraji karibu ili kujaribu kutengeneza sura za watu wanaotafutwa.

FBI walikuja nchini baada ya kualikwa na Serikali ya Tanzania ambayo inataka kujua chanzo cha vitendo vinavyotishia maisha ya viongozi wa dini huko Zanzibar.
Hii ni mara ya pili kwa FBI kufanya kazi Tanzania baada ya mwaka 1998 walipokuja kuchunguza kulipuliwa kwa bomu kwa ubalozi wa Marekani.

Bunge, CHADEMA hapatoshi................!!

Bunge limeingia katika mzozo mwingine na Chadema baada ya kudaiwa kutoa ripoti polisi likitaka wabunge 28 wa upinzani waitwe ili wahojiwe katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na fujo zilizotokea bungeni Februari, mwaka huu. Hata hivyo, chama hicho kikuu cha upinzani kupitia kwa 
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, kimepinga hatua hiyo kikisema kamati hiyo haipo kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya 113(7) kwa kuwa imemaliza muda wake tangu Februari 8, mwaka huu na Spika hajaunda nyingine. 

Hata hivyo, madai hayo ya Lissu yamepingwa vikali na Naibu Spika, Job Ndugai ambaye amesema kamati hiyo pamoja na nyingine mbili za Uongozi na ile ya Kanuni zinatambulika mpaka zitakapoundwa nyingine... “Hizo tatu ni ‘ongoing’ (zinaendelea) zisipokuwapo, basi Bunge hakuna.” 
Mvutano huo ni wa pili katika siku za karibuni baada ya ule uliotokea katika Kikao cha Bunge la Februari baada ya Wabunge wa Chadema kuzua tafrani zilizosababisha kukatishwa kwa kikao kimoja cha Bunge hilo. 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Lissu alisema yeye na wabunge wenzake wapatao 28 watafika mbele ya kamati hiyo lakini wamekubaliana kuwa hawako tayari kuhojiwa nayo.
Mbali ya Lissu, jana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma alisema wabunge wa chama chake hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo. 
Lissu alisema njia iliyotumika kuwaita mbele ya kamati hiyo kwa kupitia polisi ni kinyume na utaratibu.
“Utaratibu uliotumika ni haramu kwa kuwa polisi ndiyo wametumika kutujulisha kwamba tunatakiwa tufike mbele ya kamati hiyo, kutumiwa ujumbe wa polisi si sawa kwani utaratibu wa Bunge unajulikana,” Lissu alisema na kuongeza: 
“Kamati iliposema bungeni kuwa mimi na wenzangu watatu ni vinara wa fujo ilituhukumu tayari, hivyo kisheria wale wengine waliobaki walikuwa hawana makosa kwa mujibu wa sheria zetu.” 
Ilidaiwa kwamba Ofisi ya Bunge iliiandikia Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kutaka kuwaelekeza makamanda wake kufikisha taarifa hizo.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema hakuwa na taarifa hizo na kuahidi kufuatilia. 
Alipoulizwa kuhusu wabunge hao kuitwa kwa kutumia polisi, Ndugai alisema hakuwa na taarifa hiyo na kuelezea wasiwasi kwamba suala hilo limefikia hatua hiyo.
“Sidhani kama imefikia huko (kutumia polisi kuwaita wabunge), kwani kamati ina utaratibu wake wa kumwita mtu yeyote hata asipokuwa mbunge, kwa kweli sijui na sifikirii kama watakuwa wamefikia huko,”alisema Ndugai. 
Mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kumpigia simu Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kumpa wito wa kufika mbele ya kamati hiyo ya Bunge na pia alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu (OCD), kuwapa taarifa Mbunge wa Karatu, Israel Natse na Mbunge wa Viti Maalumu Cecilia Paresso. 
SOURCE::MTANZANIA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...